Ushauri kwa Rais Samia kuelekea Mei Mosi: Usipandishe mishahara kwa wafanyakazi, bali punguza Kodi/PAYE

Ushauri kwa Rais Samia kuelekea Mei Mosi: Usipandishe mishahara kwa wafanyakazi, bali punguza Kodi/PAYE

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Huu ni ushauri kwa Rais wetu kipenzi Cha Watanzania, mama Samia Suluhu Hassan.

Nafahamu kwamba pamoja na Mambo mengine serikali ya mama Samia ina nia njema ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi hapa nchini wawe wa sekta binafsi ama wale wa serikalini.

Ushauri wangu kwa mama kuelekea mei mosi, asijikite kwenye kupandisha mishahara ya wafanyakazi Bali ajikite zaidi katika kupunguza Kodi inayokatwa kwenye mishahara maarufu Kama PAYE.

Unapoponguza Kodi unakuwa tayari umegusa sekta zote yaani serikalini na wale wa mashirika au taasisi binafsi.

Kodi ikipungua tayari kipato au take home inaongezeka na hii inakuwa faida au nyongeza kwa wote ( walioko serikalini na walioko private sekta)

Rais akipandisha mishahara bila kupunguza Kodi wanufaika peke watakuwa wafanyakazi wa serikalini tu.

Tunafahamu malengo ya serikali ya awamu ya sita ni kuboresha maisha ya mtanzania bila ubaguzi, hivyo ni Imani yangu kuwa Rais atapokea ushauri huu na kuufanyia kazi.

Amen.
 
Kwa mjibu wa ImF mfumko wa bei ya vitu utakua 37% kwa serikali makini mishahara ya watumishi ingepanda kwa 37% ili ku pambana na huo mfumko wa bei ya bidhaa mbali mbali, na serikali ina mbinu nyingi za kutekeleza hili,.
 
na trade union wachukue asilimia moja ya mshahara sio mbili
 
Ngoja tuone..ila kimsingi watumishi waendelee kusaga meno..chaka la kujifichia liko wazi ni vita vya U&R mtaambiwa subirini mpaka vita viishe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huu ni ushauri kwa Rais wetu kipenzi Cha Watanzania, mama Samia Suluhu Hassan.
Nafahamu kwamba pamoja na Mambo mengine serikali ya mama Samia ina nia njema ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi hapa nchini wawe wa sekta binafsi ama wale wa serikalini.
Ushauri wangu kwa mama kuelekea mei mosi, asijikite kwenye kupandisha mishahara ya wafanyakazi Bali ajikite zaidi katika kupunguza Kodi inayokatwa kwenye mishahara maarufu Kama PAYE. Unapoponguza Kodi unakuwa tayari umegusa sekta zote yaani serikalini na wale wa mashirika au taasisi binafsi. Kodi ikipungua tayari kipato au take home inaongezeka na hii inakuwa faida au nyongeza kwa wote ( walioko serikalini na walioko private sekta)
Rais akipandisha mishahara bila kupunguza Kodi wanufaika peke watakuwa wafanyakazi wa serikalini tu.
Tunafahamu malengo ya serikali ya awamu ya sita ni kuboresha maisha ya mtanzania bila ubaguzi, hivyo ni Imani yangu kuwa Rais atapokea ushauri huu na kuufanyia kazi.

Amen.
UVCCM asubuhi asubuhi mnapiga K-vant
 
Mshahara aliahidi kuuongeza,hana jinsi.Endeleeni kuumia roho,wenye hela zao wanazitaka.
 
Back
Top Bottom