mimi ni mwislamu na nimetoa ushauri kwa mwislamu wala sijagusia maswala ya kiserikali au kinchi hapa wala sija... sasa nashangaa matusi kwa kwenda mbele sijui kilichokukereni ni kipi?. vinginevyo angekuja shekhe hapa anielimishe hiyo "kwa jina la jamhuri" kama haina shirk ili niondokane na hiki ninachokielewa kuhusu kauli hiyo.
narudia tena "SALAMU TUNAYOELEKEZWA KUTUMIA WAISLAMU NI ASSALAAMU ALAYKUM" nyinyi wengine salimieni vyovyote mlivyofundishwa lakini ninachokazia ni kwamba JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KAZI IENDELEE siyo salamu bali ni kibwagizo kama watumishi wasemavyo solidarity forever (mshikamano daima) au wanamichezo wanavyosema michezo safii
narudia tena kushauri watu (hasa waislam akiwemo mama yangu rais samia) wasiseme "...kwa jina la jamhuri ya muungano wa tanzania" bali waseme tu "jamhuri ya muungano wa tanzania" kuitikia kutabakia ni vilevile kwamba "kazi iendelee"
na mwenyezimungu ndiye mjuzi zaidi