Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Mkuu achana na biashara za bodaboda zitakuua na presha tu kwanza unamkabidhi MTU kesho hakawii kukuambia ameibiwa uanze kuhangaika na police pia MTU unaweza kumuamini ukampatia kesho akafanyia tukio LA ujambazi ikakuhusu wewe na bado zina matukio mengi sikushauri ukikosa ushauri Wa biashara ambayo unaihitaji kuifanya ni bora upite kwenye depot za vinywaji vya jumla omba kuonana na mmiliki utapata usaidizi achana na biashara kichaa za bodaboda utatupa hela zko kwa wanyoa viduku hao
 
Mkuu achana na biashara za bodaboda zitakuua na presha tu kwanza unamkabidhi MTU kesho hakawii kukuambia ameibiwa uanze kuhangaika na police pia MTU unaweza kumuamini ukampatia kesho akafanyia tukio LA ujambazi ikakuhusu wewe na bado zina matukio mengi sikushauri ukikosa ushauri Wa biashara ambayo unaihitaji kuifanya ni bora upite kwenye depot za vinywaji vya jumla omba kuonana na mmiliki utapata usaidizi achana na biashara kichaa za bodaboda utatupa hela zko kwa wanyoa viduku hao
Ahsante Mkuu kwa ushauri wako
 
Habari mkuu,niliwahi kupitia nyuzi fulani huko nyuma juu ya biashara ya soda kwa ujumla,vipi mdogo wako alieendelea maana nilikaa kimya kusubiri mrejesho wa mtu aliyekuwa ameeomba ushauri kama alijaribu au aliibadilisha maamuzi hakurejea,hebu nifahamishe anaendeleaje jamaa yako? na ikibidi ningependa kupata mawasiliano naye maana nina pesa kiasi fulani nafikiria kuifanya hiyo biashara.
Kakimbia nini
 
Ni dhahiri kwamba wajasiriamali wengi wamekuwa wakijiuliza ni njia gani wazitumie katika kuanzisha,kukuza ama kuboresha biashara zao za kuuza vinywaji ili wapate kunufaika na faida kubwa.

Kama wewe pia ni mmojawapo kati ya wajasiriamali wanaotafuta mafanikio makubwa kwa kufanya biashara ya namna hii utakuwa umewahi kujiuliza maswali kama haya;

Je, mtaji wa biashara hii (bar) ni kiasi gani?
Mbona baa ya huyu inalingana na ile kwa mwonekano lakini yule anamafanikio zaidi kuliko huyu?
Nitapajaje wateja wengi kila siku?
Majibu ya maswali yako yote ya kwanini na kivipi ni rahisi tu, zifuatazo ni mbinu zinazoweza kukuwezesha kufanikiwa sana katika biashara yako ya vinywaji au 'BAR'.

1. Fanya Maandalizi ya awali {Weka nia na malengo ya biashara yako (Ni vema Ukiandika)
Ili kufanikiwa katika biashara hii kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote,kitu cha kwanza kufanya ni kuweka nia na malengo au matarajio yako baada ya muda fulani. Kwa mfano, lengo lako la kwanza linaweza kuwa baada ya miezi sita, biashara hii iwe imekuzalishia faida kubwa inayoweza kutosha kuwa kama mtaji wa kufungua biashara nyingine n.k.
Ni lazima pia kuainisha mahitaji yote yanayohitajika kuanzisha biashara yako ikiwemo gharama ya ujenzi, malipo ya wahudumu (kwa miezi sita ya mwanzo), jinsi ya kufanya malipo, Gharama za bidhaa (vinywaji), friji, vyombo na samani za kukalia wateja.

Umakini wa hali ya juu unahitajika katika kufanya upembuzi yakinifu wa gharama za mahitaji ya biashara na muda wa kutosha pia unahitajika ili kupata bei sahihi.

2. Jiandae kiuchumi
Baada ya kufanya maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kufahamu kiasi cha pesa kinachohitajika ili kuanda biashara bila mawaa yoyote, sasa unaweza kujiandaa kiuchumi kwa kukusanya taratibu na kudunduliza pesa kwa ajili ya kufungua biashara (bar). Kama pesa ipo tayari ni vema kuihifadhi vyema na kuhakikisha haiingiliani na matumizi mengine.

3. Chunguza eneo unalohitaji kufanyia biashara

Eneo unalohitaji kuweka bar yako linanakiwa kuwa sehemu ambayo imezungukwa na wahitaji wa aina ya vinywaji unavyotaka kuuza. Kwamfano, eneo liwe sehemu ambayo ni rahisi watu kuhitaji kuja kupumzika baada ya kazi au kukutana na marafiki na sio karibu na Makanisa wala Misikiti au eneo lolote ambapo unaweza kuwakera watu wenye misimamo tofauti ya kiimani.

4. Jenga Bar yako kwa jinsi ya kumvutia macho ya mteja (kistarehe)
Wateja wengi hupenda bar yenye mandhari mazuri ya kuvutia macho ikiwa ni pamoja na usafi wake na mpangilio wa counter, maeneo/vyumba vya kunywea na sehemu za starehe nyingine kama 'pool table' na Muziki/Tv. Vyoo pia vinatakiwa kuwa visafi muda wote ili kuvutia wateja kuendelea kuja katika bar yako kila watakapohitaji kunywa.

5. Ajiri wahudumu wenye mwonekano na lugha nzuri ya biashara
Kufanikiwa kwa Biashara kunategemea sana mahusiano kati ya wateja na watoaji wa huduma. Wahudumu wa Bar yako wanatakiwa kuwa wenye mwonekano na lugha nzuri kwa wateja, wasafi,wakarimu na wasiowahi kukasirika wakati wa kuwahudumia wateja. Wahudumu wenye sifa zilizotajwa hapo juu wanafaa na ndio hitaji la wateja wako wengi kama si wote.

6. Hakiki hesabu za mauzo ya kila siku
Unatakiwa kufanya hesabu za mauzo yanayokusanywa kila siku na kufahamu aina za vinywaji vilivyonunuliwa (kila aina kwa idadi yake). Uhakiki wa hesabu za mauzo ya kila siku yatakupa wastani wa mauzo ya kawaida kila siku, kwa wiki,mwezi na mwaka. Yanakupa pia uwezo wa kukadiria mauzo ya chini kabisa (minimum) na mauzo ya juu kabisa (maximum) kwa siku. Hii inakusaidia wewe kuweka malengo na faida unayoipata katika biashara yako.
Ni vizuri kuweka rekodi ya kila mauzo kwa maandishi ili kurahisisha tathmini yoyote inayoweza kufanywa kwa minajili ya kuboresha biashara.

7. Chunguza vitu wanavyopenda na vinavyowachukiza wateja wako
Ni rahisi kufahamu wateja wanapenda nini na wanachukia nini. Kwa upande wa vinywaji,ni wazi kuwa vile vinywaji vinavyowahi kuisha kuliko vingine ndivyo vinapendwa na wateja na inabidi viwepo vingi vya kutosha. Kuhusu ubora wa huduma, unaweza kuongea na wateja wako (wenye busara) moja kwa moja ili kutoa kero zao ili zile zinazorekebishika zirekebishwe maramoja ili kuepuka kupoteza wateja ambao ndio muhimiri wa biashara yako.

8. Epuka urafiki na mikopo kazini

Hii inawahusu wote, wewe mwenye bar, meneja na wahudumu. Biashara nyingi zinakufa au hazizai matunda tarajiwa kutokana na urafiki na mikopo mingi. Katika bar yako ni vema ifahamike kwa wote kuwa Ofa na mikopo isiyo na ulazima sio njia sahihi za uendeshaji wa biashara. Weka taratibu za wazi kuhusu kukata kwenye posho,malipo au mshahara ya mfanyakazi yeyote ambaye kwa uzembe wake mwenyewe au makusudi amesababisha upungufu katika mauzo ya kawaida ya kila siku.

9. Ubunifu na upekee katika biashara ya 'Bar' ni muhimu

Jitahidi kuwa na ubunifu wa pekee ili kufanya biashara yako kuwa tofauti na wengine. Kwa mfano, unaweza kuandaa tamasha dogo la muziki, urembo au vichekesho katika bar yako ambapo kiingilio chake ni kununua ki/vinywaji tu. Huu au ubunifu mwingine wowote utakukuzia biashara yako kwa kasi kubwa kama utakuwa makini kuwa utekelezaji wa ubunifu usigharimu zaidi ya faida unayoweza kupata.

10. Pokea ushauri na maoni kutoka kwa watu wengine

Unatakiwa kuacha masikio yako wazi kwa ajili ya kupokea kila wazo litakalolenga uboreshaji wa biashara yako wa Bar kutoka kwa wazoefu wa biashara ya namna hii au hata washauri wengine. Kuwa makini pia katika kutekeleza ushauri unaopewa kwani si wote wanaokupa uashauri wanakutakia mema katika mafanikio yako na wala si wote wanaokutakia mabaya katika biashara yako.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi kama umejirudia kutoka kitambo. Nzuri hii ina toa mwangaza wa biashara.
 
Safi sana mkuu

Hii biashara nitaifanya hapa mjini!

"mwanaume mashine"
 
Hapo kwenye wahudumu sasa, wawe wenye vyura vya uhakika kibongobongo utashangaa unajaza wateja ile mbaya...nilikuwa chuo kimoja nasoma kukawa na stationery mbili, moja kuna mhudumu mama mtu mzima na nyingine kulikuwa na wadada wawili warembo.. yaani unakuta pale kwa wadada wateja kibao wanaenda kufanyia hapo kazi hata kama ni ndogo tu ya photocopy, mama anakuwa yuko tu nje ameweka kiti chake anaota jua wateja ni wa kuhesabu
 
Habari wadau,

Samahani nilikuwa nataka kujua mwenendo mzima wa biashara ya duka la jumla vinywaji laini kwa kuangalia mtaji, faida zake, hasara na changamoto zake. Mtaji wangu milioni 13.
 
Kwa bei ya jumla faida yake ni kidogo sana .niliwahi kufanya hii biashara coca kwa jumla walikua wananiletea kwa 11000 na pepsi kwa 10900 mimi nauza 11500.faida kama 500.maji uhai carton ilikua 2500 yale litre 1 .mimi nauza 2800,faida kama 300 hivi.angalau kipindi hicho kodi ya TRA tulikua tunapeta. Bor tafuta sehemu kuna watu wengi unatafuta deepfreezer na vijana wako wanakimbiza kwa rejareja.ukifungua kuuza jumla jiandae na TRA wa magu hawajui kama bidhaa yako unapata faida ya 10, hata pipi mashine ya EFD itakuhusu.
 
kwa bei ya jumla faida yake ni kidogo sana .niliwahi kufanya hii biashara coca kwa jumla walikua wananiletea kwa 11000 na pepsi kwa 10900 mimi nauza 11500.faida kama 500.maji uhai carton ilikua 2500 yale litre 1 .mimi nauza 2800,faida kama 300 hivi.angalau kipindi hicho kodi ya TRA tulikua tunapeta.bor tafuta sehemu kuna watu wengi unatafuta deepfreezer na vijana wako wanakimbiza kwa rejareja.ukifungua kuuza jumla jiandae na TRA wa magu hawajui kama bidhaa yako unapata faida ya 10,hata pipi mashine ya EFD itakuhusu

Ahsante kwa ushauri na maelezo mazuri mkuu
 
Back
Top Bottom