Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

..labda hawa ndugu zetu waliozaliwa Tz na kuchukua uraia wa nje watengenezewe UTARATIBU MAALUM utakao rahisisha mambo yafuatayo.

1. Mirathi.

2. Uwekezaji.

3. Ukaazi.

4. Ajira.

..Mengine mnaweza kuongezea. Na utaratibu huo sio lazima uwe ktk daraja sawa na sisi tunaoendelea kuulinda na kuuhifadhi Uraia wetu wa Tanzania.
 
Balozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.

Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?

Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?

Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.

Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?

Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi nane Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu.

Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha! Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!

Kwa hiyo Balazo Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana.

View attachment 1808843

Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:

Na wengine:​

Yeah, mkuu swala hii inabidi lifanyiwe kazi kwa haraka sana
Dunia saivi imebadlika ni vema tukawa na utaratbu wa Urai pacha
 
Kumbe ni kweli hamuna hoja zaidi ya vihoja na chuki tu.
Mie nilishawagundua siku nyingi Mkuu. Siku moja tulikuwa sehemu sehemu jamaa walikuwa wanabisha eti sie tumesota hapa wao wakakimbia nchi halafu wanataka warudi kututambia! Ndipo nilijua kumbe watu ni chuki na wivu tu vinawasumbua!
 
Marekani ni tajiri na inadumu na hali nzuri kwa sababu ya mchanganyiko wa watu, kuna wahindi, wachina, waarabu mpaka wamasai wapo kule.

South Africa ni nchi yenye uchumi mkubwa kwa sababu ya mchanganyiko mkubwa wa watu wa rangi mbalimbali wanaoishi pamoja.

Watanzania wenzetu ambao wapo nje wanao mchango mkubwa sana wa kuipeleka Tanzania mbali kiuchumi, wanao uzoefu (exposure) wa hali ya juu kwenye masuala mengi. Sisi wenyewe kwa kubagua wenzetu hatuwezi kufika mbali.
South Afrika ina uchumi mzuri kuliko Tanzania, lakini bado ikaona umuhimu wa uraia pacha. Tanzania masikini wao ndio wanajifanya ooh uzalendo, ulalama wa nchi. Point off kabisa.
 
Kwani shida ni ya nani? Ni watanzania kutaka uraia wa nchi zingine au wa nchi zingine kutaka uraia wa TZ? Shida ni kwamba kuna wa-TZ walioamua kuukana uraia wao na kuchota uraia wa nchi zingine wakiamini wameukata. Sasa kihoro kinawasumbua wanataka waruhusiwe kuwa tena wa TZ.

Ndo maana unasikia maneno kama kuonea wivu. Ni kwa kuamini kwamba walipopata uraia wa nje waliukata: BAlozi Mula mula huyo muonee huruma tu! NI bahati mbaya leo hii ni waziri labda naye anataka uraia wa Rwanda.
Unaona basi usivyo na point? Aina ile ile ya wabishiwa wivu na chuki tu.

Kwanza hao walioukana uraia, wakipewa tena uraia wa Tanzania wewe unaathirikaje, na hasa ukizingatia itawawezesha kuhamisha mitaji kuja Tanzania kirahisi?

Pili, kama hao walioukana uraia wanatamani tena kuwa Watanzania, sio lazima wawe raia pacha. Bado wanaweza kuwa raia wa Tanzania tena, kwa hiyo issue sio hiyo. Uko off kabisa.

Uraia pacha unaingia pale ambapo inakuwa rahisi kwa mtu kuhamisha capital kati ya nchi mbili (repatriation of earnings, profits or capital). Ukitaka kuona ni jinsi gani, hebu nenda Bank waambie ninataka kutuka Dola Elfu mbili kwa rafuiki yangu pale Kenya uone utakavyotolewa nje. Lakini sasa, ukiwa na uraia pacha wa Tanzania na Kenya, utaruhusiwa kirahisi kwa kuwa wewe ni raia wa Kenya pia, kwa hiyo inakubalika kwamba unafanya repatriation of profits. Ndio maana hata makampuni ya kigeni yanaruhusiwa kutoa fedha walizochuma hapa nchini kwenda nje. Ni kwa msingi huo mie nikiwa Kenya na nina uraia pacha na Tanzania, inakuwa rahisi kutuima fedha toka Kenya kuja Tanzania.

Yaani watu mnabisha wakati hivi vitu hamvielewi. Eti uzalendo, usalama, wivu tu na chuki vimewazidi. Uzalendo wako unaisaidia nini Tanzania kama hujawahi kuiingizia nchi hata dola moja toka uzaliwe?
 
Point nzuri, ila watoto wao hawana uraia pacha Mkuu, labda kwa siri. Maana Tanzania bado hairuhusu.
Kuna jamaa yangu alikua akifanya usajili wa vitambulisho kule maeneo ya oysterbay ambapo wengi wao ni watoto was vigogo na vigogo wenyewe.

Sasa wale jamaa wanakuja na passport mbili ya Tanzania na ughaibuni na zote zinataarifa zao sasa hio sio uraia pacha kweli?
 
Mkuu Membe alifanya kazi nzuri sana alipokuwa Foreign Affairs kwenda katika nchi mbali mbali za Africa na Caribbean kukusanya important info ya advantages na disadvantages za uraia pacha katika nchi ambazo zinaruhusu hilo. Nchi zote alizotembelea maoni ya Marais na pia Wizara zao za nje zilifagilia sana uraia pacha na hawakusagia chochote lakini UNAFIKI wa Kikwete baada ya kuona ndani ya ccm linapingwa sana bila ya kuwepo hoja ya msingi ukakwamisha hili kufanikishwa. Nadhani Tanzania katika Africa inaweza kabisa kuwa nchi ya mwisho kuruhusu uraia pacha.
Nasikia leo saa 12 jioni EAT kulikuwa na kikao cha Diaspora na balozi zetu mbali mbali za nchi za nje ambacho Mwenyekiti wa kikao alikuwa Asha Migiro.
Ningewashauri wale wote wanaoona faida za Tanzania kuwa na uraia pacha watoe msisitizo wao kwenye hii thread
 
Hata swala la passport wangepunguza vikwazo na mlolongo, ili vijana wakajimwage mambele ili kujiokotea chochote na kuleta nyumbani
 
Ni mhindi gani wa kuhangaika na ajira za kulipwa milioni kwa mwezi? Labda mhindi koko

Ah aha kumbe wewe hujui...
Nenda vuwanda vya Cement utajua wahindi ni Kina Nani na wanapokea Tsh ngapi?
Unaweza Kupata Ugonjwa wa Moyo ukianbiwa Mshahara wao,
Hata Mimi nilidhani Tsh 5,6M tuuu..
Kumbe duuu...
Nikasema Ahsanteeee Piga Mara 5,6 ya Hizooo
 
Mkuu kuna baadhi ya Watanzania wana chuki za kutisha. Akiona kitu yeye hawezi kukipata basi anaweza kufanya juu chini hata kusema uongo ili mwenzake pia asikipate. NTIMA NYONGO!!!
Kumbe ni kweli hamuna hoja zaidi ya vihoja na chuki tu.
 
Hoja yako kuhusu Wahindi inaonekana msingi wake ni Uhamiaji hawako makini, wanachukua rushwa kutoa vibali.

Hapo ni kuimarisha hii idara iwe na watu makini. Diaspora wengi ni watu weusi kama wewe. Wahindi wanaweza kuwa less than 5%.

Mkuu Wahindi ndio waneshikila Uchumi wetu Mkuu!
Pia Ni ngumu...Nasema ngumu kwa hiyo Taasisi kudhibiti Vibali vya Kazi!
Kwani Hawapendi Hela?
Angalia Work Permit tuu za Makampuni Kama ya cement,Migodini,Simu,nk!
Halafu uwaulize ni Mara ngapi wanatembelea Site au Wameonana na Vyama vya wafanyakazi angaalu kuwahoji?
 
Niambie faida na hasara za uraia pacha. Tuanzie hapa kwanza na asiniambie Hakuna hasara maana Hakuna jambo lolote lisilokuwa na hasara
 
..anaweza kuwekeza kwa kuwatumia wazazi au ndugu zake.

..sokomoko linakuja kukitokea bahati mbaya kuwa aliyeandikishwa mali amefariki.

..au aliyeandikishwa mali amekosa uaminifu huyu diaspora anakuwa hana namna ya kupata haki yake.
Duh! Wacha ni reserve comments zangu tusije kukwazana. Kumbe na wewe ni wale wale tu, Sema una kauli za kinafiki.
 
Duh! Wacha ni reserve comments zangu tusije kukwazana. Kumbe na wewe ni wale wale tu, Sema una kauli za kinafiki.

..Umenielewa vibaya. Mimi nilikuwa namjibu Econometrician.

..Umefanya vizuri ku-reserve comments zako.

..Ungeweza kupata DHAMBI za bure kwa kunituhumu kitu ambacho sicho.

..I am just being realistic here.

..Kama itakupendeza tafuta mrejesho aliofanya muwakilishi wa diaspora ktk bunge maalum la katiba.

..baada ya kumsikiliza nime-conclude kwamba ni afadhali mpiganie kuwa na ukaazi wa kudumu kuliko kuwa na uraia pacha.
 
Mkuu Wahindi ndio waneshikila Uchumi wetu Mkuu!
Pia Ni ngumu...Nasema ngumu kwa hiyo Taasisi kudhibiti Vibali vya Kazi!
Kwani Hawapendi Hela?
Angalia Work Permit tuu za Makampuni Kama ya cement,Migodini,Simu,nk!
Halafu uwaulize ni Mara ngapi wanatembelea Site au Wameonana na Vyama vya wafanyakazi angaalu kuwahoji?

Lakini hii ni separate issue. Wengi ya hao Wahindi wanaokuja na kuomba vibali wanatoka India. Hapa tunazungumzia Watanzania (wenye asili ya TZ) walioko Ulaya, US na nchi nyingine.
 
Kubwa ni ushamba na ulimbuken wa baadhi ya wenye mamlaka

Back
Top Bottom