Ushauri kwa vijana: Kijana fanya juu chini hakikisha una check number

Bado hujasema hiyo Check number ni nini na ina msaada gani kwa kijana?

Kwa mfano msomi wa degree ya Account, akapambana kupata check number kwa kuajiriwa serikalini kama mhudumu wa kusafisha vyoo vya ofisi za halmashauri (take home mshahara wa laki mbili na nusu), ambapo anatakiwa Jumatatu mpaka ijumaa kuanzia saa moja na nusu asubuhi mpaka saa kumi jioni awepo kazini, hiyo check number inamsaidiaje?
 
Hii, kwahiyo kila mtu anataka aajiriwe kwani?
 
Haya mawazo na uchawa yametenganishwa na uzi mwembamba sana. Haya ni mawazo ya kimaskini mno na yanachochea tu upigaji. Mishahara ya serikali bila marupurupu ni midogo mno hasa sehemu ambazo sio mashirika au wakala. Mimi ninashauri familia au watu wa karibu wa hao vijana waongee nao na kuwashauri kwenye yale wanayopenda kusomea au kufanya bila kujali kuna check number au hakuna. Hata kama unachoma mahindi hakikisha unakuwa the best kwenye kuchoma mahindi. Huu uzi ni wa kuzalisha mafisadi wa baadae.
 
Acha mawazo ya kimaskini. Sasa hivi dunia ipo kwenye kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe wewe unawaza udereva. Hiyo kazi itakuja kupungua sana kama sio kutoweka kabisa.
 
Madereva wananapata hela kuliko maofisa hii ni kweli
Ila posho ya dereva na ofisa zinatifautiana ofisa daraja la II ni 150,000/-, dereva ni 100,000/-
 
Uzi ungeuweka hivi: Vijana mkitaka maisha ya kawaida yanayokaribiana na umasikini tafuta Check Number.

Bahati mbaya sana hizo kazi zote ulizotaja ziko Halmashauri hakuna hata take home ya 800K, Yaani hauingizi hata 30K per day.

Kwa udereva usichukue sample space hio moja yenye safari nyingi, Mfano Dereva wa Mkurugenzi atapiga pesa thats true.. But halmashauri moja ina madavo wangapi? Wakala ina madereva wangapi? wote hamuwezi kupata.

Uzi wako ungewashauri vijana wawe wabunifu, wasikimbilie hizo ajira ambazo hazina hata take home ya 1M.

Otherwise kama huyo kijana hana ndoto kubwa.. anataka ku afford tu bills zake kwa Mbinde.

Alfred
 
Tupeane mawazo ya Kujiajiri, hizo check number ni ngumu
 
Shkamoo Mzee Alfred.
 
Laki 8 tarehe kama hii unajikuta una buku 70 tu ndo zimebaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…