Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
- #81
Unaona basi, na wewe huelewi kabisa maana ya uraia pacha na hujui sifa za mtu kupewa uraia pacha.sisi wanyonge hatutaki uraia pacha, tutakuwa watumw kwenye nchi yetu.
Huko marekani Jaji kama mimi analipwa Mshahara milioni 45 kwa mwezi wakati hapa tunalipwa milioni 9 tu kwa mwezi.
Sasa jaji wa Marekani si atakuja kununua mashamba yote huku, hapana hatutaki.
Hebu niambie, huyo jaji wa USA anaelipwa milioni 45 kwa mwezi, atapewa uraia pacha waTanzania kwa vigezo gani?
Nahata kama ana vigezo (nakuaminisha hana), katika ncho zote zilizo na uraia pacha duniani, anasubiri tu Tanzania itakaporuhusu uraia pacha ndio aje anunue mashamba ya babu zako? Kwa lipi hasa tulilonalo ambalo nchi nyingine zote duniani ambazo zinaruhusu uraia pacha zmekosa?
Ndio maana nikasema wazi, mnaobisha juu ya uraia pacha wala hamuelewi maaana ya uraia pacha na hamjui vigezo vya mtu kupewa uraia pacha. Mnabisha tu kwa chuki na wivu, sio hoja za maana