Ushauri kwa Wakili Mwabukusi kuelekea maandamano ya kitaifa

Hawa hawa waTanzania walio busy kujadili umri wa wema na goli la Simba?
 
Ndiyo anataka waunge mkono maandamano badala ya kurudi kwenye maridhiano fake
Lini CHADEMA imepinga maandamano? Yeye aliwakaribisha kwenye mkutano hawakwenda ndio kapanic.
 
Chadema wako bize na maridhiano ili waonewe huruma wazazwadiwe baadhi ya majimbo na viongozi wawe wabunge. Baaasi!

Mwabukusi kapiga kwenye utosi (kaongea kweli tupu). Upinzani una lengo la kutibu njaa tu kupitia posho za ubunge.
 
Wewe ni kama hao wakina Mbowe mmekata tamaa. Ukikata pumzi kaa pembeni wapambanaji wengine waingia ulingoni siyo unatumia vinguvu vilivyobaki kuwakatiza wenzako morali. Kila binadamu anakipaji chake nyie mkishindwa siyo lazima na wao washindwe. Michakato yote mnayofanya sasa haileti matokeo. Watu wanataka CCM iondoke 2025 unaanza kuongelea ruhusa ya kufanya mikutano wakati juzi Mbeya CCM wameiba Kura za Ubunge na tupo October 2023 unadhani chaguzi ndogo za 24 ni mbali au chaguzi kuu 25. Mwakubusi amewambia ukweli muda wenu umefika pumzikeni.
 
Chadema wako bize na maridhiano ili waonewe huruma wazazwadiwe baadhi ya majimbo na viongozi wawe wabunge. Baaasi!

Mwabukusi kapiga kwenye utosi (kaongea kweli tupu). Upinzani una lengo la kutibu njaa tu kupitia posho za ubunge.
Sasa si aanzishe chama chake ili kiwe anavyotaka? Zitto na Kitila walianzisha chama Chao walipoona Mbowe hafai!

Yeye anatukana wenzie wakati aligombea ubunge 2020 licha ya kujua hakuna tume huru
 
Chadema wako bize na maridhiano ili waonewe huruma wazazwadiwe baadhi ya majimbo na viongozi wawe wabunge. Baaasi!

Mwabukusi kapiga kwenye utosi (kaongea kweli tupu). Upinzani una lengo la kutibu njaa tu kupitia posho za ubunge.
Uzuri wa ukweli ni ngumu kuupinga. Ni sababu wanapata taabu kujibu.
 
Wapinzani wanastahili kutukwanwa. Kwasbb wamekuwa wakichosha masikio ya watanzania kuwa wanadai katiba mpya na tume huru.

Ccm imekuwa ikiwachezesha danadana wapinzani kama watoto wadogo. Lkn cha ajabu wapinzani wamebakia kubwabwaja tu kwenye press.

Hivi Sasa ndiyo wameamua kuwapigia magoti ccm wanaomba tume huru na katiba mpya kwa kutumia kikosi kazi na wengine wanaomba waachiwe majimbo kupitia maridhiano.

Mwabukusi yuko sawa kabisa. Mm niko na Mwabukusi, hawa wapinzani ni waganga njaa
 
Unajua Tanzania haipo mjini tu. Ni watu wachache sana wanafanya hivyo kati watu ya 60m.
Nimepita mitaani asubuhi 90% ya vijana wana discuss simba na yanga kufuzu makundi. Hayo wanajadili huku hawana umeme?? Hao ndio wanaelewa kweli hata umuhimu wa bandari?
 
wengine wanaomba waachiwe majimbo kupitia maridhiano.
Waombe ubunge? If that was the case kwanini Chadema ilikataa tume huru ila wanadai katiba mpya? Means wanachotaka sio kushinda chaguzi ila mabadiliko ya mfumo wa utawala wa nchi hii.
 
Mwabukusi kaitisha maandamano ya watanzania, ila analaumu vyama vya upinzani! Je hayo maandamano yake yanategemea backup ya vyama vya upinzani tu? Haoni ni hatari hoja binafsi kubebwa na chama? Afahamu kuwa vyama vinafanya maamuzi kupitia vikao, na sio kuburuzwa na hoja za mtu binafsi. Yeye aendelee na hamasa za hayo maandamano yake, watanzania wasioogopa watajiunga naye.
 
Wapinzani wanastahili kutukwanwa. Kwasbb wamekuwa wakichosha masikio ya watanzania kuwa wanadai katiba mpya na tume huru.
Maridhiano unayokejeli hapa ndio yamezaa mchakato wa katiba, mikutano ya siasa, na tume huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…