Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Imekata upepo? Duuh hii mikutano yenye hamasa kubwa huioni?
Chadema haijawahi kufeli ktk ku-mobikize watu ili kupata support. Chadema kama kungekuwa na tume huru siku nyingi ingekuwa ishachukua dola.

Ninaposema imekata moto ni kwenye issue ya kuishinikiza ccm ikubali kuandika katiba mpya ili hiyo support ya wananchi iwe na tija kwenye chaguzi.
 
Kipi tofauti? Video si iko hapo

Vyote ulivyoandika ni tofauti audio Iko hapo sikiliza kujiridhisha.

Kimsingi anachosema Mwabukusi hapa ndicho hicho hicho anachosema Lissu.

Nia Yako ilikuwa tukusome wewe tusimsikilize Mwabukusi siyo? Hapo umekwama. Mtawadanganya mamburula peke yao.

Ndiyo maana polisi wameanza mazoezi siyo?

Maandamano yako pale pale.
 
Hapana hamjafanya chochote sijawahi kuona maandamano ya Chadema ya kusimamisha Nchi wala Sijawahi kuona wananchi wakifanya civil disobedience kwa ajili ya Chadema. Hata hivyo haijalishi hamtabadilika.
Mwananchi wa Tanzania yuko radhi aandamane kwenye Yanga na Simba ngoja tuone Maandamano ya Slaa na Mwabukusi kila la heri
 
Mwananchi wa Tanzania yuko radhi aandamane kwenye Yanga na Simba ngoja tuone Maandamano ya Slaa na Mwabukusi kila la heri

Kwa hiyo mkuu wewe utakuwa
pembeni ukingoja kuona kama wanavyofanya wale wenye kuandamania yanga na simba?
 
Hii ya Mwabukusi inatofauti kidogo. Maana inahusisha wadau wengi, asasi za kiraia, vyama vya siasa na makundi mbali mbali ya kijamii.
Hivyo itakuwa na kishindo kikubwa.

Chadema ilishindikana kwasabb ilikuwa ni issue ya chama kimoja tu cha siasa.
Labda azihusishe na Yanga na Simba vinginevyo....Well ngoja tuone.
 
Na Mwabukusi analifahamu Hilo ndiyo maana anawashangaa chadema. Alitarajiwa chadema ingedandia hoja na kuisukuma ipasavyo
Mbona wamedandia kupitia oparesheni 255 okoa bandari zetu..... yeye alitaka chadema impigie magoti na ijipendekeze kwake au impe cheo?

Ni hivi taasisi haiwezi mfuata mtu ila mtu hufuata taasisi.... kwamba chadema haina wanasiasa au mawakili wasomi calibre ya Mwabukusi hadi wamuone almasi.

Acha aendelee mwenyewe aone ilivyo ngumu.
 
Tarime ilifanyika sana hii..... Arusha ilikua maandamano kila wiki.... juzi tu Akwilina aliuwawa maandamano ya chadema so hii imefanyika sana hili. Sema kwa aina hii ya wananchi sio rahisi kupata turn out kubwa
Narudia Nchi haijawahi kusimama. Wananchi waliona madhaifu ya viongozi wenu wakati wa Magufuli. Vyama vinavyotaka kujijenga kama taasisi vingebadili viongozi na kuweka radicals na hardliners ilikuamsha Ari za wananchi.
 
Kwa hiyo mkuu wewe utakuwa
pembeni ukingoja kuona kama wanavyofanya wale wenye kuandamania yanga na simba?
Mimi kama Mwanachama wa CHADEMA nitasikiliza viongozi wangu wa Chama na msimamo wa Chama bado na hapo hapo ninaweza kutoa ushauri wangu kuwa tusiwe Chama cha Matukio tujikite kwenye Manifesto yetu.
 
Mwananchi wa Tanzania yuko radhi aandamane kwenye Yanga na Simba ngoja tuone Maandamano ya Slaa na Mwabukusi kila la heri
Narudia hata wakiandamana watu kumi ni mafanikio. Nyie endeleni na kajeli na maridhiano.
 
vingebadili viongozi na kuweka radicals na hardliners ilikuamsha Ari za wananchi.
Politics sio pressure group au activism ni leadership. Sasa unapotaka uongozi kuna ushawishi mpana kwa makundi yote wakiwemo ccm, wasio na vyama n.k ila radicalism ni kuamini yeyote asiye na wewe ni adui.

Siasa haziendi hivyo
 
Sisi CHADEMA tuendelee strategy yetu ya kuongea na Mabalozi wa Nchi za Magharibi ambao ni Donors na Patners wa hii Serikali ili wakate misaada kwa Serikali ya CCM hiyo pressures ndio Watawala wanazielewa.
 
Mimi kama Mwanachama wa CHADEMA nitasikiliza viongozi wangu wa Chama na msimamo wa Chama bado na hapo hapo ninaweza kutoa ushauri wangu kuwa tusiwe Chama cha Matukio tujikite kwenye Manifesto yetu.
Una document yenye sera za Chadema unaweza uka share? Kama una link unaweza ukatuma pia.
 
Ainisha kimoja tu usizunguke

Si kimoja ndugu:

1. Hakuna popote alipowalaumu vyama vya upinzani kutounga mkono Maandamano waliyoitisha.

Lissu kupigwa risasi, Mbowe kufilisiwa ni maneno yako kutia chumvi kwenye lisilokuwapo kwenye maneno yake.

2. Hakuna mahali popote alipowaita wapinzani ni waoga. Zaidi ya kuwa Yuko wazi watanzania si waoga tena kwa mifano.

Ya watu kufa Arusha na kinondoni ni ya kwako kutia chumvi na nje ya context.

3. La kulipa malipo viongozi wa wenza kaliongelea vizuri sana kuonyesha kulikoni kulipa wenza wa viongozi huku ukiondoa Ile bima pendwa kwa watoto.

Hoja ya Mwabukusi kuwahusu wenza na malipo yao ni hoja yetu watanzania.

Mengine ni mawazo yako ya ki CCM. Hayo Kaa nayo yanatuhusu nini sisi?

Usituambie wewe alichosema Mwabukusi. Hicho kimo kwenye audio.

Maelezo yako kupotosha utawapata mbuzi wenzako tu ndugu.
 
Politics sio pressure group au activism ni leadership. Sasa unapotaka uongozi kuna ushawishi mpana kwa makundi yote wakiwemo ccm, wasio na vyama n.k ila radicalism ni kuamini yeyote asiye na wewe ni adui.

Siasa haziendi hivyo
Hiyo ni siasa safi. Bahati mbaya CCM ni radicals wataua, watafunga na kuwapa watu vilema iliwabaki madarakani. Jibu pekee kwa watu kama hao ni kuwapeleka radicals halafu akili zikikaa sawa na wakakubali kuacha madaraka tunakuwa waastarabu.
 
Back
Top Bottom