Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Sasa si aanzishe chama chake ili kiwe anavyotaka? Zitto na Kitila walianzisha chama Chao walipoona Mbowe hafai!

Yeye anatukana wenzie wakati aligombea ubunge 2020 licha ya kujua hakuna tume huru
Kwa mazingira ya sasa Mwabukusi anaweza kusajiri chama kikakubalika?? Kama nia ya wapinzani ilikuwa ni dhahiri na ya dhati ya kudai katiba mpya kwann wasiunge mkono mbinupya ya Mwabukusi? Badala yake wanaendelea kukomaa na mbinu mfu zile zile.

Kila mtu anajua na anaona kwamba CCM hawataki kuandika katiba mpya. Lkn wapinzani kimya tu. Eti wanafanya maridhiano. Maridhiano KONYO.
 
Salaam wana jukwaa, nimekutana na interview ya Wakili Mwabukusi na Maria Sarungi probably kutoka Maria spaces/clubhouse. Cha kushangaza Wakili msomi alikua busy kushambulia wapinzani kuwa ni wawaza ubunge, wapenda vyeo n.k. Hivi kweli hajui struggle za lissu hadi kumwagiwa risasi, hajui mbowe alivyofilisiwa na kufungwa kisa kudai katiba mpya na democracia nchi hii?

Pia kalaumu wapinzani kutosupport maandamano yake akiwaita waoga? Hivi siasa za maandamano wapinzani hawajui? Amesahau maandamano ya Arusha 2011 hadi watu wakauwawa? Amesahau maandamano ya pale Kinondoni hadi kina Mbowe wakahukumiwa kifungo na faini ya 300 Million? Yeye Leo ndio anajifanya ni pro-protest kuliko kina Hajji Duni au lissu?

Sio hivyo tu kaongelea suala la wake za viongozi kulipwa posho!! Yes ni kitu cha ajabu lakini Mwabukusi amekiadress kana kwamba tunalipia tendo la ndoa la viongozi yaani "we are paying for that thing.... we are paying for sex". As if wake za viongozi ni vyombo vya ngono tu. Kauli za namna hii ni unnecessary maana badala ya hoja kuwa bandari utaanza kujibu makelele ya feminists na UWT!!

Ushauri naoweza kumpa Mwabukusi ni kwamba atafute PR manager ajue namna ya kujenga mahusiano na umma. Ana hoja nzuri ya Bandari pamoja na katiba mpya ila lazima ajifunze kuwa na shabaha moja kwa wakati. Ni hatari sana kupambana na CCM, CHADEMA na wanawake kwa wakati mmoja utaondoka kwenye limelight in no time....

Kingine kuna haja ya vyama kama CHADEMA au ACT kupitia TCD kuanzisha chuo cha uongozi, diplomacy na political science ili wanasiasa/wanaharakati wote vijana wapitie huko kabla ya kupewa teuzi/uongozi hasa kwenye vyombo vya uwakilishi au kuongoza taasisi/jumuiya ya vyama.

Hili litasaidia kuondoa mihemko, kuleta utulivu wa akili kwenye mijadala, na kuwa na mawasiliano mazuri na jamii. Sasa mtu kawa maarufu juzi tu kaanza kumshambulia Mbowe out of nowhere! haya mambo hayapendezi especially tuliopo opposition maana tukikwaa madaraka si yatajirudia ya sabaya na Makonda!

View: https://youtu.be/78Gi9mXZWwA?si=YMXW0PFJ-jpAesu9

Sisi wengine tulisema zamani tunangoja tarehe ya maandamano na mahala yatapoanzia; lkn nikatanabahisha kwamba hayatofanywa kwa sababu Watu ni waoga. Mwabukusi atalalamika sana kwani mwenyewe hajui anachotakiwa kukifanya na ukimshauri anaona anajua sana. Akishindwa anaweza kuamua ama kurudia udereva wa daladala au kuendelea na uwakili kwani kazi hizi anazimudu vyema na sio SIASA.
 
Mwabukusi kaitisha maandamano ya watanzania, ila analaumu vyama vya upinzani! Je hayo maandamano yake yanategemea backup ya vyama vya upinzani tu? Haoni ni hatari hoja binafsi kubebwa na chama? Afahamu kuwa vyama vinafanya maamuzi kupitia vikao, na sio kuburuzwa na hoja za mtu binafsi. Yeye aendelee na hamasa za hayo maandamano yake, watanzania wasioogopa watajiunga naye.
Upo sahihi asilazimishe wote wawaze kama yeye
 
Waombe ubunge? If that was the case kwanini Chadema ilikataa tume huru ila wanadai katiba mpya? Means wanachotaka sio kushinda chaguzi ila mabadiliko ya mfumo wa utawala wa nchi hii.
Lisu alisema anasikiasikia maridhiano haya yana ajenda ya kuiachia chadema majimbo 25. Au hukumsikia??

Kwann Mbowe hataki kujiondoa kwenye ujinga huu??
 
Mwabukusi na genge lake la Bandari super stars wafungue Chama cha Siasa, na kama wanataka mipasho wafungue Bandari Modern Taarab.
 
Maridhiano unayokejeli hapa ndio yamezaa mchakato wa katiba, mikutano ya siasa, na tume huru.
Tutakuwa tunakosea sana kama tutaanza kuwasujudia ccm kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kitu ambacho walikizuia kinyume kabisa na katiba. Hapa ndipo ccm wanaona upinzani hauna meno na hauna cha kuwafanya. Na ndiyo sababu wanafanya watakavyo. Hili la kuzuia mikutano lilipaswa lipingwe kwa jasho na damu.

Kuhusu mchakato wa katiba mpya na tume huru ndugu yangu hii kitu haitakaa ifanyike. Umemsikia Samia anataka elimu ya Katiba itolewe kwa miaka 3. Maana yake ni kwamba hataki .
 
Wangekua serious wangeshaandamana kupinga mgao wakati tuna gesi ya kutosha.
Mbona hueleweki wakina Mwabukusi unawakejeli kwa kuandaa maandamano halafu mtu huyo huyo unawesema vijana hawapo serious kufanya maandamano.
 
Sana tu. Utayari upo, unadhani Polisi wanapambana maandamano yasitoke sababu ni checklist yao? Vyombo vya usalama vinafahamu hasira zilizopo mtaani na wanajua usalama wa viongozi wa CCM utapotea siku wananchi wakipata kiongozi wa kuwaingiza barabarani.
Na vyombo hivyo vya usalama vina take advantage ya woga wa watanzania especially vijana wengi ambao hawapo tayari kwa mapambano ni waoga sana kiasi cha kujiingiza kwenye uchawa kama fichio la huo woga wao.

Uhakika uliyopo ni kupigana vita hiyo na maamdamano hayo nyuma ya viboard vyetu humu jf na mitandao mingine.
 
Lisu alisema anasikiasikia maridhiano haya yana ajenda ya kuiachia chadema majimbo 25. Au hukumsikia
Hiyo ilikua proposal ya ccm kama goodwill ya kufidia makosa ya 2020 hata zenji kuna mbunge wa CCM alijiuzuru na kuwaachia kiti ACT lakini sio kwamba ndio walichotaka Chadema.
Kwann Mbowe hataki kujiondoa kwenye ujinga huu??
Mbowe alishajiondoa tokea June 31 mbona kasema kwenye hotuba ya jana!
 
na hicho ndicho kilichomfanya Mwabukusu kuondoka chadema akaenda NCCR mageuzi. huyo alikuwa CHADEMA kindakindani huyo zamani.
 
Mbowe alishajiondoa tokea June 31 mbona kasema kwenye hotuba ya jana
Sasa kama kajiondoa the way forward ilikuwa ni kuunga juhudi za Mwambukusi. Maana uchaguzi umekaribia lkn chadema yaonekana kama imekata upepo. Ndiyo maana Mwabukusi anawashangaa!
 
Kuhusu mchakato wa katiba mpya na tume huru ndugu yangu hii kitu haitakaa ifanyike. Umemsikia Samia anataka elimu ya Katiba itolewe kwa miaka 3. Maana yake ni kwamba hataki .
Anataka sana tu sema anajua amechokwa so hata akishindanishwa na upepo, chini ya tume huru ataangushwa 2025; ila hana shida kukabidhi madaraka kwa upinzani 2030.
 
Mikakati ya chadema ni butu. Huwezi kuwa unampigia magoti mtesi wako. Haipo hiyo. Akisha kuona boya hutashi da. Dawa ya mbabe ni ubabe
Sio kwamba Dunia haioni huu ubabe wa CCM
 
Salaam wana jukwaa, nimekutana na interview ya Wakili Mwabukusi na Maria Sarungi probably kutoka Maria spaces/clubhouse. Cha kushangaza Wakili msomi alikua busy kushambulia wapinzani kuwa ni wawaza ubunge, wapenda vyeo n.k. Hivi kweli hajui struggle za lissu hadi kumwagiwa risasi, hajui mbowe alivyofilisiwa na kufungwa kisa kudai katiba mpya na democracia nchi hii?

Pia kalaumu wapinzani kutosupport maandamano yake akiwaita waoga? Hivi siasa za maandamano wapinzani hawajui? Amesahau maandamano ya Arusha 2011 hadi watu wakauwawa? Amesahau maandamano ya pale Kinondoni hadi kina Mbowe wakahukumiwa kifungo na faini ya 300 Million? Yeye Leo ndio anajifanya ni pro-protest kuliko kina Hajji Duni au lissu?

Sio hivyo tu kaongelea suala la wake za viongozi kulipwa posho!! Yes ni kitu cha ajabu lakini Mwabukusi amekiadress kana kwamba tunalipia tendo la ndoa la viongozi yaani "we are paying for that thing.... we are paying for sex". As if wake za viongozi ni vyombo vya ngono tu. Kauli za namna hii ni unnecessary maana badala ya hoja kuwa bandari utaanza kujibu makelele ya feminists na UWT!!

Ushauri naoweza kumpa Mwabukusi ni kwamba atafute PR manager ajue namna ya kujenga mahusiano na umma. Ana hoja nzuri ya Bandari pamoja na katiba mpya ila lazima ajifunze kuwa na shabaha moja kwa wakati. Ni hatari sana kupambana na CCM, CHADEMA na wanawake kwa wakati mmoja utaondoka kwenye limelight in no time....

Kingine kuna haja ya vyama kama CHADEMA au ACT kupitia TCD kuanzisha chuo cha uongozi, diplomacy na political science ili wanasiasa/wanaharakati wote vijana wapitie huko kabla ya kupewa teuzi/uongozi hasa kwenye vyombo vya uwakilishi au kuongoza taasisi/jumuiya ya vyama.

Hili litasaidia kuondoa mihemko, kuleta utulivu wa akili kwenye mijadala, na kuwa na mawasiliano mazuri na jamii. Sasa mtu kawa maarufu juzi tu kaanza kumshambulia Mbowe out of nowhere! haya mambo hayapendezi especially tuliopo opposition maana tukikwaa madaraka si yatajirudia ya sabaya na Makonda!

View: https://youtu.be/78Gi9mXZWwA?si=YMXW0PFJ-jpAesu9

CCM na vibaraka zenu mmeshikwa pabaya. Anayosema Mwabukusi yuko sahihi.

Mnukuu Mwabukusi kwenye context.

Tofauti gani ya anachosema Lissu, anasema Mwabukusi hapa ?

Usimsemee Mwabukusi wacha watu wamsikilize wenyewe.

Alipo Mwabukusi tupo!
 
Back
Top Bottom