Ushauri kuhusu biashara ya ushonaji wa nguo na upatikanaji wa vifaa vyake

Habari wanabodi, nimepata na kuvutiwa na wazo la kufungua karakana na kufanya biashara ya kutoa huduma za ushonaji wa nguo.

Lakini binafsi sina ufahamu juu ya seti za vyerehani zinazohitajika na aina/chapa inayofaa kibiashara na gharama za hizo cherehani, kikubwa nilichosikia kutoka kwa watunga sera ni kwamba vyerehani vi4 ni kiwanda [emoji23](Nakubaliana nao kwa maana ya skeli ndogo).

Hivyo kutokana na kutojua huko nimeonelea ni vema nikiwashirikisha ili kupata msaada kwa sababu naamini hapa ni nyumbani kwa wabobezi wa masuala mbalimbali na mimi nitaambulia chochote kitu. Natanguliza shukrani na karibuni kwa A,B,C ...!.
 
Tafuta mafundi uwaulize watakupa ukweli cherehani zinahitajika

Ukipata mafundi wazuri ukawa mwaminifu ni uwekezaji mzuri

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Je ww binafsi unaujuzi angalau kidogo wakushona kwakutumia cherehani?
 
Nunua vyerehani vya kisasa vyenye uwezo wa kufanya mambo mengi. Anza kuwaajiri vijana wachache wenye uwezo na ubunifu kisha tafuta eneo zuri na uiweke Ofisi yako katika muonekano mzuri. Shona suti za kiume, suti za kike, uniforms za makazini na mashureni na baadhi ya nguo za mitindo ya kiubunifu. Walenge wateja wa uchumi wa Kati. Buni Logo yako na slogan ya kibiashara kisha jitangaze vizuri mitandaoni.
 
Asante Sana [emoji1666]
 
vp bro ulifungua?
 
Ushauri mzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…