Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla
Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama
Napenda kuwashauri hivi;
Embu jitahidini kusoma na kujua angalau kidogo historia ya nchi hii na nadhani itawasaidia kidogo
Wanajeshi wa kesi ya Mbowe si watu wa kwanza nchini kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama vya Tanzania baada ya kufanya Jinai.
Mwaka 1981, Wanajeshi kadhaa akiwemo Komando Tamimu, Kapteni Kadego,Kapteni Maganga, Luteni Zacharia Hanspope, Kapteni Maghee na wenzako walifanya mpango wa kutaka kuiangusha Serikali ya Awamu ya kwanza.
Kwenye mipango iyo Walishirikiana na Wanajeshi wenzao akiwemo Luteni Ndejembi( Ambaye alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma- Ni baba Mzazi wa Naibu Waziri Ndejembi, Mbunge wa Chamwino)
Wakati wanapanga mipango yao Ndejembi na wenzake waliwaripoti kwa Mkuu wa Usalama Jeshini . Enzi izo alikuwa Luteni Kanali Davis Mwamunyange ( Ambaye Kwa sasa ni CDF Mstaafu )
Baada ya mipango iyo kusanuliwa Vikosi vya ulinzi na Usalama ( JWTZ, TISS na Polisi) walifanya operesheni maalumu iliyowezesha wanajeshi hao wote kukamatwa na kuuwawa kwa Komando Tamimu ambaye aliuliwa akijaribu kutoroka. Wanajeshi hawa ukisoma kesi hii walipitia msoto wa uhakika ikiwemo torture ili kupata kiundani mipango yao
Kesi ilienda Mahakamani na watuhumiwa wote walihukumiwa vifungo gerezani! Kesi iyo iliendeshwa na Wakili wa Serikali matata aliyejulikana kama Sekule ambaye alikuwa DPP na baadae akaja kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kwa maelezo haya napenda leo kuwahusia Bavicha na Chadema, acheni kuanzisha vi thread vyenu uchwara ambayo vinaonesha hamjui historia ya hii nchi. Kama mnadhani mnaleta uchonganishi basi jueni mnakosea sana. Vyombo vya dola vya Tanzania vinafanya kazi kwa utaratibu maalum na ndo mana nchi iko salama miaka yote hii tangu Uhuru
Poleni sana Bavicha na Chadema!
Mbowe haponi!
..naona kama umekuwa na haraka kidogo kuleta habari hii.
..sio kweli kwamba washtakiwa wote ktk kesi ya uhaini ya mwaka 1984 walipatikana na hatia.
..wako baadhi ya watuhumiwa ambao waliachiwa huru.
..pia suala la TORTURE halikuwa prominent na wazi kama ilivyo ktk kesi hii.
..vilevile upande wa serikali ulikuwa na mashahidi wengi, tena baadhi wakiwa ni askari active na senior officers ndani ya JWTZ.
..kesi hii inaelekea kuwa ya Polisi peke yao, na so far ushahidi unaonekana ni mwembamba, na mashahidi ni wachache.
..lingine ni kwamba wakati ule Polisi walikuwa wanafuata taratibu na walikuwa wawazi kuhusu watuhumiwa. Kwa mfano, haikuchukua muda mrefu toka watuhumiwa kukamatwa mpaka kufikishwa mahakamani.
..Serikali iliwaalika shirika la kutetea haki za binadamu AMNEST INTERNATIONAL kuja kuhakiki kwamba watuhumiwa wa uhaini wa mwaka 1984 walikuwa ktk mikono salama.
..Sina uhakika kama kamanda Sirro yuko tayari kualika mashirika ya kimataifa kuhakiki kwamba mahabusu wetu hawateswi na kutendewa kinyume na taratibu.
..kwenye kesi hii kuna walakini kwamba " ring leader " Mbowe aliachwa mtaani kwa muda mrefu bila ya kukamatwa.
..Hivi kweli unaweza kuwa na kesi ya ugaidi halafu mpanga ugaidi akaachwa mtaani akiendelea na maisha?
..Watuhumiwa watatu walishafikishwa mahakamani huku " ring leader " na sponsor wa tuhuma zao akiwa mtaani, akitoka na kurudi nchini.
..Kigugumizi cha kumkamata " ring leader " wa huu ugaidi kinaleta mashaka kuhusu uzito wa hizo tuhuma. Nikukumbushe kwamba wale watuhumiwa wa 1983 walikamatwa haraka sana bila kigugumizi hiki tulichokishuhudia safari hii. Na " ring leader " alikuwa ni raia Thomas Lugangira " uncle tom. "
..Lingine ambalo hukulieleza ni jitihada za watuhumiwa wa mwaka 1983 kukwepa mkono wa dola. Wako watuhumiwa ambao walitoroka gerezani na kukimbilia Kenya.
..Sasa mwaka huu tunaambiwa " ring leader " alikwenda zake Dubai, Kenya, na Ulaya, halafu akarudi Tanzania. Yaani hakuwa na harakati zozote zile za kutoroka wakati vijana wake wamekamatwa.
..Lugangira bosi wa watuhumiwa wa mwaka 1984 alipopata nafasi ya kuchomoka alitorokea Nairobi na kutokomea Uingereza ili kukwepa mkono wa dola hapa Tanzania.
..Tofauti nyingine inahusu utoaji wa taarifa kuhusu mwenendo wa kesi. Mwaka 1984 magazeti yote yalikuwa yanatoa taarifa za kesi ya uhaini kwa uhuru na uwazi. Nazungumzia magazeti ya chama na serikali kwa wakati huo.
..Kipindi hiki sioni jitihada za vyombo rasmi vya habari kueleza kinachojiri mahakamani. Hali hiyo inatoa nafasi kwa watu wasio na utaalamu kuripoti kuhusu kesi ambayo naaamini wananchi wanapaswa kupewa taarifa sahihi.
..La mwisho, ni kuhusu timu za mawakili walioshiriki ktk kesi ya uhaini ya mwaka 1984.
..Upande wa utetezi ulikuwa na mawakili mahiri na machachari kwelikweli. Hapa nawazungumzia watu mawakili kama Murtaza Lakha, Tarimo, Mucadam, na wengine.
..Upande wa mashtaka uliongozwa na William Sekule, akisaidiwa na kina Kulwa Massaba, Johnson Mwanyika, na wengine. William Sekule alifanya kazi kubwa sana ktk closing arguments.
..Kesi ilisikilizwa na Jaji Kiongozi Nassoro Mnzavas.