Pre GE2025 Ushauri kwa Kassimu Majaliwa: Mjomba kesho yako imevurugwa kwa Makusudi, fuata nyazo za Dkt. Mpango Philip

Pre GE2025 Ushauri kwa Kassimu Majaliwa: Mjomba kesho yako imevurugwa kwa Makusudi, fuata nyazo za Dkt. Mpango Philip

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu naomba kujua kwa sasa PM yupo wap? Maana kwenye summit sijamuona sina kumbu2 kw Mara ya mwisho nmemsikia lini ila nadhan wakati wanafunga bunge! Au nafas yake imekasimiwa au kukaimiwa na mtu? Ambae anafanya majukum kama yy?


Sitaki kuamini Nwm kama anakaim? Au anafanya majukumu yake kama naibu!
Yaani hata mimi nashangaa, naona ni mwendelezo wa Sabotage,kuvurugana kabla ya mwezi wa saba!!

Ningekuwa mimi najudhuru kabla ya mwezi wa saba, na bila notification kwa mkuu wa nchi, na kupost resignation letter kwenye social network ila aendelee Naibu waziri kumalizia uwaziri mkuu!!
 
Waziri Mkuu akishastaafu katika huo wadhifa hawezi kugombea Ubunge !
Wenye kulitaka hilo jimbo wajiandae tu !
 
Kassim Majaliwa ikifika mwezi wa kumi mwaka huu atakuwa kafikisha miaka 10 ya kuwa waziri mkuu.

Sawa na Fredrick Sumaye aliyedumu na Mkapa kwa kipindi cha miaka 10, itabidi aanze kuishi maisha ya waziri mkuu mstaafu na ataendelea kutunzwa kwa pesa ya hazina mpaka siku ya kuaga dunia.
 
Heshima kwenu,

Moja kwa moja kwenye mada husika.

Mheshimiwa PM, Mbunge wa Ruangwa "Makomasho"

Napenda kutoa ushauri wangu kwako, kuhusu upepo A.K.A "mbungo" ambayo inavuma katika viunga vya msitu wa rangi ya uhai kijani.

Jaribio la Mama kujipitisha kwa mfumo wa "hati ya dharula "certificate of emergency/urgency" ambayo iliacha watu midomo wazi na kusabisha wengi kukosa usingizi usiku wa siku ile ya mkutano.

Kadiri ya upepo ulivyo, mimi naiona nafasi yako ni ndogo sana kuendelea vema kwenye siasa za Tanzania baada ya uchaguzi mkuu huu 2025.

Dr Emanuel Nchimbi mgombea mwenza tarajali wa Samia ni team Lowasa/ambayo ni team Rostam Aziz , A.K.A "King 👑 Maker "

Rostam ,is not in favor of you ku hold nafasi kubwa Tena ndani ya Serikali, na hata Mama pasi na shaka ana mtizamo tofauti kabisa juu yako.

Nafasi Yako ilikuwa ,na ulistahili pasi na shaka wewe ndio uwe mgombea Mwenza wa Samia, lakini mambo yamekuwa tofauti na ulivyotarajia/walivyotarajia wajuvi pamoja na mimi binafsi kama self political analyst.

Chemistry imekaa vibaya., kwa hili nisitafsiriwe mimi ni mdini, la hasha!!
Zanzibar Daktari Hussein Mwinyi Muslim, Samia Bara Toka Zanzibar Muslim, na wewe Toka Bara Muslim??

Naiona nafasi ndogo ya kuwa PM baada ya Uchaguzi mkuu ujao.
Uwaziri mkuu wa 2025 October utakuwa na misingi ya dini ,na kanda, hasa kanda ya Ziwa.

Kwanini kanda ya ziwa , watasema tuleteeni "PACHA" tuna mpango naye ili zipatikane kura za kanda ya ziwa za kutosha za CCM.

Nia Yako ya kugombea tena ubunge Ruangwa ni njema sana, kwa kazi kubwa nzuri uliyofanya kwa watu wa Ruangwa miundombinu ya Afya, Elimu na kikubwa zaidi ni barabara ya lami Nanganga, Ruangwa to Nachingwea, kwakweli tunakushukuru.

Pamoja na hayo yote, naona sio vizuri wewe kurudi bungeni ukawe mbunge wa kawaida kutoka uwaziri mkuu, hiyo haijakaa vizuri mbele ya Jamii, vikubwa kwa wale ambao walikuwa chini Yako ulipokuwa PM ambao kwa maagizo Yako na maelekezo yako ya kiutawala wengine walionankama wanachapwa bakora, Kwenzi au "Njingo" nkokota.

Natamani sana kuona haugombei Tena ubunge Ruangwa, sio kwamba sipendi haugombei la hasha!! unless una ahadi isiyo na shaka na Mama ya kukurudisha umalizie U PM kwa miaka mitano ijayo ili mumalize safari pamoja.

Nasema hivyo kwa vile chemistry ili ikae sawasawa ni muhimu PM awe Mkristu, VC Mkristu , Rais Zanzibar Mwislamu na Rais Bara ni Mwislamu.

Ingawa pia niweke "benefit of doubt " bonafide ,kwamba hiyo sio kanuni inaweza isifuate hivyo ila tu ni tahadhari ambayo naiona kwa jicho pekenyevu na fikra tunduizi.

Mwisho Mwishoni natamani kwa kweli kwa ajili ya heshima yako uliyojijengea mbele ya jamii, ni vema ukatafakari ikikupendeza kufuata nyayo za Mzee wetu Daktari Philip Mpango.

Nakuangalia sana katika medani za Siasa kwa sasa ndani ya CCM ulistahili hata kuwa kiongozi mkuu wa nchi yetu,lakini mazingira ya siasa,Kuna hila za makusudi , ghiriba, husuda za kuzima nyota yako utoke nje ya duara mapema.

Leo hii wewe unavokubalika kanda ya ziwa, ambayo watu wanaona sura ya Mwamba Jiwe ndani yako ilikuwa ni turufu tosha CCM kupata votes nyingi bila kumtumia "pacha"

Lakini bahati mbaya mfumo hauendi kadiri ya matakwa yetu.

Kugombea ubunge Ruangwa Leo ni sawasawa na kucheza kamari Gambling, unaweza kigombea na Mama akabadili gia angani akakuteu Tena uwe PM.

"To choose between two equal,is bad alternative in serious dillema.

Watu wa Ng'au ,Chimbila, Nanditi,Manokwe,Chiepo,Mandambe,Mandarawe,Ole, Nanguruwe,Namahema,Nnindu,Nkowe,Kipindimbi, Mitope na Likunja kuwataja wachache, wangetamani sana kuona heshima yetu inasimama mahali pake kutokana na upepo unaoendelea Chamani.

Mimi ni mdogo kiumri Sina mang'amuzibya kutosha,ila naona tu Mungu ameniongoza hivyo,Sina nafasi ya kukuona, Mwishoni mwa mwaka nilisafiri ili kupata angalalau nafasi tutete lakini protocol hazikuruhusu

Ndimi "Mjomba"

Nandagala one, Mpumalanga Afrika Kusini.
🙏🙏
Waziri mkuu kamaliza ten years apumzike tu hakuna namna ,tuongeze wastaafu wanaokula keki ya taifa
 
Huna kazi ya kufanya mpaka uandike hizi porojo za kipuuzi. Mtu amekuwa waziri mkuu miaka 10 bado unataka sijui awe nano, kwa lipi alilonalo? Watanzania wenye sifa zaidi yake ni wengi sana apumzike. Halafu issue ya kanda ya ziwa ni ya kipuuzi, kwanza hakuna kitu kinaitwa kanda ya ziwa. hakuna utawala wa ukanda nchi hii. PM huteuliwa baada ya uchaguzi mkuu sasa mambo ya kura ya kanda ya ziwa yanahusiana vipi na PM kuteuliwa kutoka hiyo kanda ya kufikirika. Ujinga huo uliletwa na yule mshamba wenu marehemu. Sema wasukuma msijifiche kwenye blanketi ya kanda ya ziwa. wasukuma ni watu wachache sana kulinganisha na watanzania. Hawana impact yoyote kwenye uchaguzi mkuu. Mikoa iliyoko kanda ya ziwa ni makabila tofauti yenye misimamo, mila na desturi tofauti kabisa. Msilazimishe upumbavu wenu kutumia jina kanda ya ziwa. Semeni nyie washamba wasukuma mlioonja upendeleo. Huo ubaguzi na upendeleo haupo tena umeshakufa na yule mshamba wenu Magu.
Siku utakapojua watu wa Kanda ya ziwa wanaitana home boy na home girl ndio utajua kwanini neno Kanda ya ziwa kwenye campaign za wanasiasa linatajwa sana na ni muhimu sana ,unafikiri ccm na chadema kwanini wanapenda kuzindua campaign Kanda ya ziwa na kufunga campaign Kanda ya ziwa?
 
Waziri mkuu kamaliza ten years apumzike tu hakuna namna ,tuongeze wastaafu wanaokula keki ya taifa
Ndivyo nilivyoshauri kama umesoma vizuri!! Unless kama Mama anataka kumwongezea muda wamalize wote
 
Siku utakapojua watu wa Kanda ya ziwa wanaitana home boy na home girl ndio utajua kwanini neno Kanda ya ziwa kwenye campaign za wanasiasa linatajwa sana na ni muhimu sana ,unafikiri ccm na chadema kwanini wanapenda kuzindua campaign Kanda ya ziwa na kufunga campaign Kanda ya ziwa?
Mpe dozi haijui maana ya Demografia!!
 
Angekaa kimya kama kazi haikuwa yake! Kujitokeza na kusema mtu yuko anafanya kazi ili hali alishakuwa maiti halikuwa Jambo la kiungwana .
From that point on , he was no longer credible.
Tena akiwa msikitini 😀 very sad moment at that time.
 
Kwakweli sijui, yupo Jimboni kwake? Yupo Dodoma, yupo DSM?? ila nimeshanngaa kuona Dotto Biteko yupo kwenye mkutano wa nishati kwa kofia ya Naibiu PM, wakati PM yupo.

Pia mkutano wa nishati unahusu Marais na mawaziri wa fedha 🤔🤔🤔🚴🤔
Acheni kukuza mambo Dotto Biteko yuko pale kama waziri wa Nishati na mkutano wenyewe ni wa Nishati hajaenda pale kwa title ya naibu waziri mkuu. Mkutano ni wa wakuu wa nchi mkuu wa nchi yupo mbona hauulizi kutokuwepo kwa makamu wa rais na rais wa Zanzibar?
Kuhusu PM yuko wapi jpili alikuwa huko simiyu akiendeleza uchawa wake wa mitano tena akiwa kwenye shati lake la kijani pia leo alikuwa bungeni Dodoma.
 
Acheni kukuza mambo Dotto Biteko yuko pale kama waziri wa Nishati na mkutano wenyewe ni wa Nishati hajaenda pale kwa title ya naibu waziri mkuu. Mkutano ni wa wakuu wa nchi mkuu wa nchi yupo mbona hauulizi kutokuwepo kwa makamu wa rais na rais wa Zanzibar?
Kuhusu PM yuko wapi jpili alikuwa huko simiyu akiendeleza uchawa wake wa mitano tena akiwa kwenye shati lake la kijani pia leo alikuwa bungeni Dodoma.
Mkutano ule unawahusu mawaziri wa fedha na Marais tu, wewe ndo unakuza mambo ,eti doto kama waziri wa nishati 😅🤣🤣🤣 unachekesha sana
 
Back
Top Bottom