Ushauri kwa Serikali: Mtu anayepinga tozo na kodi kwa maendeleo ya Taifa akamatwe

Bandiko hili naona limekuja na mawazo mazuri ya wachangiaji.

Bila shaka wadau huko serikalini mnafatilia maoni ya wananchi wenu.👍👍👍
 
UJINGA ,MARADHI NA UMASKINI BADO NI TATIZO.KAMA UNGEWEZA KUNAMBIA VAT NA TOZO NANI ANACHUKUA KWENYE MUAMALA NA UKANAMBIA MAANA YA DOUBLE TAXATION NINGEUNGA MKONO HOJA.
Swali lako watakuja kulijibu wataalam maana humu naimani wamo
 
Umesahau hii:

"Unapipinga Tozo unawakosesha usingizi walamba asali jambo ambalo halikubaliki."

Kwani utakuwa unataka walambe nini sasa?
🤣🤣🤣🤣we jamaa
 
Umeongea point muhimu sana mkuu.

Bila shaka wadau katika serikali ya Mh Rais Samia wanachukua notes na nina imani watalifanyia kazi
 
Kamua tu hadi watoe damu. Kamshahara kamepitia bank unataka kumtumia kijana ada ya shule. Unatoa ada bank TOZO,unaweka kwenye simu unatuma TOZO, anatoa kwa agent TOZO-je tutafika?
Hahahaa hili nalo watalitazama
 
Ingekua vizuri kama ungeshauri wanaobainika kufuja mali za umma na mafisadi wafilisiwe mali zao ingekua vizuri zaidi. Kuliko kupambania kulipa tozo alafu wakazifaidi wachache.
Lakinj sheria za kudhibiti uhujumu uchumi na ufisadi zipo na zinafanya kazi.
 
Hakuna mtu anaeunga mkono swala la tozo kwahali hiyo mtakamata wengi na nagereza yatakuwa machache.
Wanaendelea kuelimishwa nadhani bado hawajajua umuhimu wa jambo hili. Kwa mujibu wa tafiti za Twaweza jana waliripoti kuwa acceptance ni 60%.

Hii ndogo iliyobaki ya 40 wataendelea kuelimika kidogo kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…