Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Sana tu. Utayari upo, unadhani Polisi wanapambana maandamano yasitoke sababu ni checklist yao? Vyombo vya usalama vinafahamu hasira zilizopo mtaani na wanajua usalama wa viongozi wa CCM utapotea siku wananchi wakipata kiongozi wa kuwaingiza barabarani.
Hawa hawa waTanzania walio busy kujadili umri wa wema na goli la Simba?
 
Ndiyo anataka waunge mkono maandamano badala ya kurudi kwenye maridhiano fake
Lini CHADEMA imepinga maandamano? Yeye aliwakaribisha kwenye mkutano hawakwenda ndio kapanic.
 
Mbowe, Lissu tunawapa pole za kupigwa risasi na kufilisiwa lakini hii struggle siyo ya watu binafsi sababu kuna watu wamekufa kabisa kwa ajili ya mapambano ya kuitoa CCM. Je hao utawambia nini familia zao? Viongozi wa sasa hawana mbinu, ari wala mikakati ya kiuhalisia wakuitoa CCM. Wakina Mwakubusi wanajaribu kuratibu maandamano na civil disobedience na hiyo ndio lugha CCM wanaelewa na kuogopa. Hivi nyie mnawezaje kuwa waastarabu kwa watu wanaoiba kura mchana kweupe huko Zanzibar na mkaamini watabadilika na kuwa waastarabu? Eti unaongelea vyuo vya Uongozi, Diplomacy una akili kweli wewe? Unapambana na mhuni wa Mbagala kwa technique za Oysterbay.
Chadema wako bize na maridhiano ili waonewe huruma wazazwadiwe baadhi ya majimbo na viongozi wawe wabunge. Baaasi!

Mwabukusi kapiga kwenye utosi (kaongea kweli tupu). Upinzani una lengo la kutibu njaa tu kupitia posho za ubunge.
 
Ndio, hao wazanzibar mbona waliandamana wakafa Mamia walipata nini? Wamekuja kupewa serikali ya Umoja wa kitaifa mezani. Same to CHADEMA kama ni maandamano tulifanya sana ila mchakato wa katiba enzi za JK na Sasa zimepatikana mezani wala sio kwa maandamano.

Nimeongelea uwasilishaji mada kwa wananchi, mbona Mbowe au Mbatia au Zitto wapo composed kwanini mpaka uanze matusi weeee hadi kwa wapinzani wenzako waliokutoa gerezani?

Kwa nchi kama Kenya ni kweli ila waTanzania wengi bado wajinga na hawaamini katika nguvu ya umma. Ndio maana kuna mgao ila wanacheka cheka tu na simba na yanga.

Mbinu waliotumia ni ya diplomatic na ndio imeleta mikutano kuruhusiwa, na sheria mbovu za uchaguzi zinaenda futwa, tume huru inaanza na mchakato wa katiba mpya umekuja. Ukipata tume huru na katiba mpya ni step ya kwanza kuitoa ccm sasa unadhani ccm itatoka kwa NEC au maandamano? Zaidi watamtoa Samia watamweka Mpango na watendelea kutawala miaka 60 mingine kama Zimbabwe!!
Wewe ni kama hao wakina Mbowe mmekata tamaa. Ukikata pumzi kaa pembeni wapambanaji wengine waingia ulingoni siyo unatumia vinguvu vilivyobaki kuwakatiza wenzako morali. Kila binadamu anakipaji chake nyie mkishindwa siyo lazima na wao washindwe. Michakato yote mnayofanya sasa haileti matokeo. Watu wanataka CCM iondoke 2025 unaanza kuongelea ruhusa ya kufanya mikutano wakati juzi Mbeya CCM wameiba Kura za Ubunge na tupo October 2023 unadhani chaguzi ndogo za 24 ni mbali au chaguzi kuu 25. Mwakubusi amewambia ukweli muda wenu umefika pumzikeni.
 
Chadema wako bize na maridhiano ili waonewe huruma wazazwadiwe baadhi ya majimbo na viongozi wawe wabunge. Baaasi!

Mwabukusi kapiga kwenye utosi (kaongea kweli tupu). Upinzani una lengo la kutibu njaa tu kupitia posho za ubunge.
Sasa si aanzishe chama chake ili kiwe anavyotaka? Zitto na Kitila walianzisha chama Chao walipoona Mbowe hafai!

Yeye anatukana wenzie wakati aligombea ubunge 2020 licha ya kujua hakuna tume huru
 
Chadema wako bize na maridhiano ili waonewe huruma wazazwadiwe baadhi ya majimbo na viongozi wawe wabunge. Baaasi!

Mwabukusi kapiga kwenye utosi (kaongea kweli tupu). Upinzani una lengo la kutibu njaa tu kupitia posho za ubunge.
Uzuri wa ukweli ni ngumu kuupinga. Ni sababu wanapata taabu kujibu.
 
Msijazane upepo, kuna tofauti ya ukweli na UJINGA. Mtu kma unaona vyama vyote ni feki si uanzishe chako? Au kama unaona wenzio hawaku support si usonge mbele alone why mpaka utukane watu ambao hawako liable kwako?

Ni sawa na umemchoka ndugu yako kukaa hapo kwako si unaweza mtoa kwa gia ya kumtafutia kazi au biashara kwani lazima mpka umuite umwambie NIMEKUCHOKA??

TCD anzisheni chuo shida ni kubwa zaidi ya nilivyodhani
Wapinzani wanastahili kutukwanwa. Kwasbb wamekuwa wakichosha masikio ya watanzania kuwa wanadai katiba mpya na tume huru.

Ccm imekuwa ikiwachezesha danadana wapinzani kama watoto wadogo. Lkn cha ajabu wapinzani wamebakia kubwabwaja tu kwenye press.

Hivi Sasa ndiyo wameamua kuwapigia magoti ccm wanaomba tume huru na katiba mpya kwa kutumia kikosi kazi na wengine wanaomba waachiwe majimbo kupitia maridhiano.

Mwabukusi yuko sawa kabisa. Mm niko na Mwabukusi, hawa wapinzani ni waganga njaa
 
Unajua Tanzania haipo mjini tu. Ni watu wachache sana wanafanya hivyo kati watu ya 60m.
Nimepita mitaani asubuhi 90% ya vijana wana discuss simba na yanga kufuzu makundi. Hayo wanajadili huku hawana umeme?? Hao ndio wanaelewa kweli hata umuhimu wa bandari?
 
wengine wanaomba waachiwe majimbo kupitia maridhiano.
Waombe ubunge? If that was the case kwanini Chadema ilikataa tume huru ila wanadai katiba mpya? Means wanachotaka sio kushinda chaguzi ila mabadiliko ya mfumo wa utawala wa nchi hii.
 
Mwabukusi kaitisha maandamano ya watanzania, ila analaumu vyama vya upinzani! Je hayo maandamano yake yanategemea backup ya vyama vya upinzani tu? Haoni ni hatari hoja binafsi kubebwa na chama? Afahamu kuwa vyama vinafanya maamuzi kupitia vikao, na sio kuburuzwa na hoja za mtu binafsi. Yeye aendelee na hamasa za hayo maandamano yake, watanzania wasioogopa watajiunga naye.
 
Wapinzani wanastahili kutukwanwa. Kwasbb wamekuwa wakichosha masikio ya watanzania kuwa wanadai katiba mpya na tume huru.
Maridhiano unayokejeli hapa ndio yamezaa mchakato wa katiba, mikutano ya siasa, na tume huru.
 
Back
Top Bottom