Ushauri juu ya biashara ya kitimoto

Ushauri juu ya biashara ya kitimoto

Hiyo biashara sio ya kuuliza, ni wewe tu na pesa zako uanze kupiga hela. Cha msingi ni kuwepo kwenye pilika pilika za watu,ila hapo pa kutokuwepo kwa vinywaji vikali ndipo utakapokosea,maana mdudu mwenzie "ngumu kumeza"

Daaa! Asante mkuu, ngoja nijilipue kujaribu si kushindwa!
 
Habarini wana JF,

Mimi nina wazo hapa kuhusiana na biashara ya Kitimoto. Labda nifafanue vizuri kuhusiana na hii biashara yani ni nanunua nyama ya ngurue kwa wachinzaji halafu ninakuwa na kibanda kwa ajili ya kuipika au roasting kwa ajili ya watumiaji.

Location ya Biashara naifanyia Dar es salaam.

Napenda kuuliza labda mwenye experience na hii biashara yupo tuweze peana mawazo na changamoto mbalimbali zinazohusiana na hiyo biashara.

Asante
 
Hakuna namna, nenda kwa wanaokaanga kitimoto kawaulize maswali ya msingi, wapi wanapata nyama, kilo wananunua sh ngapi, n.k
 
Wadau kuna hili wazo la biashara ya kununua nguruwe huko Morogoro kuchinja na kuleta hapa Dar, ofcourse itahitaji uwe na order kwenye vituo vya kuuzia nyama ya nguruwe, kwenye mabaa na watu binafersi.

Unanunua nguruwe wa 100 kg kwa TZS 300,000/- unachinja na kuondoka na nyama fasta hadi Dar unaanza kusupply. Unaweza beba wawili hadi wanne kutokana na usafiri unaotumia na maandalizi uliyoweka.

Kama wapo wadai ambao wanaielewa hii biashara mazuri na mabaya mnijuze tafadhali.

Samahani wa wadau ambao hii ni haramu kwao.

Natanguliza shukrani.
soko ni tatizo kubwa sana dar es salaam, kama unabiahsara kubwa lazima upitie kwa middle men, hao watanunua nguruwe wako kwa 5000 hadi 6500. tatizo lingine nililoliona dar kwa wale wanaosafirisha nguruwe wakiwa hai, ukishamfikisha dar kwa watu wenye mabanda na machinjio wanafanya udanganyifu kwenye mizani yao na wakati wa kuchinjwa wanakatia mabegani ili sehemu kubwa ya nyama ibakie kama sehemu ya kichwa maana ujira wa wachinjaji ni kuwaachia kichwa na miguu. jamani naona kuna tatizo kubwa sana la nguruwe sasa hivi. lakini changamoto hii wadau tuine kama fursa kwa kufiria kufanya packaging au kusindika na kufanya biashara nje ya nchi. kama kuna mtu anajua wapi tunawweza kupata soko la uhakika la nguruwe aniibox ili tufanye biashara ninanguruwe wengi tatizo soko la uhakika
 
Hii nzuri mkuu go ahead cha kuzingatia eneo ukikosa mtu wa kukushauri kuhusu hii biashara njoo nikuelekeze nijuacho
 
Wakuu,

Nampango wa kufungua sehemu kwa ajili ya kuchoma/kuroast kitimoto. Kwa ambaye anauzoefu wa biashara hii naomba ushauri tafadhali hususani kwenye vitu vya muhimu kuzingatia kabla ya kuanza na baada ya kuanza hii biashara.

Binafsi ninampango wa kufungua sehemu ambayo siyo bar ila ni karibu na taasisi ya elimu yenye wanafunzi wengi. Ugali, Ndizi, Kitimoto, vinywaji baridi ndivyo natagemea kuviuza (Pombe haitakuwepo).

Natanguliza shukrani.

View attachment 448509
MKUU,ULIFANIKIWA?
 
Habari ya asubuhi wanajamvi

Katika harakati zangu za kuongeza kipato hasa kwa kuzingatia ugumu wa maisha ulivyo hivi sasa, nimevutiwa na biashara ya kufuga kitimoto kwa ajili ya kuuza ambayo nasikia inalipa sana.

Nimeandaa shamba tayari maeneo ya Kongowe lakini sina uhakika juu ya gharama halisi ya kuwakuza wanyama hao hadi kufikia maturity.

Naomba ushauri wenu juu ya hili. Nitaappreciate kama nitapata mchanganuo kuanzia vyakula madawa na gharama za kuwaingiza sokoni.

Napenda kuanza na nguruwe kumi wa majaribio.

Msaada wenu please!
MKUU,ULIFANIKIWA
 
Habari wakuu,

Mimi ni kijana mjasiriamali mwenye jiko la kupika kitimoto Kimara. Ninahitaji kupanua biashara yangu, yaani nifungue jiko lingine maeneo ya kimara mpaka mbezi mwisho. Hivyo ninaomba msaada kama una bar au unamfaham mtu mwenye bar eneo lililochangamka na anahitaji mtu wakufungua jiko. Please niPM

Natanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu...mimi ni kijana mjasiriamali mwenye jiko la kupika kitimoto kimara...ninahitaji kupanua biashara yangu, yaani nifungue jiko lingine maeneo ya kimara mpaka mbezi mwisho. Hivyo ninaomba msaada kama una bar au unamfaham mtu mwenye bar eneo lililochangamka na anahitaji mtu wakufungua jiko...please ni pm

Natanguliza shukran

Sent using Jamii Forums mobile app
Astaghfirullah

sent from my Samsung S9 plus using jamiiforums mobile application.
 
Habari wakuu...mimi ni kijana mjasiriamali mwenye jiko la kupika kitimoto kimara...ninahitaji kupanua biashara yangu, yaani nifungue jiko lingine maeneo ya kimara mpaka mbezi mwisho. Hivyo ninaomba msaada kama una bar au unamfaham mtu mwenye bar eneo lililochangamka na anahitaji mtu wakufungua jiko...please ni pm

Natanguliza shukran

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa Uungwana zaidi mwisho wa maelezo yako ungeomba radhi kwa Waislamu waliopo humu ambao hiyo kitu ni ' haram / mwiko ' Kwao ili wasikwazike na huu uzi wako. Huu Mtandao siyo tu wa Wakristo Mkuu hivyo ' busara ' kubwa mno inahitajika pale unapotaka kuwasilisha jambo ambalo lina sura mbili hasa ya Kimtizamo na ya Kiimani.

Nikutakie tu kila la kheri Mkuu katika Biashara yako hiyo ya Ng'ombe Katoliki / Ngurumwe / Kitimoto / Noah / ARV.
 
We kama mtakatifu....usingeifungua hii thread.....sahizi ungekua unahubiri huko mtaan kwenu
Wajina lolo123 na Mimi ni lolowapi. Usijali pamoja mkuu.

sent from my Samsung S9 plus using jamiiforums mobile application.
 
Back
Top Bottom