- Thread starter
- #41
Bandiko hili naona limekuja na mawazo mazuri ya wachangiaji.Tatizo ni wenye nyumba, watakubali kupokea kiasi kinachobaki baada ya kulipa tozo?
Mimi nafikiri, Serikali iwe serious kidogo, kabla ya kuanzisha hizi tozo na kuzizindua waweke mazingira mazuri kwa mlaji wa mwisho.
Leo hii unataka 10% ya pango, mwenye nyumba nae anasema nataka unipe kodi yangu kama ilivyo bila kukatwa TRA utajuana nao wewe, au anaongeza kidogo badala ya sh 200 anapangisha kwa 250, hivi hapa nani anateseka?
DHIBITI BEI YA KUPANGISHA NYUMBA KWANZA. Kama haiwezekani tuondolee huu mzigo.
Bila shaka wadau huko serikalini mnafatilia maoni ya wananchi wenu.👍👍👍