Ushauri kuhusu kituo kizuri cha kujiandaa kurudia mtihani wa Kidato cha Sita

Ushauri kuhusu kituo kizuri cha kujiandaa kurudia mtihani wa Kidato cha Sita

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2019
Posts
495
Reaction score
708
Natumaini kila mmoja wetu hapa yupo na siku nzuri kabisa;

Nimekuja kwenu asubuhi hii ili kuomba ushauri wa mambo ya kielimu; hasa kurudia mtihani wa kidato cha sita. Kitaaluma mimi ni mwalimu wa ngazi ya cheti, pia nilisoma kidato cha sita mwaka 2014 mchepuo wa PCM. Sikufanya vema kipindi hicho kutokana na sababu mbalimbali kwani nilipata alama za DEE katika mchepuo wangu;hiyo D ni kwenye Physics na hizo EE ni kwenye Chemistry na Advanced Mathematics.

Mwaka jana nilijiunga na Diploma ya Ualimu Msingi yaani DPTE pale Open University;lakini baada ya kusoma kwa muda mchache kwa mtaala wao mpya nimeona kozi hii hainipi wigo mpana wa kujiendeleza hapo baadaye kwenye masuala ya mbali na ualimu, mimi napendelea taaluma ya sayansi na kompyuta hasa Uhandisi.

Nilijaribu kuomba kubadilisha kozi ya DPTE ili nisome Foundation Program lakini ikawa ngumu kwani nilishasajiliwa kwenye Diploma. Kuna uzi unaofanana na huu nilishauweka hapa na wadau kadhaa wakanishauri, nashukuru sana kwa ushauri wenu na niliufanyia kazi lakini hili la sasa ni tofauti kidogo, japo linaonekana kufanana na lile! hasa baada ya kusoma kwa muda hiyo Diploma ya Ualimu.

Sasa nimeazimia kwa dhati kabisa kurudia mtihani wa kidato cha sita kwa masomo ya Chemistry na Adv. Mathematics pekee kama Mtahiniwa wa Kujitegemea. Naamini nikipata kituo kizuri cha kusomea wakati wa jioni;hii ikihusisha wawezeshaji yaani walimu wa hayo masomo, mwaka ujao nitafanya mtihani huo panapo majaliwa.

Mimi kwa sasa nipo Dar Es Salaam na ni mtumishi wa umma kwa upande wa elimu msingi.
Tafadhali, kama kuna mtu anajua kituo chenye wafundishaji mahiri kwa masomo hayo mawili na ambacho naweza kusoma nyakati za jioni naomba anifahamishe hasa kwa maeneo ya Temeke au Ilala.

Shukrani sana na samahani kwa uzi mrefu ndugu zangu.
 
Mkuu kwa kuwa sasa hivi una DEE,hapo unapaswaa kusoma somo Moja ambalo ukikazana sana upate walau Kuanzia D kwenda A ili uwe na vingezo vya kudahiliwa chuo kikuu.

Kingine naona kama huna future kwenye carrier yako,yaani una tapa tapa hujui kipi ifanye na kipi unatakiwa kufuata.Mwisho wa siku utasoma unachotaka ila utakosa application yake kwenye maisha yako unless uwe risk taker.


Nikushauri tuzingatie malengo yako katika maisha na ujiuize hiyo kozi unayitaka kusoma itakuweka wapi na kwa Muda Gani,je huu ualimu ulio nao unauweka wapi baada ya kusoma kozi nje na ualimu jambo ambalo linaweza kukurudisha nyuma.


Mwisho hakuna kituo kizuricha kurist ili ufaulu mtihani,kituo kizuri ni kichwa chako ulivyokuandaa kujibu mtihani
 
Shukrani mdau, natamani kufanya kile ambacho napendelea na si kile ambacho nakifanya kwa sababu sina namna.
Mi nina swali.

Ukifanikiwa kufahuru form 6, unaenda chuo si ndio.

Kwanini usitumie matokeo ya form 4 ukaenda Diploma nyingine then ukaenda Chuo.

Au unaona mzunguko mrefu?
 
Mi nina swali.

Ukifanikiwa kufahuru form 6, unaenda chuo si ndio.

Kwanini usitumie matokeo ya form 4 ukaenda Diploma nyingine then ukaenda Chuo.

Au unaona mzunguko mrefu?
Swali nzuri sana. Kuhusu kutumia matokeo ya kidato cha nne si tu mzunguko utakuwa mrefu bali gharama itakuwa kubwa zaidi, na pia nitahitajika kusoma Full time kitu ambacho kitakuwa kigumu kwangu kwa wakati huu. Hii itakuwa tofauti na nikitumia matokeo ya ACSEE.
 
Kemia achana nayo komaa na Adv mathematics ukikaza umefeli sana una C na pepa za siku hzi zimekuwa nyeupe sana.....

ila mkuu form six 2014 muda wote ulikuwa wapi ulishindwa hata kusoma diploma UDOM miaka miwili sahivi ungekuwa mbali sana,..... yahn ukitoboa mwakani ndio uanze chuo .....ukisoma hizo injineering unamaliza 2031 kmmke. Hapo naamin unakuwa unaitafuta 40yrs huko....

Anyway muda bado unao kufukuzia ndoto.
 
Back
Top Bottom