Ushauri kwa Waziri Mkuu: Aliechangisha milioni 37 za maafa asidhuriwe na sheria serikali imuajiri kwenye kamati ya maafa ana uwezo wa kuhamasisha

Alafu ukute alikusanya 1m tu ye akaongeza sifuri aonekane ana ushawishi mkubwa,
Ngoja tuone kati yake na mh.nani ana strong army!
Ila akivuka hili mshaurini aache kimbelembele anguko lake litakua kubwa huko mbeleni mana anajaa kwenye mifumo ya watu!
He's just a hustler.
 

Wazo lako ni zuri sana;
1. Kazi kubwa ya Tanzania ni kuua vipaji na kuvunja moyo

2. Tanzania ukiwa bora unapigwa mazengwe hadi ufe moyo...ukamuuliza; Tido Muhando na Muhongo
 
Nguvu ya kufuatilia wachangishaji ni kubwa kuliko nguvu ya kumtafuta mwenye jengo.....ila yoye kwa yote serikali nayo iitoe update kama Niffer
Sasa mkuu, records za mwenye jengo ni kitendo cha kunyanyua simu kupiga pale wizara ya ardhi, au?

Hivyo afanya Chalamila, IGP au mkuu wa polisi wa wilaya.

Pengine tayari wamepata taarifa who knows?
 
Alichokifanya Nifa, nikuudanganha Umma ,wamwamini, akishaaminika, Kila MTU atataka asibaki nyuma, na hapo ndipo kulipo na kilio Cha kusaga meno.


Naaaa kama kweli kafikisha 37M, Yule Nabii mgawa magari kahusika, na hapa ndipo tunaposema, Utajiri wa mwanamke uko katikati ya mapaja yake.
 
Kwani kku

Kwani Kuna aliyeenda kumshtaki Kwa kudhulumiwa. Aliyedhulumu uhai wa watanzani amechukuliwa hatua gani
 
Mkuu followers wa insta wana mambo hiyo milioni 37 ni sawa na shilingi 1500 kwa followers elf 25! Nimeona kachapicha statement ni msururu wa miamala ya buku buku mbili!

Kumbuka wana mamilioni ya followers
 
Tabu wanaochangia wanamuamini yeye Niffer na sio serikalini, hivyo wafungue labda akaunti atakayo jisimamie yeye waone pesa yao ikitumiwa vizuri.

Hivi mfuko huo wametoa updates au kimya kama kawa? Ila lazima wapige tu 😀
 
Yawezekana kabisa usemayo lakini kwa jicho la tatu Nifa ana potential kwa maana kwamba ana nguvu ya kuhamashisha.

Na uwezo wa kuwafanya watu washawishike kufanya jambo fulani kama kununua kitu fulani, kwasababu ya nafasi yake redioni na mitandaoni na uhusiano wake na hadhira.

Hivyo hata kama atakuwa amekosea lakini bado fact yabaki kuwa amekusanya (kama sijakosea) zaidi ya kamati ya maafa.

Kuna "huge difference" kati yake na wao.
 
Basi na Wenye case za kuua mahakamani wasamehewe waajiriwe jeshini waende Congo kuua m23
Kesi za mauaji ni habari ingine.

Huu ni wizi wa mitandaoni ambao umehama kutoka kwenye wizi wa kalamu.
 
Mkuu followers wa insta wana mambo hiyo milioni 37 ni sawa na shilingi 1500 kwa followers elf 25! Nimeona kachapicha statement ni msururu wa miamala ya buku buku mbili!

Kumbuka wana mamilioni ya followers
Alisema watu walifika kama sijakosea zaidi ya laki 1, na hata 500tshs na 1,000tshs zilikuwemo yeye kunoti alisema akishukuru kuaminiwa. Hata kesho ataweza tu, hard working girl.
 
Alafu ukute alikusanya 1m tu ye akaongeza sifuri aonekane ana ushawishi mkubwa,
Ngoja tuone kati yake na mh.nani ana strong army!
Ila akivuka hili mshaurini aache kimbelembele anguko lake litakua kubwa huko mbeleni mana anajaa kwenye mifumo ya watu!
Hivi Million 37 hahahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…