Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

ni kweli,

kuna changamoto mbali mbali kwetu Tanzania...............wangekuja na alternative solutions,tungewaheshimu more...........

its time, kuwork with government,not to work against.....

maandamano haya achieve chochote,
 
Pasco bwana!
Sasa Chadema wakisikiliza Ushauri wako si kitakoma kuwa chama cha siasa, maana ground za kufanyia siasa zote zinapigwa libiti!
Grounds zipi za kufanya siasa? Si wanatakiwa kumuandikia ocd tu na akiridhia wanafanya tu! Acha kushikishwa UKUTA.
 
MLAPUNDA soma hii
 


SOMA HAPA KWENYE LINK UTAMJUA NYERERE NI NANI Mohamed Said: MWL. JULIUS K. NYERERE, KANISA KATOLIKI NA UISLAM: DOLA NA TATIZO LA UDINI TANZANIA
 
Kama reference yako ni huyu mdini Mkuu humu jf, endelea, jamaa kasomeshwa na misheni lakini Shukrani hana! . Kwa kukusaidia tuu, misheni ndio kila kitu na akiwa Mkristu ni lazima awe Mkatoliki, alianza Juliasi, akaja Benyamini na sasa nI Yohana, ni chaguo la Kurasini japo muungwana alimtaka Benado pia wakamleta Petiro ili kumtumia kama kichinjio cha kumchinjia Eduadi.

Tena Nyerere ni wa kumshukuru sana maana asingeifutilia mbali ile jumuiya ya mujahidina, saa hizi na sisi tungekuwa kama Somalia! .

Pasco
 


Katika kitabu chake Bw. Bergen, kiitwacho Development and Religion in Tanzania, katika Ukurasa wake wa 98 mwanadishi huyo anasema:- “Catholic Missionaries came to East Africa to find not new churches, but new provinces of the Roman Church” Kwa mujibu wa tafsiri yangu “Wamishionari wa Kikatoliki hawakuja hapa Afrika ya Mashariki kwa minaajili ya kuasisi Makanisa mapya, bali walikuja kuunda majimbo mapya ya Kanisa la Roma”. Ni kwamba, Tanzania (Tanganyika) ipo Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa mwandishi Bergen, Tanzania nayo ni moja ya majimbo ya Kanisa la Roma, au kwa lugha nyepesi tuseme Tanzania ni Koloni la Vatican! Je, ni kweli Tanzania (Tanganyika) ni Koloni la Vatican? Padri. Dk. Sivalon, naye katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara (1953-1985) anaeleza bayana kuwa Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa nchi yetu, alikuwa kiungo pekee kati ya Chama (CCM), Serikali na Kanisa Katoliki.

Na kwa msingi huo viongozi wa Kanisa wamekuja kuwa na nafasi ya pekee kuelekeza hisia, mitazamo na siasa ya Tanzania, na wamefanya hivyo wakipania pia kuwa kuhujumu Uislamu. (Msomoe Sivalon Uk. 5-6,
katika kitabu chake hicho). Naye m mwandishi Bergen katika kitabu chake amemnukuu Mwalimu Nyerere akisema kamwe hawezi kwenda kinyume na kanisa lake. (Bergen Uk. 335). Agosti 3, 1970 Mwalimu Nyerere, alimwita Ikulu Padri Rweyemamu katika mazungumzo maalum ambapo Nyerere alimuahidi Rweyemamu kuwa, hivi sasa Kanisa ndilo lililoshika hatamu za kuongoza dola naye atahakikisha hali inaendelea kuwa hivyo. “Tanzania is not Catholic country, but Catholics is strong, I want to give the church a better chance here”. Akiwa na maana kwamba:- japo “Tanzania si nchi ya Kikatoliki, lakini Ukatoliki una nguvu, hivyo nataka kulipa Kanisa nafasi ya pekee hapa nchini” (Msome, Bergen Uk. 335). Na hali hii ya Kanisa kuwa na nafasi kubwa Serikalini iko wazi.

Waandishi wote hawa wanatuthibitishia kuwa, kuna ukweli fulani kwamba yapo mafungamano ya dhati kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Tanzania. Ni mafungamano hayo hayo ndiyo yameendelea kuwapa uweza viongozi wa Kanisa Katoliki kutoa maelekezo, maagizo na vilio vyao Serikalini na wakasikilizwa pamoja na kutekelezwa yale wanayoyahitaji hata kama yamelenga kuleta maafa kwa Waislamu. Mfano, mwaka 1998, Padri Lwambano, ambaye ni Paroko wa Kanisa Katoliki Mburahati Jijini Dar es Salaam, alisema kuiambia Serikali:- “Lazima Serikali ichukue hatua kali sana kwa Waislamu wanaoendesha Mihadhara, sababu ni watu wabaya kabisa, nimepita Sinza na Mwembechai, nimekuta Waislamu hao wanamtukana Yesu wanasema Yesu si Mungu”, alisema Paroko huyo na kuongeza; “Kama Serikali imeshindwa kuchukua hatua kali kukomesha Mihadhara ya Waislamu na kuendelea kutupaka matope kwa mgongo wa chupa, Serikali hii ijue sisi tutalishughulikia jambo hilo kwa nguvu zetu zote”.

Kauli hii ya Padri Lwambano, ilirushwa hewani na Kituo cha Radio Tumaini kinachomilikiwa na Kanisa hilo hapa nchini, Februari 13, 1998. Padri Lwambano bila kujali kuwa imani yake inaamini ‘Yesu ni Mungu’ na Waislamu imani yao inaamini ‘Yesu si Mungu’, aliinyooshea kidole Serikali nayo ilifuata bila kujali yenyewe (Serikali) haina dini na raia wake wana dini, kwa imani tofauti.

Katika utekelezaji wa agizo hilo bila shaka kila mtu anakumbuka kilichotokea. Ama kwa wale ambao walikuwa ni wadogo kipindi hicho ni kwamba Jeshi la Polisi lilifika Msikiti wa Mwembechai na kuuwa Waislamu kwa risasi na kikumbukumbu ni maarufu kwa ‘Mauaji ya Mwembechai’. Kufuatia madai hayo ya Padri Lwambano, viongozi kadhaa wa nchi walifikia hatua ya kuliomba radhi Kanisa Katoliki na Wakristo kwa ujumla. Majina na vyeo vya viongozi hao wakuu wa Serikali yanafahamika.

Baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi la Polisi, kazi ya kukatili maisha ya Waislamu na kubaka haki zao, kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini Polycarp Kadinali Pengo, aliipongeza Serikali kwa upande mmoja na Polisi kwa upande wa pili kufuatia mauaji hayo hayo ya Waislamu, Mwembechai. Pongezi hizo alizitoa April 12, 1998 wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Dar es Salaam (DTV). Kanisa likionekana kuuchukukia vilivyo Uislamu, liliongeza harakati za siri na za wazi na kwa kutumia nguvu za dola ili kupunguza kwa upande mwingine nguvu ya Uislamu, maana kuuzima kabisa ni jambo lisilowezekana.

Askofu Mkuu Pengo alitoa taarifa ya kuenea Uislamu hapa Tanzania huku akihitaji msaada wa hali na mali katika kuhidhibiti hali hiyo. Na kwa kweli, Serikali ilitekeleza kudhibiti Mihadhara na Wahadhiri, ambapo wahadhiri maarufu nchini wakiongozwa na Habib Mazinge, walitiwa mbaroni na kutupwa Magerezani. Aidha sehemu ya taarifa yake ilisema hivi; “Uislamu umekuwa tishio kubwa sana kwa imani ya Kikristo nchini Tanzania, iwapo mihadhara ya Waislamu itaachwa iendelee, Kanisa litegemee kukimbiwa na waumini wake na kusilimu, kwa hiyo juhudi lazima zifanywe kuzuia Mihadhara hiyo.

“Tunashindwa kujibu hoja zao Waislamu sababu zina ukweli ndani yake”, maelezo haya yanapatikana katika kitabu cha Askofu Pengo kiitwacho Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwenye vijilia Sinodi ya Maaskofu wa Afrika kwa ajili ya Afrika.
 
S
Sheria ipi inayohitaji maandamano yawe na kibali, hususan kibali cha polisi?
 
S
Sheria ipi inayohitaji maandamano yawe na kibali, hususan kibali cha polisi?
Kila sheria inatungiwa kanuni za utekelezaji, kwenye kanuni ndipo lilipo hitaji la kumwarifu OCD kwa maandishi na OCD atoe kibali kwa maandishi kuwa atapawatia Usalama.

Ikitokea siku hiyo ndio siku ya seminar elekezi kwa askari, hivyo kukawa hakuna askari wa kutosha, au wakipokea taarifa za kiinteligensia za uvunjifu wa amani na Usalama, then OCD atawajibu kwa maandishi kuwa hakuna kibali cha kuandamana wala mikutano!, kwa hoja ya kutokuwepo askari wa kutosha kulinda amani, ila mkiandamana bila kibali askari wa kutosha kuzuia maandamano watapatikana.

Pasco
 
Circuses
 
Nimesoma hiyo link na hiki ndicho nilichokupa comment kwenye linki hiyo.

Leo nimeelekezwa na mtu kule jamiiforums kuja bandiko hili. Niliposoma tuu Chapter 1 na kukutana na urongo, nimeishiwa nguvu kuendelea kusoma! . Mwandishi anasema Wamishenari walikuja Africa Mashariki ili kuutokomeza Uislamu!. Huu ni uwongo mkubwa wa mchana kweupe wenye nia ovu, "the ill motives behind ". Wamishenari walikuja kueneza dini na walioenda mahala pengi hata kule ambako hakuna Uislamu kabisa! .

Ukiishaweka urongo mmoja tuu, hata kama kuna ukweli 99, ule ukweli wote unakuwa dismissed na urongo mmoja tuu! .

Wewe mwandishi mwenyewe hiyo elimu yako umeponea shule ya misheni, wasingekuwepo saa hizi ungekuwa wapi? !.

Pasco
 
Asante, tumekuelewa, sasa turudi kwenye mada iliyoko mezani.

Kuleta hoja za udini ni dalili ya kuwa mufslisi wa hoja, udini huu peleka huko kunakohusika.

Hapo tuendelee kukata issue iliyomo mezani.

Pasco
 


Hiyo elimu yako ya misheni imekusaidia kitu gani ?? Zaidi ya kuhesabu namba na kutapatapa kujipendekeza huku na kule ?? Hufahamiki mara unawaonya chadema mara unataka kwenda kwenye maandamano , umekuwa hufahamiki unataka kitu gani ?

Mara ujipendekeze kwa Magufuli , mara Magufuli ni Dikteta mara Magufuli anahitajika kuwa dikteta

Ni vizuri ukamwona psychiatric NAMBA UNAZISOMA KINYUME NYUME
 
Asante, tumekuelewa, sasa turudi kwenye mada iliyoko mezani.

Kuleta hoja za udini ni dalili ya kuwa mufslisi wa hoja, udini huu peleka huko kunakohusika.

Hapo tuendelee kukata issue iliyomo mezani.

Pasco


NILIKUWA NAKUFAHAMISHA HUO UDIKTETA WA NYERERE LAKINI NJAA INAKUSUMBUA UNAJIFANYA HUTAKI KUSIKIA

SIKILIZA VITABU VYA KIKATOLIKI VINAVYOSEMA au navyo ni kama unavyosema ni

"the ill motives behind ". ???????

 
NILIKUWA NAKUFAHAMISHA HUO UDIKTETA WA NYERERE LAKINI NJAA INAKUSUMBUA UNAJIFANYA HUTAKI KUSIKIA

SIKILIZA VITABU VYA KIKATOLIKI VINAVYOSEMA au navyo ni kama unavyosema ni

"the ill motives behind ". ???????

Asante nishafahamu sasa turudi kwenye mada iliyo mezani.
Nitamuomba mode jukwaa la dini liwe public ili hawa wafia dini wamalize hasira zao huko.
Pasco
 
Unaniona kama sina msimamo kwa sababu sina kabisa upande niliiegemea, mimi niko kwenye total neutrality ndio maana Ufipa naenda, Lumumba naenda na Buguruni Mnyamani pia naenda! .

Sifungamani na chama chochote cha siasa bali ukweli pekee.

Pasco
 
Big up Pasco!! ushauri mzur sana...Wahenga walisema asiye sikia la mkuu huvunjika guu...wasipokusikia shauri yao
....yetu macho hyo sinema ya tar moja sept.
 
Uonekane hiyo tarehe moja, sio unatoa maneno kwenye mitandao alafu tar 1 ujifiche.
 
Unaniona kama sina msimamo kwa sababu sina kabisa upande niliiegemea, mimi niko kwenye total neutrality ndio maana Ufipa naenda, Lumumba naenda na Buguruni Mnyamani pia naenda! .

Sifungamani na chama chochote cha siasa bali ukweli pekee.

Pasco

Usijidanganye nafsi yako wewe ni mtu unayeganga njaa na ndio ukajifanya eti uko neutral . Njaa kitu hatari . Umekua kama paka lenye mikia 9 .Opportunist kinoma. Mara umgeukie magufuli dikteta mzuri. Mara uwageukie chadema msiandamane mara unawaambia chadema nitakuja kuandamana kupinga udikteta . Unafiki mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…