Ushauri kwa Serikali na Huduma za Jamii Tanzania

Nalitupia hili hapa.

Hivi hao wawekezaji tunaoambiwa wanawekeza na kuongezeka bwelele, wananchangia nini kwenye huu Uchumi wetu?

Ninavyofikiri kuwa, uchumi unavyo kua na Huduma za Jamii ndivyo zinavyo kua, au?
Nisaidieni.
Uwekezaji siyo muujiza, haulipi leo na kesho. Soma kuhusu ROI katika uwekezaji.

Kikiubwa tunachofaidika kuanzia mwanzo wa uwekezaji ni ajira. Faida zingine huja baada ya wawekezaji kurudisha gharama zao.
 
Hata sahivi unalipia, si una lipa kodi na wao wanalipwa mishahara? tatizo ni mfumo mbovu wa CCM
 
Suala la rushwa ni kwa serikali karibu zote za Afrika. Lazima tutibu kwanza mzizi wa tatizo.

Mishahara mingi ya wafanyakazi wa serikali ipo chini haikidhi uhalisia wa maisha.Hivyo wanajiongeza kwa kuomba rushwa.
Tatizo la rushwa Tanzania linaanzia juu kushuka chini, utachukuaje rushwa kama boss wako siyo mla rushwa? Waziri kituo chake cha kazi kipo Dodoma analipwa perdiem 470,000 na yupo Dodoma(Bungeni) na wakati kuna VEO anadai nauli yake ya likizo 30,000 anazungushwa kila siku na ni halali yake, why asichukue rushwa kwa mnyonge wake ambaye ni mwananchi? Katibu Mkuu wa Wizara anajilipa per diem 250,000 siku 20 kuzunguka mikoani matokeo yake anaenda siku 3 anarudi ofisini hiyo siyo rushwa? mfumo wa kijinga uliopo umeletwa na CCM
 
Nilienda siku moja kupata huduma kwa VEO hana karatasi wala printer ikabidi nitoe pesa akachapishe pamoja na kutoa copy, nilipiga naye story akasema tangu ameajiriwa 2019 amewahi kupewa ream paper moja tu kutoka kwa DED, unategemea huyo mtu afanyeje kuwahudumia wananchi? nami nilimhurumia nikampa elf 5 ya vocha, tuna mfumo wa kijinga sn, pesa za kulipana posho nono wanazo lakini siyo za kutoa huduma kwa wananchi
 
Eh hujazoea tu matukio + uzembe wa fire
Hivi tuwalaumu fire au ilaumiwe serikali

Ova
 
Zaidi ya miaka 60 ya uhuru mnaongoza nchi ambayo bado ni maskini wa kutupwa.

Hamna mnachoweza.

Nini kimewashinda kuifanya nchi iwe na trillion dollar economy?
Kuna kaa laana fulani

Homeboy

Ova
 
Baada ya wiki Moja tu jembe JPM kulala mavumbini kila kitu kilirudi kama awali.niloshangaa sana hili ni kasema hii nchi ya ajabu sana
 
hiyo kawaida ya uongozi wote duniani, lazima muwepo mnaolalamika bila kuleta njia kifanyike nini.

Mapapai yaliyovunda hayajifichi.
Kama wananchi kinachotakiwa nikubadili chama ndio suruhisho. Kumbuka huwezi kutatua tatizo kwakutumia njia ileile uliokosea na utegemee kupata matokeo tofauti lakini ulivyo sikio lakufa huwezi kuamini.
 
Baada ya wiki Moja tu jembe JPM kulala mavumbini kila kitu kilirudi kama awali.niloshangaa sana hili ni kasema hii nchi ya ajabu sana
Kwani ilikwisha, sisi yeye ndiye aliwapa "go ahead" mapolisi kwa " za kupigia polish viatu?
 
"Platinum Member" umewaaaazaa na kuwazua ukaja na hii.. ujinga mtupu. Yaani CCM imeshindwa kuthibiti rushwa mkaona hio iwe fursa kwenu na kuwapa mzigo tena wananchi. Na hio huduma ikiwa ya kulipia hizo hela zikienda kwenye miradi n.k mwende mzipigee tenaa.. ujinga mtupuu
 
Uwekezaji siyo muujiza, haulipi leo na kesho. Soma kuhusu ROI katika uwekezaji.
Kwa msingi huo, kwanini unaona miaka miwili ya Samia haitoshelezi kurejesha uwekezaji/faida kwa Wananchi?
Kikiubwa tunachofaidika kuanzia mwanzo wa uwekezaji ni ajira. Faida zingine huja baada ya wawekezaji kurudisha gharama zao.
Sawa, hayo hata Darasa la Saba anaweza kudadavua.

Turudi kwenye hoja yako ya msingi kwamba Serikali haikusikilizi, kwamba Rushwa imekithiri, kwamba huduma za kijamii au za kiserikali zianze kulipiwa.

Ni dhahiri umekerwa wakati ukitafuta huduma katika hayo maeneo uliyoyataja-Mahakamani, Polisi n.k Lakini kikubwa ni Rushwa na kukosekana kwa Sheria au sera madhubuti za kupambana nayo.

Je, unafikiri Wawekezaji wataweza kuja kutatua masuala/kero hizo? Badala ya Serikali kusimamia Huduma hizo? How?
 
Nilileta wazo huduma za Kipolisi ziwe "private", Sasa nimeboresha wazo "privatization" ianzie serikalini wapate ujuzi.

Hizo idara zote zinazotowa huduma za bure ziwe ni vyanzo vya pesa na watu walipwe vizuri rasmi, badala ya kuteswa raia.
KUNA KITU HAPA unakumbuka vyoo vya uma awali ilikuwa bure na huduma ilikuwa mbya na chafu baada ya kulipia ikawa nzuri.huduma zilipiwe kwa garama ndogo
 
Leo siju umesoma suratu kursiyu akili imechangamka vibaya sana
 
TANESCO wananchi wanalipia kila huduma... Nguzo, Meter, n.k.

Mwananchi anakamilisha kila kitu, lakini hawaendi kumfungia huo umeme unless ametoa rushwa!

Ukikaza kwamba hutoi rushwa, then utazungushwa sana... "Nguzo za eneo lenu bado hazijafika. Meter zimeisha subiri batch ijayo" n.k n.k.

Nchi hii ujinga ujinga rushwa na dharau kwenye ofisi za umma bado ni doa sugu!

-Kaveli-
 
Hayo ndio matunda ya chama chetu.
Na kwenye paragraph ya mwisho kinachoongezeka ni uchawa na bila connection hupati kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…