Ushauri kuhusu biashara ya ushonaji wa nguo na upatikanaji wa vifaa vyake

Wanazengo, Mimi nilikuwa na shida ya fundi cherehani/ nguo. Wapi naweza kuwapata au Kama mtu anaweza niunganisha na mmoja?
uko mkoa gani mkuu kama hutojali niambie pia unataka kufungua biashara ili nikuunganishe
 
Habari za wakati huu

Wakuu nakuja mbele yenu mnipatie msaada wa mawazo, ninafikiria kufungua duka/frem ya kushona nguo za akina mama na watoto (me na ke). Naamini mavazi ya akina mama na watoto yanavalika sana kwa mfano kipindi cha sikukuu, sherehe n.k

Kifupi nataka kuwa fundi nguo niwe na kiofisi changu nifanye kazi na Mungu akinipa nguvu niajiri watu au hata partneship tufanye kazi.

Tukiachana na ujuzi, sijui ni vitu gani hasa vya msingi kua navyo (mashine zipi), wapi nitavipata na bei zikoje, pia malighafi (vitambaa) nitapata wapi kwa unafuu.

Nishaurini lolote linalohusiana na hii biashara wakuu.

Najua humu kuna wazoefu wa hizo biashara tafadhali nisaidieni niweze kujiajiri.
 
Naomba kujua chuo au mahala pazuri ambapo wanafundisha fani hii ya kushona.Gharama zake zikoje na mafunzo huchukua muda gani?Natanguliza shukrani.
 
Mrejesho tafadhali. Ulifanikiwa? Kama ulifanikiwa, tunaomba utuwekee bei ya hivyo vitu na wapi ulinunulia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naomba mwenye ujuzi wa biashara ya kusona nguo aniambie abc zake maana nataka nichukue frem mahali , kisha nitafute mwanaume na mwanamke wanaojua kushona na kudisigne vizuri tuanze kazi.

Binafsi sijui kushona ila nitakuwa nafanya marketing na kusupervise.

Naombeni msaada tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…