Ushauri Kwa BAVICHA na CHADEMA; Someni Historia ya Nchi hii, mnajidhalilisha kwa wenye akili

Stori haijakamilika- Shingo upande Mwalimu aliomba msaada kwa Malkia Elizabeti kuzima ausi.Bila hiyana malkia alingiza timu ya who dare win, ikafyeka waasi. CCm lazima muheshimu "mabeberu" bila msaada wa malkia sidhani ccm ingezaliwa 77.
Mkuu kambona alishiriki kwenye nini kuwatuliza waasi,maana hakua kwenye chombo chochote cha usalama
 
Hao watu kama waliteswa kweli basi ni 2020, na hiyo kesi ilifunguliwa hiyo 2020!! Huyo Mama kawatesa vipi wakati hiyo kesi ni mojawapo ya majanga aliyoachiwa na mtangulizi wake?
Kwanini ulete suala la mama kuupiga mwingi kwenye muktadha huu?! Wewe ndo unamuingiza Mazaa, huku!
 
Endelea kuamini hizo chai za warumi, walizitunga ili wakutawale vizuri jinga wewe....Uliletewa hizo dini na wakoloni ili wakutawale, na wewe umezipokea kama zuzu flani, hata kuhoji unashindwa..
Kwenye uchawi na ushirikina unakoamini Wewe, huwa unahoji?
 
Ndugu,
Yaonyesha kuwa VI THREAD hivyo vinakukera sana. Onyesha ukubwa kwa kuvumilia.
Hata hivyo kwa tuliyojaliwa kuwepo kipindi hicho, kuna mambo ya msingi yanayoonekana PEUPE kabisa.
-Busara za viongozi wa wakati huo zilitawala. Rais Nyerere na hata IGP (nadhani Mahundi) walikuwa kimya kabisa kuhusiana na kesi hiyo.
-Tofauti na mwenendo wa kesi hii iliyopo, ni kuwa mashitaka ya akina Tamimu yalionekana wazi kuwa hayakuwa ya kubumba.
-Vyombo vya habari (Radio TZ na magazeti; Uhuru, Ngurumo, Mfanyakazi na Daily News) viliripoti waziwazi kabisa kila hatua bila vikwazo.
 
Nyie acheni uzwazwa, kesi gani ambayo washitakiwa hawateswi? Kama kutesa ni warrant ya kufuta kesi, basi wote walioshitakiwa waachiwe huru.
 
Lakini waliteswa
 
Mtoa mada Kama ulikuwepo wakati wa hiyo kesi ya uhaini au umesimuliwa uwe mkweli basi. Kuna tofauti kubwa ya kesi hiyo na hii. Kwa taarifa yako hakukuwa na torture unayoisema wakati huo ndio maana hata hao watuhumiwa wengine, wameandika mpaka vitabu mfano Luteni Eugene Maganga hakuna sehemu anayosema aliwekwa kama mshkaki.

Kapteni Zakaria Hans Pope wewe mwenyewe umeona mpaka anakufa ni bilionea. Na hiyo kesi kwa tuliokuwepo hiyo kesi iliendeshwa kwa uwazi mkubwa mno tena kwa kuripotiwa na vyombo vya habari vya umma. Siyo sahihi kulinganisha kesi hiyo na kesi ya Mbowe. Hii ipi kuiaibisha nchi tu hakuna kingine. Hao unaowasema kina Mwamunyange walikuja mahakamani kupambana na Wakili Murtaza Larka.
 

..naona kama umekuwa na haraka kidogo kuleta habari hii.

..sio kweli kwamba washtakiwa wote ktk kesi ya uhaini ya mwaka 1984 walipatikana na hatia.

..wako baadhi ya watuhumiwa ambao waliachiwa huru.

..pia suala la TORTURE halikuwa prominent na wazi kama ilivyo ktk kesi hii.

..vilevile upande wa serikali ulikuwa na mashahidi wengi, tena baadhi wakiwa ni askari active na senior officers ndani ya JWTZ.

..kesi hii inaelekea kuwa ya Polisi peke yao, na so far ushahidi unaonekana ni mwembamba, na mashahidi ni wachache.

..lingine ni kwamba wakati ule Polisi walikuwa wanafuata taratibu na walikuwa wawazi kuhusu watuhumiwa. Kwa mfano, haikuchukua muda mrefu toka watuhumiwa kukamatwa mpaka kufikishwa mahakamani.

..Serikali iliwaalika shirika la kutetea haki za binadamu AMNEST INTERNATIONAL kuja kuhakiki kwamba watuhumiwa wa uhaini wa mwaka 1984 walikuwa ktk mikono salama.

..Sina uhakika kama kamanda Sirro yuko tayari kualika mashirika ya kimataifa kuhakiki kwamba mahabusu wetu hawateswi na kutendewa kinyume na taratibu.

..kwenye kesi hii kuna walakini kwamba " ring leader " Mbowe aliachwa mtaani kwa muda mrefu bila ya kukamatwa.

..Hivi kweli unaweza kuwa na kesi ya ugaidi halafu mpanga ugaidi akaachwa mtaani akiendelea na maisha?

..Watuhumiwa watatu walishafikishwa mahakamani huku " ring leader " na sponsor wa tuhuma zao akiwa mtaani, akitoka na kurudi nchini.

..Kigugumizi cha kumkamata " ring leader " wa huu ugaidi kinaleta mashaka kuhusu uzito wa hizo tuhuma. Nikukumbushe kwamba wale watuhumiwa wa 1983 walikamatwa haraka sana bila kigugumizi hiki tulichokishuhudia safari hii. Na " ring leader " alikuwa ni raia Thomas Lugangira " uncle tom. "

..Lingine ambalo hukulieleza ni jitihada za watuhumiwa wa mwaka 1983 kukwepa mkono wa dola. Wako watuhumiwa ambao walitoroka gerezani na kukimbilia Kenya.

..Sasa mwaka huu tunaambiwa " ring leader " alikwenda zake Dubai, Kenya, na Ulaya, halafu akarudi Tanzania. Yaani hakuwa na harakati zozote zile za kutoroka wakati vijana wake wamekamatwa.

..Lugangira bosi wa watuhumiwa wa mwaka 1984 alipopata nafasi ya kuchomoka alitorokea Nairobi na kutokomea Uingereza ili kukwepa mkono wa dola hapa Tanzania.

..Tofauti nyingine inahusu utoaji wa taarifa kuhusu mwenendo wa kesi. Mwaka 1984 magazeti yote yalikuwa yanatoa taarifa za kesi ya uhaini kwa uhuru na uwazi. Nazungumzia magazeti ya chama na serikali kwa wakati huo.

..Kipindi hiki sioni jitihada za vyombo rasmi vya habari kueleza kinachojiri mahakamani. Hali hiyo inatoa nafasi kwa watu wasio na utaalamu kuripoti kuhusu kesi ambayo naaamini wananchi wanapaswa kupewa taarifa sahihi.

..La mwisho, ni kuhusu timu za mawakili walioshiriki ktk kesi ya uhaini ya mwaka 1984.

..Upande wa utetezi ulikuwa na mawakili mahiri na machachari kwelikweli. Hapa nawazungumzia watu mawakili kama Murtaza Lakha, Tarimo, Mucadam, na wengine.

..Upande wa mashtaka uliongozwa na William Sekule, akisaidiwa na kina Kulwa Massaba, Johnson Mwanyika, na wengine. William Sekule alifanya kazi kubwa sana ktk closing arguments.

..Kesi ilisikilizwa na Jaji Kiongozi Nassoro Mnzavas.
 
Nani kakwambia suala la Torture halikuwa component ya wazi kwenye kesi hii?

Kina Kapteni Maganga na Kadego walilalamika sana kuteswa!

Hadi Maganga kwenye simulizi yake juu ya hii kesi kwenye Gazeti la RAI alielezea kuteswa na Mkuu wa Usalama Jeshini Luteni Kanali Mwamunyange!
 
Kwani Mashahidi kwenye kesi ya Mbowe wameisha?

Nani kakwambia Serikali ( Jamhuri) wamefunga ushahidi wa kesi ya msingi?
 

..sikusoma likiripotiwa kama wakati huu.
 

..kama unathibitisha kwamba watuhumiwa wa 1983 waliteswa, inabidi uthibitishe kwamba sheria za Tz zinaruhusu ushahidi uliopatikana kwa kumtesa shahidi.
 
..kama unathibitisha kwamba watuhumiwa wa 1983 waliteswa, inabidi uthibitishe kwamba sheria za Tz zinaruhusu ushahidi uliopatikana kwa kumtesa shahidi.
Ndiyo , Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaruhusu ushahidi uliopatikana kwa njia ya utesaji hasa huo ushahidi unaposababisha kupatikana au kugundulika kwa kitu au jambo fulani
 
Mimi ni MATAGA ila mbona nahisi kudharirishwa na kufedheheshwa na uzi huu wa MATAGA mwenzangu?
 
Kweli kabisa mtu aliiona ya vyombo vya habari nyakati hizo waliandika kila kitu. Mbona Nyerere alikuwa haogopi vyombo vya habari mpaka kuviachia vifanye kazi kwa huru namna ile!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…