Ushauri kuhusu biashara ya ushonaji wa nguo na upatikanaji wa vifaa vyake

Ushauri kuhusu biashara ya ushonaji wa nguo na upatikanaji wa vifaa vyake

Habari wanabodi, nimepata na kuvutiwa na wazo la kufungua karakana na kufanya biashara ya kutoa huduma za ushonaji wa nguo.

Lakini binafsi sina ufahamu juu ya seti za vyerehani zinazohitajika na aina/chapa inayofaa kibiashara na gharama za hizo cherehani, kikubwa nilichosikia kutoka kwa watunga sera ni kwamba vyerehani vi4 ni kiwanda [emoji23](Nakubaliana nao kwa maana ya skeli ndogo).

Hivyo kutokana na kutojua huko nimeonelea ni vema nikiwashirikisha ili kupata msaada kwa sababu naamini hapa ni nyumbani kwa wabobezi wa masuala mbalimbali na mimi nitaambulia chochote kitu. Natanguliza shukrani na karibuni kwa A,B,C ...!.
 
Tafuta mafundi uwaulize watakupa ukweli cherehani zinahitajika

Ukipata mafundi wazuri ukawa mwaminifu ni uwekezaji mzuri

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Je ww binafsi unaujuzi angalau kidogo wakushona kwakutumia cherehani?
 
Nunua vyerehani vya kisasa vyenye uwezo wa kufanya mambo mengi. Anza kuwaajiri vijana wachache wenye uwezo na ubunifu kisha tafuta eneo zuri na uiweke Ofisi yako katika muonekano mzuri. Shona suti za kiume, suti za kike, uniforms za makazini na mashureni na baadhi ya nguo za mitindo ya kiubunifu. Walenge wateja wa uchumi wa Kati. Buni Logo yako na slogan ya kibiashara kisha jitangaze vizuri mitandaoni.
 
Nunua vyerehani vya kisasa vyenye uwezo wa kufanya mambo mengi. Anza kuwaajiri vijana wachache wenye uwezo na ubunifu kisha tafuta eneo zuri na uiweke Ofisi yako katika muonekano mzuri. Shona suti za kiume, suti za kike, uniforms za makazini na mashureni na baadhi ya nguo za mitindo ya kiubunifu. Walenge wateja wa uchumi wa Kati. Buni Logo yako na slogan ya kibiashara kisha jitangaze vizuri mitandaoni.
Asante Sana [emoji1666]
 
Najua kila siku watu wanakula na kuvaa, ukija kwenye sekta ya Chakula watu wengi wamewekeza huko kuna cafe za kila aina Mjini Canteen za kutosha na kila siku wanapiga hela ata kwa mtaji kidogo wa mama ntilie,

Leo mi nataka nifanye kwa upande wa pili kwa kuwa watu wana kula basi wanavaa pia na ndio maana hauwezi kutana na binadamu anaetembea uchi,

Lengo.
Kufungua kiwanda cha nguo, ninachoitaji ni vitendea kazi vyereani 3 tofauti,mashine ya kuchapa maandishi kwenye t shirt(siyo lazima nianze nayo)

--Kwenye kiwanda changu nitahitaji vijana watatu tu wa ushonaji na hao hao ndio watadili na designing ya mavazi,

--malipo watakuwa wanalipwa kwa mwezi kama wafanyakazi wengine na watakuwa na mikataba ili tubanane vizuri

--Kiwanda changu kitadeal sana na designing ya ushonaji wa nguo za kike na za watoto,kidogo na nguo za vijana wa kiume kwa sababu nafikiri ndio soko lilipo,

--Kiwanda changu kitakuwa cha kisasa nataka nitengeze website Acount mbali mbali kwenye social network eg insta, tweeter N.k zitakazodili na kutangaza bidhaa zinazotoka kiwandani kwangu,

--Nataka kiwe free delivery unaagiza mzigo kutoka kiwandani designing yake unashonewa unapakiwa na kukufikia popote ulipo ndani ya tanzania(siyo leo biashara ikikua kua)


Mtaji nilionao wa kuanzia ni takribani milioni 2 Tsh pesa halali kwa malipo ya kitanzania.

Najua humu kuna Wazoefu naomba mnipe changamoto kama hela niliyonayo inatosha au niongeze ngapi kwa mahitaji ya kiwanda changu.


CC Zero IQ
vp bro ulifungua?
 
gpblaze,

Kazi ya ushonaji inahiji saana mtu kujituma. Unaweza uwe na mtaji mkubwa saana but asipojituma ni buree... Mtaji wa kushona ndio moja ya biashara unaweza anzia hata nyumbani kama huna pesa ya office ingawa office yapendeza zaidi.

Vitu vya msingi vya kuzingatia (upande wa gharama na ufanisi)

Vifaa:-

A]. Cherehani ya kawaida (line or zig zag) na Cherehani ya finishing.
B]. Vifaa vidogo kama pasi, Mkazi, Nyuzi, Sindano, ki-mashine kidogo cha kugundisha vitu kama stones, maua n.k.
C]. Hivo vipengele [A] & ndizo basics za kuwezesha.

Ya Kuzingatia:-



  1. Kwanza mdogo wako hakikisha kuwa kweli anaipenda hiyo kazi na biashara ya kushona. Maana inaweza ukawa umem direct huko kama njia rahisi ya kuhakikisha kuwa ana kipato kumbe yeye hata haipo moyoni, akilini wala malengoni. Kama hataki unamlazimisha... Hata ugharamie vipi hawezi fanikiwa sababu ni kazi inayohitaji mtu kujituma na kuipenda kazi yake.
  2. Shughuli ya ushonaji imekuwa saana hapa karibuni, inapanuka na kukua kiwango cha heshima juu ya hio sector na Biashara za ushonaji. Hivo inatakiwa ajitume saana kufuatilia nini wengine wanafanya. Ufundi nguo ni moja ya eneo ambalo mtu haachi kujifunza. Kila siku ya Mungu kuna kitu kipya.
  3. Inatakiwa awe mbunifu, mjanja, na makini katika kazi yake. Kuna wateja wengine anaweza ona mshono akataka (maybe ni mnene anataka mshono wa mtu mwembamba); ajue namna ya kujua hii nguo huu yamfaa na kumpendeza, huyu hii itakuwa kituko n.k. Hii inaepusha kutupiwa lawama za kutojua kazi yako. Mwisho wa siku nguo isipopendeza itakuwa kama vile sabb haijashonwa vizuri kumbe mshono kituko.
  4. Ajatahidi saana kutokuwa mroho wa pesa, asiwe mvivu, asiwe msumbufu... Hii yooote itamjengea kuwa na nidhamu katika kazi yake. Kuhakiki ngua inakuwa tayari by deadline, kupanga within range anayoweza mudu (labda nguo zote kuchukua wiki mbili iwe tayari imeisha, na the like)

Mtu ukijipanga vema.... Ushonaji unalipa saana na ni mzuri mradi uwe na malengo na focus ya Biashara yenyewe. Ujue nini unataka, soko lako ni akina nani (akina dada/mama tu? Harusi? n.k); na wanawake wanavaa jamani... Ni moja ya biashara ya uhakika ambayo hulali njaa... Kila la kheri kwa mdogo wako.


Pamoja Saana.
Ushauri mzuri sana
 
Back
Top Bottom