Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Hili jambo liko wazi kua uraia pacha una faida nyingi kuliko hasara.yaliyobaki ni ujinga wetu tu.Tuna tatizo kubwa sana lakucomplicate mambo badala ya kuyarahisisha.Wakati wenzetu wanatumia hiyo fursa ya kwenda kuchuma uko ugenini na kuleta kwao sisi bado tunawaza kuishi kwakujifungia wakati hatuna manufaa yoyote kwa nchi.Tukifunze kua opportunistic.
 
Kuwekeza nchi flani sio mpaka uwe na uraia wa nchi hiyo,wanaosema eti wao wanamitaji ya kuwekeza lakini wanakwamishwa na Tanzania kukataa uraia pacha ni waongo na wazandiki mbona dangote kawekeza tanzania kwani anauraia wa Tanzania?
 
Kwa mtu aliyezaliwa Tanzania , ukaazi wa kudumu siyo sahihi. Napendekeza uraia pacha...Labda huyo muwakilishinwa Diaspora, alipendekeza kwa wakati ule ambapo wengi walipinga tofauti na sasa. Ukaazi wa kudumu iwe kwa ambao hawajazaliwa Tanzania na wanataka kupata uraia nk.
 
Kuwekeza nchi flani sio mpaka uwe na uraia wa nchi hiyo,wanaosema eti wao wanamitaji ya kuwekeza lakini wanakwamishwa na Tanzania kukataa uraia pacha ni waongo na wazandiki mbona dangote kawekeza tanzania kwani anauraia wa Tanzania?
Mfano wako wa Dangote, ni irrelevant.

Tunazungimzia watanzania wazawa ambao wanataka kurudi na wasiwekewe masharti kama ya wawekezaji wageni pale wanapotaka kurudi na kuwekeza nyumbani.
 
Mfano wako wa Dangote, ni irrelevant.

Tunazungimzia watanzania wazawa ambao wanataka kurudi na wasiwekewe masharti kama ya wawekezaji wageni.
Shida ni kwamba kwa Sera zetu za kodi na sheria zinavyobadilika badilika MTU akishakua na uraia pacha in simple kuhamisha biashara zake pindi pale kunapotokea sintofahamu na serikali na kukimbilia nchi yenye unafuu ambayo kidogo imeendelea.

Pia katika maswala ya usalama ni rahisi kutumiwa na watu flani flani ambao hawalitakii mema taifa
 
Tunazungukwa na nchi zenye matatizo lukuki hapa ukanda wa maziwa makuu

Ndoto zao Ni Tz kuwa na uraia pacha ili wayakimbie matatizo Yao huko kwao

Wengine nchi zao hakuna ardhi ya kutosha .

Watakuja wakwapue ardhi yetu hapa wafanye Yao

Labda huu uraia pacha utuhusu sisi tuliozaliwa TZ sio wa kutoka nje
 
Kuwekeza nchi flani sio mpaka uwe na uraia wa nchi hiyo,wanaosema eti wao wanamitaji ya kuwekeza lakini wanakwamishwa na Tanzania kukataa uraia pacha ni waongo na wazandiki mbona dangote kawekeza tanzania kwani anauraia wa Tanzania?


Kwahiyo unaona ni sawa wewe ungeenda kutafuta maisha au kusoma baada ya kusoma ukapata kazi, halafu Uraia ( kwa maslahi matibabu bure kwako na watoto wako, elimu bure, unasafiri nchi nyingi bila visa, bughudha etc.)

Ukitaka kurudi nyumbani uombe visa? Kuwekeza uwe treated kama mgeni sehemu uliyokulia Baba,Mama, Babu Bibi, Mjomba Shangazi wote wako hapo.

Dangote ni Mnigeria.
 
Siyo kweli. Kuhamisha biashara siyo lazima uwe na uraia pacha. Wawekezaji wakubwa kutoka nje mfano tu Dangote, nani angeweza kumzuia kuhamisha biashara kama alivyokuwa akitaka kufanya?

Kutumiwa kivipi katika masuala ya kiusalama na hao unaosema “watu flani flani” wasiolitakia mema Taifa? Ebu toa mfano mmoja kwa Taifa lenye kukubali uraia pacha na usalama wao ukaharibika kwasababu hiyo. Weka mfano wa Taifa moja tu.
 
Somalia
 
sisi wanyonge hatutaki uraia pacha, tutakuwa watumw kwenye nchi yetu.
Huko marekani Jaji[Watanzania wanao shika nyadhifa za Uwakili na attorneys] kama mimi analipwa Mshahara milioni 45 kwa mwezi wakati hapa tunalipwa milioni 9 tu kwa mwezi.
Sasa jaji wa Marekani si atakuja kununua mashamba yote huku, hapana hatutaki.
 
Sasa kama waliweza kuukana uraia wa Taifa lao ati kwa kigezo cha kupata maslahi walyo yapata huko ugenini wana uzalendo gani tena kwa taifa na kuna haja gani ya kurudi kama RAIA wa Tanzania?wao waje tu kama wawekezaji wengine milango iko wazi,watashindwa kuuza nchi kwa masilahi mazuri watakayopewa na mabeberu kama tu uraia waliukana
 
Haahaaahaa!! Eti kuna Wa Tanzania Mamilioni wanaishi nje. Haaahaaaahaaahaaaaa
 
Wewe hangaika na maisha yako. Kama uliamini ukiwa m-Nigeria ni sifa, usitusumbue kurudi nyumbani. Au unaamini tulioko TZ hatujawahi ishi nje ya nchi? Ulaya, Asia, na Amerika tunapajua boss. Kuleni kibano cha maisha, mukija likizo tambeni na waya masikioni, lakini wajuvi wa mambo tunajua hali ngumu inavyowasumbua.

Mtu anajidai eti watachangia maendeleo, wakati wanashindwa hata kuwasaidia wadogo zao wanaosota nchini. Kuna mijitu imesomba hata wadogo zao na kuwafanya vibarua nchi za watu wakiamini itawatoa, waaapi!
 


Sasa hapo sio ndio tunatengeneza ajira zenyewe, exports mazao yatauzwa ndani na nje, kodi zitalipwa kwa wingi( barabara, madawa, elimu, miundombinu), kupunguza bei na uhaba wa chakula, labda kusaidia matunda yasiozee shambani (more 50% Tanga matunda yanaoza shambani). Huu ndio ufanisi wenyewe,( increase in productivity)

Kuna Watanzania wana ekari hadi elfu kumi lakini hawaziendelezi. Sana sana wanaombea mkopo.

Nimeona Njombe Kuna Wazungu kutoka South Africa wamelima Ekari 10, 000 za Maparachichi wameajiri Watanzania kibao. Kwa hiyo bora uwape wazungu uwanyime ndugu zako.

Shamba usipoliendeleza kwa miaka miwili linachukuliwa. Ardhi ya TZ ni mkopo haiuzwi, kwa hiyo haiwezi kupotea.

Pia unaweza kuweka mikataba sheria flani kuwapa kipaumbele wazawa (ndivyo ilivyo sasa).

Watasaidia pia kwenye nyanja na secka zingine. Masoko, technology, innovation etc.
 
Wewe ni mmoja wapo unabisha uraia pacha juu ya kuelewa mtu anapataje uraia pacha. Hao watu unaowasema watapata uraia pacha wa Tanzania kwa vigezo gani? Wewe unafikiri uraia pacha ni kama kuomba visa?
 
Lazima kutakuwa na ndugu yako nje amekataa kukutumia hata dola moja kukusaidia, na sasa una hasira na uraia pacha ili umkomoe!
 
In short issue hii inacheleweshwa na baathi ya watu wachache ndani ya chama na serikali kwa sababu zao binafsi, lakini naamini Raisi SSH anauwezo wa kupindua meza iwapo itaridhira na nina imani mama ana vision kubwa hata waangusha Watanzania wenzentu kwa hofu za kutengeneza.
 
Lazima kutakuwa na ndugu yako nje amekataa kukutumia hata dola moja kukusaidia, na sasa una hasira na uraia pacha ili umkomoe!
Aliyefanikiwa nje asingeweza kuhangaikia uraia pacha. waliokwama ndo tatizo. wanaasumbuliwa na kihoro. Utaweza kubeba maboksi hadi uzeeni?

Dunia naijua boss! Niko Bongo mchana huu najiandaa jioni niingie mitaani kucheka na majirani na wine yangu. wewe endelea kudumaa akiamini mitaji iko nje na eti tunakuhitaji sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…