ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 3,586
- 3,857
Diaspora wa kitanzania aliopo Nje kama ana nia kweli ya kuwekeza hapa Tanzania sidhani swala la uraia pacha ni kikwazo.
Yeah, mkuu swala hii inabidi lifanyiwe kazi kwa haraka sanaBalozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.
Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?
Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?
Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.
Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?
Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi nane Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu.
Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha! Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!
Kwa hiyo Balazo Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana.
View attachment 1808843
Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:
Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!
Wakati Tanzania imezama katika mawazo mgando ya mwaka 47 kuwakatalia raia zake uraia pacha, nchi nyingine sasa zinatoa uraia kukaribisha wawekezaji!
Wengi wanaopinga uraia pacha, wanajua hawana nafasi ya kuja kuwa raia pacha
Na wengine:
Hutaki wewe Mkuu, na nahisi sababu zako zitakuwa hazina mshikoMambo ya Uraia pacha hatutaki...
Mie nilishawagundua siku nyingi Mkuu. Siku moja tulikuwa sehemu sehemu jamaa walikuwa wanabisha eti sie tumesota hapa wao wakakimbia nchi halafu wanataka warudi kututambia! Ndipo nilijua kumbe watu ni chuki na wivu tu vinawasumbua!Kumbe ni kweli hamuna hoja zaidi ya vihoja na chuki tu.
South Afrika ina uchumi mzuri kuliko Tanzania, lakini bado ikaona umuhimu wa uraia pacha. Tanzania masikini wao ndio wanajifanya ooh uzalendo, ulalama wa nchi. Point off kabisa.Marekani ni tajiri na inadumu na hali nzuri kwa sababu ya mchanganyiko wa watu, kuna wahindi, wachina, waarabu mpaka wamasai wapo kule.
South Africa ni nchi yenye uchumi mkubwa kwa sababu ya mchanganyiko mkubwa wa watu wa rangi mbalimbali wanaoishi pamoja.
Watanzania wenzetu ambao wapo nje wanao mchango mkubwa sana wa kuipeleka Tanzania mbali kiuchumi, wanao uzoefu (exposure) wa hali ya juu kwenye masuala mengi. Sisi wenyewe kwa kubagua wenzetu hatuwezi kufika mbali.
Unaona basi usivyo na point? Aina ile ile ya wabishiwa wivu na chuki tu.Kwani shida ni ya nani? Ni watanzania kutaka uraia wa nchi zingine au wa nchi zingine kutaka uraia wa TZ? Shida ni kwamba kuna wa-TZ walioamua kuukana uraia wao na kuchota uraia wa nchi zingine wakiamini wameukata. Sasa kihoro kinawasumbua wanataka waruhusiwe kuwa tena wa TZ.
Ndo maana unasikia maneno kama kuonea wivu. Ni kwa kuamini kwamba walipopata uraia wa nje waliukata: BAlozi Mula mula huyo muonee huruma tu! NI bahati mbaya leo hii ni waziri labda naye anataka uraia wa Rwanda.
Kuna jamaa yangu alikua akifanya usajili wa vitambulisho kule maeneo ya oysterbay ambapo wengi wao ni watoto was vigogo na vigogo wenyewe.Point nzuri, ila watoto wao hawana uraia pacha Mkuu, labda kwa siri. Maana Tanzania bado hairuhusu.
Ningewashauri wale wote wanaoona faida za Tanzania kuwa na uraia pacha watoe msisitizo wao kwenye hii thread
Ni mhindi gani wa kuhangaika na ajira za kulipwa milioni kwa mwezi? Labda mhindi koko
Kumbe ni kweli hamuna hoja zaidi ya vihoja na chuki tu.
Hoja yako kuhusu Wahindi inaonekana msingi wake ni Uhamiaji hawako makini, wanachukua rushwa kutoa vibali.
Hapo ni kuimarisha hii idara iwe na watu makini. Diaspora wengi ni watu weusi kama wewe. Wahindi wanaweza kuwa less than 5%.
Kwanini isiwe kikwazo na wakati anachukuliwa kama raia wa kigeni?Diaspora wa kitanzania aliopo Nje kama ana nia kweli ya kuwekeza hapa Tanzania sidhani swala la uraia pacha ni kikwazo.
Duh! Wacha ni reserve comments zangu tusije kukwazana. Kumbe na wewe ni wale wale tu, Sema una kauli za kinafiki...anaweza kuwekeza kwa kuwatumia wazazi au ndugu zake.
..sokomoko linakuja kukitokea bahati mbaya kuwa aliyeandikishwa mali amefariki.
..au aliyeandikishwa mali amekosa uaminifu huyu diaspora anakuwa hana namna ya kupata haki yake.
Duh! Wacha ni reserve comments zangu tusije kukwazana. Kumbe na wewe ni wale wale tu, Sema una kauli za kinafiki.
Mkuu Wahindi ndio waneshikila Uchumi wetu Mkuu!
Pia Ni ngumu...Nasema ngumu kwa hiyo Taasisi kudhibiti Vibali vya Kazi!
Kwani Hawapendi Hela?
Angalia Work Permit tuu za Makampuni Kama ya cement,Migodini,Simu,nk!
Halafu uwaulize ni Mara ngapi wanatembelea Site au Wameonana na Vyama vya wafanyakazi angaalu kuwahoji?
Balozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.