Mkuu sina shaka na maelezo mengine uliyoandika, ila kwenye ili eneo nadhani haupo sahihi sana.
Kwasasa tulipo kama nchi, Kila kitu ni bahati zaidi kuliko mipango. Kama ningepata nafasi ya kumshauri mtu, basi ningemshauri asome anachopenda, na kama vipo zaidi ya kimoja basi anaweza omba ushauri wa mawazo toka kwa watu sahihi.
Broh, serikali sio ya kuifatisha kabisa hasa kwenye mambo kama Elimu. Rejea 2012/2013 kipindi ambacho gesi asilia na mafuta viligunduliwa huko kusini, serikali ilikuja na mkakati wa kuzalisha wataalam wa maswala ya petrol, zikaanzishwa na kozi. Sasa hivi ni 2024 nenda kawatafute wale graduates wa hizo kozi ujionee.