Ushauri: Kuongeza Tax base, Rais na Wabunge walipe Kodi

Sasa hao Si watoto WADOGO kwamba wasamehewe Kodi ilhali mkulima analipishwa Kodi 100% ya mapato yake ilhali mbunge alipe 25% tu ya mapato yake.

Hivyo Kwakuwa hiyo 25% ya mapato Yao yaani 4ml kati ya ml 18 inayokatwa Kodi Kwakuwa ni kinyume na Utaratibu na HAKI, hao hawalipi Kodi.

Twende Kwa Rais, Yeye ndo sent Tano ya Kodi halipi!

Kwann?
 
Kwanza kabisa, umekubali wabunge wanalipia kodi kipato chao kwa angalau 25%, kama kweli wanalipwa marupurupu yanayofanya kipato chao kufikia 18 milioni, na si kweli kwamba hawalipi kodi?
 
I agree with you mkuu.
 
Kwanza kabisa, umekubali wabunge wanalipia kodi kipato chao kwa angalau 25%, kama kweli wanalipwa marupurupu yanayofanya kipato chao kufikia 18 milioni, na si kweli kwamba hawalipi kodi?
Kwa kuwa ,

Kuhamishia kipato kikubwa Cha mapato Yao kifikiacho ml 14 kati ya ml 18 ni Hila Ili kukwepa Kodi,

Wabunge hawalipi Kodi.

Wote wanatakiwa kuhesabiwa sawa mbele ya Sheria.
 
Tuweke mipaka ya wanafunzi wanaosoma shule za binafsi kwa kutoza kodi ya ada kwa kila mwanafunzi kwa % 0.03 ya ada ya mwanafunzi kwa mwaka ili ata mawaziri wakiona ninyingi waboreshe shule za umma
Wazo Zuri.
 
Kwa kuwa ,

Kuhamishia kipato kikubwa Cha mapato Yao kifikiacho ml 14 kati ya ml 18 ni Hila Ili kukwepa Kodi,

Wabunge hawalipi Kodi.

Wote wanatakiwa kuhesabiwa sawa mbele ya Sheria.
Ukisema kuwa wabunge hawalipi kodi na ukisema wabunge hawalipi kodi kwa kiasi kikubwa cha kipato chao, hizo ni statements mbili tofauti.

Hiyo statement ya kwanza inatoa impression kwamba wakilipwa shilingi milioni 18 hawalipi kodi hata shilingi moja, which is not the case.
 

Unashauri nini kifanyike ili mambo yawe tofauti, ukizingatia hali halisi ilivyo?
 
Unashauri nini kifanyike ili mambo yawe tofauti, ukizingatia hali halisi ilivyo?
Watu wengi wana focus kwenye mambo ya juu juu, hawaangalii matatizo ya msingi.

Watu wanapenda sana kulaumu vi9ngozi, bila ya juangakia matatizo ya jamii kiujumla na kukubali kuwa hata hao viongozi wametoka katika janii yetu hii hii na hata matatizo yao kimsingi ni natatizo ya jamii yetu.

Utamaduni wetu kama taifa inabidi ubadilike. Inabidi watu wachukue ownership zaidi kwenye mambo ya kuendesha nchi. Hilo ni jambo la msingi kabisa. Sasa hivi watu wengi wamesha give up hawajaki wala hawafuatilii.

Watu wakichukua ownership katika mambo ya kuendesha nchi, jambo ambalo kwa sasa kuna wengi hawalifuatilii, watagundua kuwa kuna mambo mengi hawayaelewi, wamewaachia viongozi tu, na hapo ndipo viongozi wanapowapiga.

Wakigundua kuwa kuna mambo mengi hawayaelewi, kama wana nia thabiti kuiendeleza nchi yao, watajifunza zaidi na kuungana zaidi kuelewa mambo, ku lobby ili kupata uhuru zaidi na habari zaidi, kuwafanya viongizi wawe wanawajibika zaidi, kufanya mfumo uwe na checks and balances nyingi zaidi.

Eventually utapata maendeleo ya polepole yatakayoleta critical mass ya kuwafanya viongizi wasiwe mabwana wa wananchi, wawe kile kinachoitwa "servant leaders" zaidi.

Ukiangalia hii process, hii ni bottom up approach, wananchi wana ji organize wenyewe kuwawajibisha viongozi na kuleta uwajibikaji.

Tatizo sasa hivi wananchi wengi hawako involved, hawana elimu, hawana taarifa, hawana organization, wamebaki kutegemea viongozi wawahurumie na kuwafanyia kazi yao wananchi, viongozi wawaletee maendeleo.

Viongozi wenyewe wana matatizo kibao, wanapata "development fatigue", wana focus kwenye self preservation yao kisiasa ambayo inaweza hata kupingana na maendeleo.

Essentially viongozi wana uamuzi wa kuwaletea watu maendeleo makubwa ya kiuchumi na kielimu halafu viongozi watolewe madarakani kwa kuwa watu watakuwa wameamka sana, au viongozi kuwapa watu maendeleo kiduchu ya kupigia kampeni za kisiasa tu, halafu viongozi wabakie madarakani.

They choose the latter.
 
Ubunge ni kazi ya kuajiriwa ktk mhimili mmojawapo. Anapoomba anapata stahili zote ikiwa ni pamoja na za kstaafu- ambazo wanajipangia wenyewe na ambazo ni siri!! Za wengine znatngzwa unapoomba na kla mtu anajua mshahara unaangukia kifungu gani. Wao wana stahiki mblmbl na ni za tofauti kw xana. Na wanaziongeza watakavo! Halafu kaz kupigapiga meza na kuitikia NDIOOO! Wanakula "tulichopanda"
 
Haki inaenda na wajibu, kila mwananchi walipe kodi lkn serikali ifanye wajibu wa matumizi sahihi ya kodi. 1. Kununua magari ya bei ya kawaida km hardtop na hilux kwa wakuu wa mikoa na wakurugenzi mpaka mawaziri. Mashangingi iwe kwa Rais, makamu wa Rais, na waziri mkuu. 2. Report ya CAG ifanyiwe kazi, ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua wezi wa kodi zetu.
 
Sasa wewe unaona ni Haki wakwepa Kodi na wezi wa Kodi kuchukuliwa hatua ilhali Rais na Wabunge hawalipi na wanakwepa Kodi?
 
Ina maana hawalipi hata witholding tax?

Kama hawalipi hiyo Kodi siyo sawa kabisa
 
Sasa wewe unaona ni Haki wakwepa Kodi na wezi wa Kodi kuchukuliwa hatua ilhali Rais na Wabunge hawalipi na wanakwepa Kodi?
Siyo sahihi kabisa, posho na mshahara wa wabunge est 12m per month x no of MB x 12months = lost tax income. 2. Siyo tax exempted hata sheria ya mafao ni double standard. Wabunge hawasubiri miaka ya ku retire kupata mafao yao.
 
Hili la wabunge walipe kodi nasema hapana, hawa wanazo familia mbili mbili za kutunza, yaani Dodoma na jimboni kwake na mwisho hawatakiwa kuwa na mawazo ya siku ya mshahara ili waweze kututumikia vizuri.
Kwani wanaajiriwa ili wapate pesa za kutunza familia zao?
 
Kuna clip moja nilimsikia muhubiri mmoja wa Kikristo akisema maneno ya busara sana; halikua jambo la kidini. Mambo ya kawaida kabisa katika jamii; kwamba mzalendo namba 1 katika nchi nyingi sio rais wa nchi, wala hayupo kabisa katika list ya wazalendo katika nchi zao, wana siasa wote hasa wa nchi za Kiafrica sio wazalendo kwa nchi zao, mzalendo namba 1 ni Wanajeshi na mzalendo No 2 ni walipa kodi. Hao wengine hawana udhu wa kuuzungumza uzalendo, hawana kitu cha namna hiyo. Nakubaliana na mleta hoja, wana siasa hasa wa Chama tawala, WALIPE kodi ili na wao waone uchungu wa matumizi ya pesa zetu. Tuchange sisi halafu Mwijaku aje amsifie mtu mwingine eti kaleta pesa, sio sahihi
 
Bodaboda na winga walipe kodi
Boda na guta na Bajaj za abiria nowadays wanalipa Kodi ya mapato, 150,000 Kwa mwaka kama sikosei.

Kuhusu winga, msisitizo uongezwe, wasajili ofisi walipe Kodi, wabadilishiwe Jina Toka kuitwa winga Hadi "Commission Agents".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ