Ushauri kwa Serikali na Huduma za Jamii Tanzania

Ushauri kwa Serikali na Huduma za Jamii Tanzania

TANESCO wananchi wanalipia kila huduma... Nguzo, Meter, n.k.

Mwananchi anakamilisha kila kitu, lakini hawaendi kumfungia huo umeme unless ametoa rushwa!

Ukikaza kwamba hutoi rushwa, then utazungushwa sana... "Nguzo za eneo lenu bado hazijafika. Meter zimeisha subiri batch ijayo" n.k n.k.

Nchi hii ujinga ujinga rushwa na dharau kwenye ofisi za umma bado ni doa sugu!

-Kaveli-
Kwahiyo unashauri kifanyike nini hapo Tanesco?

Unaweza kutupa tukio moja la namna ulivyoelekeza ili tuhamishie post kwenye uzi wa Tanesco watupe majibu?

Maana kuja na tuhuma na wao wana uzi wao humu watakwambia tupe tukio.
 
Uzi wako umesema "huduma zote za jamii"... nami ndipo nikakupa huo mfano halisi upande wa Tanesco.

Ama Uzi wako huu unaexclude Tanesco kwavile wana uzi humu jf?

-Kaveli-
 
Mfano mwingine ni kwenye hospital... wananchi mbona wanalipia huduma na bado kuhudumiwa hadi utoe chochote kitu kwa dokta au nesi ndipo mgonjwa achangamkiwe?!

Uzi wako huu ni just nonsense.

-Kaveli-
 
Umeongelea upande wa wananchi.

Viongozi je?

Mimi napendekeza viongozi wa serikali wapunguziwe posho na serikali ipunguze matumizi yasiyo na tija.

Mfano majuzi hapa wake wa wastaafu wanadai mafao je kuna haja gani ya kuwapa hawa watu mafao wakati wanahudumiwa chakula, malazi, matibabu ya ndani na nje ya nchi, usafiri, na ulinzi saa 24.

Hata viongozi wastaafu kama rais anapostaafu waache kumlipa 80% ya mshahara wa rais aliyepo madarakani , hii ni kwanini?

Sababu ni kuwa rais mstaafu anapewa gari mpya bure , mafuta bure, walinzi , malazi , chakula, matibabu ya ndani na nje ya nchi, nyumba mpya yenye kila kitu anachosubiri yeye ni kuingia tu achilia mbali marupurupu ya kazi zingine ziada mfano leo hii Mzee Mwinyi licha ya kustaafu ni chancellor wa chuo cha Muhimbili na tusidanganyane hiki ni cheo cha bure bure lazima analipwa , je hatuna young brains za kushika nafasi hizi hadi wastaafu watafutiwe nafasi kama kansela, wenyeviti wa bodi mbalimbali na ubalozi?
 
Uzi wako umesema "huduma zote za jamii"... nami ndipo nikakupa huo mfano halisi upande wa Tanesco.

Ama Uzi wako huu unaexclude Tanesco kwavile wana uzi humu jf?

-Kaveli-
Tanesco tayari ni huduma ya kulipia na kama hujapewa huduma na umeilipia una haki ya kuwashitaki, unakuwa umeshaingia nao biashara.

Tanesco siyo huduma ya msaada kwako au kusaidiwa, tanesco ni biashara baina ya mteja na mtoa huduma.

Nakushauri kama wanakupiga dandana tafuta wakili yeyote ukapige pesa za TANESCO, kwanza wanasheria wao mkifika mahakamani wao wenyewe wanakupa mchongo wa vipi mtengeneze pesa vizurui.

Hayo ni kwa taasisi zote za huduma za kulipia serikalini. Wakikupa shida, funguwa kesi ya madai tu, wala huna haja ya wakili mzuri, wakili yeyote tu anaweza.
 
Mfano mwingine ni kwenye hospital... wananchi mbona wanalipia huduma na bado kuhudumiwa hadi utoe chochote kitu kwa dokta au nesi ndipo mgonjwa achangamkiwe?!

Uzi wako huu ni just nonsense.

-Kaveli-
"nonsense" halafu upo unachangia mada?

Basi wewe umeuzidi uzi kwa u nonsense.
 
Binafsi ni mwana CCM kindakindaki tokea ilipobuniwa 1977, kabla ya hapo nilikuwa TANU Youth League.

Ingawa ni mwana CCM lakini si kila jambo la serikali linaniridhisha, kuna ambayo tukipata nafasi tunayafikisha vikaoni lakini hivi sasa imekuwa ngumu sana kufikisha ujumbe kwenye ngazi za maamuzi, sifahamu kwanini wakati sasa hivi tunaishi kwenye dunia inayopitia kwenye miongo ya mawasiliano habari (IT).

Kwanza naishauri CCM iboreshe namna ya kuwasiliana na ngazi za uongozi pili naishauri serikali kuu, mawaziri wote mpaka Rais wa Tanzania waige mfumo wa Zanzibar wa "sema na Rais".

Kwa kukosa njia za kufikisha ujumbe kwa haraka nimeona bora ushauri wangu niutowe hapa JF, nafahamu utawafikia walengwa wote.

1) Nashauri huduma zinazotelewa bure na serikali ziwe za kulipia rasmi, kwa zote namaanisha zote. Kuanzia huduma zinazotolewa Polisi, iwe mtu ukitaka huduma yoyote ya kipolisi ulipie, kama siyo siku hiyo hiyo basi uandikiwe una deni kwa kupewa huduma hiyo na utailipa kupitia control numbers.

Rushwa imezidi serikalini, kama haujaombwa waziwazi basi utazungushwa kupatiwa huduma mpaka utie akili utowe rushwa au atokee "kishoka" wa hapo akusomeshe utowe rushwa, ndipo huduma yako ishughulikiwe.

Kwa mambo kama hayo, iwekwe wazi tu, kuwa ukienda kushitaki polisi unapewa control number unalipia unapewa huduma, na afisa ataekuhudumia atalipwa mgao wake hukohuko official kabisa.

Ili kupigana na rushwa, kama tumeshindwa kuweka sheria kali ni vyema tukaihalalisha tu malipo kwa kila huduma.

Au kama ilivyofanywa kwenye matibabu, iwekwe bima ya lazima kwa kila raia awe analipia hizo huduma, na pesa zitazotokana na hiyo bima waongezewe mishara na posho watowa huduma badala ya kuzungusha watu ili wale rushwa serikalini. Hii ni kwa wizara na idara zote zinazotowa huduma za bure kwa jamii, ambako ndiko kunakonuka uozo wa rushwa.

Kauli za viongozi kama zile za "za polish ya viatu", "kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake" zimekuwa zikihalalisha rushwa kiaina, sasa iwe ni wazi kabisa ihalalishwe kwa kuzilipia hizo huduma.

Polisi, mahakama, uhamiaji, ardhi, huduma zote za bure za manispaa. Ongezea na wewe kwengine.

Tunataka tuwe ni wateja rasmi wenye kuweza kudai haki zetu tunaponyimwa huduma kwa wakati.
Yaan kama Polisi naona wakate na leseni kabisa ni biashara wanafanya ukiwa na shida hupati msaada Hadi uwe na pesa
 
Vichekesho vingine bana, yaani mshindwe kusikilizana humo kwenye vikao vyenu ndio waje wakusikilizie humu jf?!

Iwapo rais anapatikana kwa rushwa na chaguzi za kihayawani, itakuwa unapoteza muda wako kushauri njia za upambanaji wa rushwa. Siku chaguzi za nchi hii zitaanza kuheshimiwa ndio tunaweza kupambana na rushwa. Ifahamike rushwa nchi hii inaanzia kwenye ofisi ya rais kushuka huku chini.
 
Tanesco tayari ni huduma ya kulipia na kama hujapewa huduma na umeilipia una haki ya kuwashitaki, unakuwa umeshaingia nao biashara.

Tanesco siyo huduma ya msaada kwako au kusaidiwa, tanesco ni biashara baina ya mteja na mtoa huduma.

Nakushauri kama wanakupiga dandana tafuta wakili yeyote ukapige pesa za TANESCO, kwanza wanasheria wao mkifika mahakamani wao wenyewe wanakupa mchongo wa vipi mtengeneze pesa vizurui.

Hayo ni kwa taasisi zote za huduma za kulipia serikalini. Wakikupa shida, funguwa kesi ya madai tu, wala huna haja ya wakili mzuri, wakili yeyote tu anaweza.

Unaongea pumba tu za kisiasa.

-Kaveli-
 
Vichekesho vingine bana, yaani mshindwe kusikilizana humo kwenye vikao vyenu ndio waje wakusikilizie humu jf?!

Iwapo rais anapatikana kwa rushwa na chaguzi za kihayawani, itakuwa unapoteza muda wako kushauri njia za upambanaji wa rushwa. Siku chaguzi za nchi hii zitaanza kuheshimiwa ndio tunaweza kupambana na rushwa. Ifahamike rushwa nchi hii inaanzia kwenye ofisi ya rais kushuka huku chini.
Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Ingawa ni mwana CCM lakini si kila jambo la serikali linaniridhisha, kuna ambayo tukipata nafasi tunayafikisha vikaoni lakini hivi sasa imekuwa ngumu sana kufikisha ujumbe kwenye ngazi za maamuzi, sifahamu kwanini wakati sasa hivi tunaishi kwenye dunia inayopitia kwenye miongo ya mawasiliano habari (IT).
Unaweza kuwasilisha kupitia e-mrejesho (e-Mrejesho) ila kupata majibu/mrejesho wa suala lako inaweza kuwa changamoto kwa sababu taasisi nyingi za serikali bado zinafanya kazi ki mazoea, na ukizingatia tupo zama za kula kwa urefu wa kamba baaasi unaweza usijibiwe kabisa. e-Mrejesho
 
Mfano mzuri ni jana kariakoo, moto uliotokea, hakuna huduma ya zima moto.

Sasa kwanini kujna vituo vya zimamoto kama hawana hata ubunifu wa kuwa na na malori kumi au kumi na tano ya maji wakati wote?

Au kuwa na ubunifu wa kuweka matank ya reserve -, mfano kariako ulipotokea moto karibia majumba yote yana visima vya maji.

Ubunifu unatushinda Watanzania, akili zetu zimelala sana, tunachowaza ni kulewa, ngoma, uasherati, kujionesha kwa watu na mambo ya kijingajinga tu.
Serikali yenu ya CCM ndio haina ubunifu. Walinunua magari mengi Sana ya polisi Yale ya maji washawasha wakasahau kununua magari ya Zima Moto na ambulance. Wenyewe mmeona biashara zenu zilivyoteketea Kariakoo kwa sababu mlichagua kununua magari yakukabiliana na raia badala ya kuokoa Mali zao
 
Back
Top Bottom