Ushauri kwa vijana: Kubeti siyo kazi

Ushauri kwa vijana: Kubeti siyo kazi

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
961
Reaction score
533
Vijana wengi wanaishi kwa matumaini yasiyokuwepo. Wanawaza ipo siku watamla mhindi anayechezesha betting. Na imekuwa kawaida sasa hivi vituo vingi vya habari nao kuchezesha michezo ya kubahatisha.

Unakuta unaangalia runinga mara kipindi kinakatishwa kwa tangazo au kumtangaza mshindi wa mchezo wa kubahatisha unaoendeshwa na kituo hicho.

Naomba nikuambie, kamali haijawahi kumnufaisha mtu yoyote isipokuwa kumuongezea umasikini.
Kucheza kamali kunamaliza hela lakini vilevile inamfanya mtu kuwa mlevi. Kipato chake chote anachokipata anawaza kwenda kuchezea kamali.

Ajabu unamkuta mtu hela ya matumizi ya nyumbani anaipeleka kwenye kamali kwa kuamini kuwa ataweza kushinda.

Kamali kwa namna ilivyoandaliwa haina manufaa yoyote kwa mchezaji bali kwa mchezeshaji kwasababu ujanja wote wa kupanga nani ashinde na kwa kiwango gani anao mchezeshaji isipokuwa kwa betting ya mpira ambayo yenyewe vigezo vya kushinda vimewekwa wazi na ni vigumu hasa kwa mchezi kuweza kubashiri.. Sasa usiposhituka utaendelea kuwa masikini kwa kujitakia.

Unakuta mtu akili yake yote masaa 24 kaipelekea kwenye kamali, daaah msiba mkubwa huu kwa taifa na nawaonea huruma sana Watanzania wenzangu waliyonaswa kwenye mtego huu. Watu wanaangamia.Watu wanakuwa masikini.

Nakumbuka siku moja kuna mama mmoja alinipigia simu kumlalamikia mwezi wake ambaye ni mwajiriwa wa Serikali ambaye alikuwa muhanga wa kamali. Mama huyo aliniambia alitamani niongee na mume wake nimshauri maana kila akipata mshahara hakuna anachowaza zaidi ya kwenda kubet. Kuna wakati anarudi nyumbani amemaliza mshahara wote ndani ya siku moja kwa kucheza betting.

Haya ndiyo madhara ya kamali, akili inakuwa imefungwa inawaza ushindi peke yake siyo kushindwa. Agopa sana mtu anayewaza kushinda peke yake anaweza kuweka bondi hadi familia yake kwasababu haamini katika kushindwa. Yeye analiona fungu lililotengwa kwa mshindi ni kama fungu lake linamsubiri. Ni ngumu kubadirisha imani yake.

Hapa ndhani kama taifa kuna ulazima wa kutoa mwongozo na mwelekeo wa vijana na hatma ya nchi yetu. Hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea kwa watu wake kucheza kamali.

Nchi zinaendelea kwa kutengeneza mipango thabiti, usimamizi mzuri wa rasilimali na kuhimiza watu wake kufanya kazi na kulipa kodi.Hakuna njia ya mkato kupata maendeleo.

Serikali itengeneze nyezo rahisi za kupata mitaji kwa vijana na idhibiti tabia kuacha kilipa mikopo yao kwa kuona ni kama ruzuku ya Serikali kwa Vijana. Watu wanatakiwa kujua kuwa ukikopeshwa una wajibu wa kulipa. Biashara ikishamiri vijana watakuwa busy hawatawaza kucheza kamali.

Kamali ni ulevi na ulevi wa kamali unaweza kukufanya uuze mali zako zote moja baada ya nyingine na hivyo kukuacha masikini. Ushindi hauko kwenye matumaini au kuaminishwa kuwa kamali itakutoa kimaisha.

Utajiri una misingi yake. Hakuna mtu aliyeendelea kwa kucheza kamali. Siku zote mali zinazokuja kwa ghafla nazo hutoweka kwa ghafla. Fuatilia washindi wengi wa kamali kama pesa walizoshinda waliweza kufanyia maendeleo. Kwahiyo, ni muhimu kushituka.

Usikubali kulaghaiwa na matangazo mazuri ya kuaminishwa au kuwaona kuna watu wanashinda. Tafuta kazi, tafuta msingi wa mtaji, jua mbinu ya kuwekeza kwenye miradi kwa kuanzia na kidogo ulichonacho. Tengeneza watu wako wa karibu mnaofahamiana tabia na wenye malengo yanayofanana.

Tumia ujuzi ulionao kukuwezesha kupata kianzio cha mtaji. Hakuna aliyezaliwa tajiri bali pesa inatafutwa.
Kazi na fursa ziko nyingi kama utatuliza akili yako vyema. Niliwahi kusema wakati fulani kuwa siyo kila mtu ana jicho la kuona fursa, unaweza kutafuta mtu wa kukushauri cha kufanya na maisha ukafanikiwa.

Vijana wanasema maisha ni timing. Ukishindwa kufanya timing utajikuta unakata tamaa na kujisemea kuwa kwa hapa ulipofika na kwa umri ulionao uwezekano wa kufanikiwa duniani haupo tena badala yake unaumua kumgeukia Mungu ili usifeli kotekote duniani na Mbinguni.

Panga maisha yako vyema, tengeneza mikakati yako vizuri na ratibu mipango yako sawasawa, naamini utafanikiwa. Usiwe mtu wa kujikatia tamaa na kujisemea kuwa umeumbwa wa kukosa.

Mungu ni wakwetu sote. Na Mungu anataka sote tufanikiwe na tuishi duniani kama mahalifa wake na tuweze kumwabudi yeye kwa hushui.

Usisite kumuuliza aliyefanikiwa kafanyaje angalau uweze kupata mbinu. Usijitenge na watu lakini jiweke kando na husuda kwasababu mara nyingi husuda inakufamya umchukie aliyefanikiwa. Mtumie rafiki yako aliyefanikiwa kama ngazi ya kukupandisha juu kwa kuomba na kuifuata mbinu zake zilizomfanya afanikiwe.

Kwa mada hii naomba niishie hapa kwa maana nimezungumza mengi, kama utaendelea kucheza kamali kwa maana ya michezo ya kubahatisha na betting za mipira ni wewe lakini wajibu wangu nimeutimiza kwa taifa langu.
 
Fanya Yako yaliokuleta duniani usijifanye mshauri kwenye mambo yasiyokuhusu kama umepigwa kwenye betting ni wewe wenzio tunakula pesa na tumefanikiwa haujaja na mtu duniani ishi maisha Yako halafu mwisho kabisa acha utapeli naona umeweka namba Ili upige wajinga.
 
Ujumbe umefika. Mwenye akili amesikia. Kazi zipo nyingi ila kama umeona hiyo ndiyo kazi inayokufaa hakuna anayekuzuia endelea kufanya utakuwa milioneo soon.
 
punguza ushauri kaka watu wana mipango yao.
maisha yote ni betting,ni kwa vile tu hupewi odds ndio maana huoni.

hubeti lakini unafungua biashara ya genge mtaani kwako hapo tunakupa odds 2.45 faida ,au 2.65 hasara,draw tunaweka 3.74.
hapo kutoka kwenye biashara hiyo ni 50/50.

Mungu unayemtaja amekataa dhambi nyingi sana,tukiorodhesha hapa utakuta hata kazi unayofanya ni haram.
watu wanafanya kazi kwa matumaini mbali mbali,hata wauguzi na madaktari wanafanya kazi kubwa sana ya kubeti kwenye uhai na ugonjwa ktk maisha ya watu
 
Hana akili huyo
 
Fanya Yako yaliokuleta duniani usijifanye mshauri kwenye mambo yasiyokuhusu kama umepigwa kwenye betting ni wewe wenzio tunakula pesa na tumefanikiwa haujaja na mtu duniani ishi maisha Yako halafu mwisho kabisa acha utapeli naona umeweka namba Ili upige wajinga.
NAKAZIA KWA NGUVU

Mzee baba kama wewe umepigwa huko usidhani ni wote na tusipangiane maisha hukuja na mtu hapa duniani.

Mtoa mada Pumbavu.
 
punguza ushauri kaka watu wana mipango yao.
maisha yote ni betting,ni kwa vile tu hupewi odds ndio maana huoni.

hubeti lakini unafungua biashara ya genge mtaani kwako hapo tunakupa odds 2.45 faida ,au 2.65 hasara,draw tunaweka 3.74.
hapo kutoka kwenye biashara hiyo ni 50/50.

Mungu unayemtaja amekataa dhambi nyingi sana,tukiorodhesha hapa utakuta hata kazi unayofanya ni haram.
watu wanafanya kazi kwa matumaini mbali mbali,hata wauguzi na madaktari wanafanya kazi kubwa sana ya kubeti kwenye uhai na ugonjwa ktk maisha ya watu
Unarahisisha betting ionekana halali kwa mifano batili.
#BettingNiHaram
 
Back
Top Bottom