Ushauri kwa vijana: Kubeti siyo kazi

Mtoa mada mbona umeukimbia uzi wako? Njoo uone majibu ya ulichokileta.

Kazi sio lazima uonekane mtaani unajishuhurisha
Duh!...wakamaria mmemaindi kweli kweli.
 
Uhuni kwako kwakua umepigwa lazima uichukie pole sana nenda kalime hii kazi huiwezi
Sijawahi kubet tokea nizaliwe na sina mpango huo , kheri nile dagaa daily na kuishi kikapuku kuliko kujiingiza kwenye Kazi haramu wazi wazi.
 
naomba odds 6 mkuu
 
Itoshe kusema kuwa Nyie makada wa kijani na njano ni chenga sana
 
Mtoa mada kubeti sio kosa kabisa.
Mimi nina Degree yangu sijapata kazi, nikivyokuwa nasoma nilidhani kuwa nitapata kazi nzuri ila ipo kabatini kazi sina.

Nina tifauti gani na mtu aliyeweka mkeka wa odd 900 akatia elfu 50?

Ukitoki katoboa
Ukikatika atajaribu tena.

Mimi nilimaliza elimu yangu: punter kaweka mkeka ni kitu kile kile.

Anayebeti mkeka ukakatika.

Mimi sijapata kazi/ wote tumekosa.

Ushauri wangu: epuka kushauri watu wanaofanya vitu halali.

Nakushauri pia upite na kipaza sauti ukemee ushoga umeshamiri sana
 
ushauri mzuri kwa jamii,vitu vya kuepuka kwa ustawi wa jamii ni pamoja na
1)kubeti kamari kama ulivyoeleza,watu wanatetea ila wanashinda kamari ni wachache kuliko wanaoliwa ,na mwisho wake ina leta uraibu kadiri siku zonavyoendelea kufikisika,pia ni dhambi kama ulivyosema
2)ulevi pombe kali,madawa ya kulevya ,bangi ,sigara ugoro,gundi,shisha n.k
3)kusubiri /kutegemea ajira rasmi kutoka serikalini/private na wengine kupenda kuwa tegemezi kwa wazazi/walezi na wengine kupenda kulelewa na wapenzi wenye umri mkubwa sugar mumy sugar dady
4)kutojifunza ujuzi mbalimbali ili kupata maarifa mapya ya kufanya ujasiriamali mdogo mdogo
5)kudharau /kuchagua kazi/baadhi ya kazi za ujasiriamali
6)energy drinks
7)kukosa uaminifu
8)kukosa bidii katika kazi nidhamu ya kazi,kupenda anasa,kukosa nidhamu ya pesa
9)kwa wale maafisa usafirishaji kutozingatia matumizi sahihi ya barabarani na sheria za usalama barabarani
10)kuto- kumcha Mungu na kuona tuko bize hatuna muda wa ibada,na kuona dhambi ni kitu cha fahari/ujanja na kuona maisha ya kumcha Mungu ni ushamba.
 
Mimi kama Mkamaria nalaani hii risala kwa niaba ya makamaria wenzangu maarufu kama maafisa ubashiri
 
Tumia nguvu hiyo hiyo kukemea wizi serikalini kwani nayo sio kazi !.....vinginevyo utambue Kila silaha yafaa wakati wa vita.....!!
 
Jaribu kujishugulisha na mambo yanayokuhusu sababu duniani umekuja kivyako hujaja na mtu
 
Mtoa mada mbona umeukimbia uzi wako? Njoo uone majibu ya ulichokileta.

Kazi sio lazima uonekane mtaani unajishuhurisha
Siwezi kukimbia kwa hoja dhaifu zinazotolewa. Taifa linateketea kwa kwa kukithiri kwa michezo ya kamari. Hata mafundisho ya dini yamekataza kamari. Endelea kucheza kwa kuwa kila mtu ashin de mechi zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…