Ushauri kuhusu biashara ya ushonaji wa nguo na upatikanaji wa vifaa vyake

Ushauri kuhusu biashara ya ushonaji wa nguo na upatikanaji wa vifaa vyake

Wanazengo, Mimi nilikuwa na shida ya fundi cherehani/ nguo. Wapi naweza kuwapata au Kama mtu anaweza niunganisha na mmoja?
uko mkoa gani mkuu kama hutojali niambie pia unataka kufungua biashara ili nikuunganishe
 
Habari za wakati huu

Wakuu nakuja mbele yenu mnipatie msaada wa mawazo, ninafikiria kufungua duka/frem ya kushona nguo za akina mama na watoto (me na ke). Naamini mavazi ya akina mama na watoto yanavalika sana kwa mfano kipindi cha sikukuu, sherehe n.k

Kifupi nataka kuwa fundi nguo niwe na kiofisi changu nifanye kazi na Mungu akinipa nguvu niajiri watu au hata partneship tufanye kazi.

Tukiachana na ujuzi, sijui ni vitu gani hasa vya msingi kua navyo (mashine zipi), wapi nitavipata na bei zikoje, pia malighafi (vitambaa) nitapata wapi kwa unafuu.

Nishaurini lolote linalohusiana na hii biashara wakuu.

Najua humu kuna wazoefu wa hizo biashara tafadhali nisaidieni niweze kujiajiri.
 
Naomba kujua chuo au mahala pazuri ambapo wanafundisha fani hii ya kushona.Gharama zake zikoje na mafunzo huchukua muda gani?Natanguliza shukrani.
 
Wakuu natumaini kwema,

Nina ndoto yangu ya kujihusisha na ushonaji mapema mwakani. Nina uhitaji wa mtaalamu anayeifahamu hii biashara vizuri anielekeze machache kabla kuingia kwenye risk.

Pia natanguliza shukrani kwa anaejua upatikanaji wa hizi mashine kwa maana ya aina na model zake;
1. Overlock machine
2. Straight machine
3. Flat lock machine
4. Hand knitting machine for sweaters
5. Tshirt printing machine (digital)
6. Embroidery machine
7. Fabric cutting machine
8. Button hole machine
9. Button attach machine

Nashukuruni sana.
Kwa mawasiliano namba ni 0757528827
Mrejesho tafadhali. Ulifanikiwa? Kama ulifanikiwa, tunaomba utuwekee bei ya hivyo vitu na wapi ulinunulia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naomba mwenye ujuzi wa biashara ya kusona nguo aniambie abc zake maana nataka nichukue frem mahali , kisha nitafute mwanaume na mwanamke wanaojua kushona na kudisigne vizuri tuanze kazi.

Binafsi sijui kushona ila nitakuwa nafanya marketing na kusupervise.

Naombeni msaada tafadhali
 
Back
Top Bottom