Ushauri kwa Waziri Mkuu: Aliechangisha milioni 37 za maafa asidhuriwe na sheria serikali imuajiri kwenye kamati ya maafa ana uwezo wa kuhamasisha

Ni kweli kwani tanzapol ni mwanachama.
Mwanachama toka zamani sana. Au amejitoa uanachama lini?
IGP mstaafu Said Mwema alikuwa huko kabla hajateuliwa kuwa IGP alitokea Interpol.
Kuna tajiri mmoja hawa maarufu kwenye band za Muziki kama Papaa fulani alikimbia kesi akakamatiwa Dubai kwa ushirikiano wa Interpol.
 
Waliompa michango huyu mdada michango ya maafa ni dalili ya kwamba serikali haiaminiki
Kwa sababu wanakumbuka madudu yaliyotokea kwenye tetemeko la bukoba mf. Akaunti feki
 
Nchi inaendeshwa kwa mihemko ya mitandao.
Premier kapita pages za udaku za insta kaona kuna battle dhidi ya wachangishaji na waliokosa fursa ya kuchangisha ili wajinufaishe basi na yeye kapita na upepo huo huo.

Lenye tija zaidi ni mmiliki wa jengo ila mpaka leo siku ya 4 hakuna hata fununu ya kuwa ni nani, yuko wapi na anawajibishwa vipi.

Sitostaajabu mmiliki wa jengo ikiwa ni mkubwa na mwenye madaraka. Wanalindana wenyewe kwa wenyewe.
Ingekuwa ni mkinga au mchaga asie na wadhifa saa hizi picha zake zingeshasambaa mitandaoni kote.
 
Hi ivi unajua mfuko wa maafa una shilingi ngapi mzee baba?? Kwamba nifa achangishe kuliko serikali.ha ha ha watu mnapenda kujichekesha wenyewe
 
Wakuu , Tukubaliane kukusanya pesa kwa kutumia majangabya kitaifa sio sawa. Tukiwacha hili wataibuka matapeli na kujipatia fedha kwa njia hii
 
Jeni ni muongo ukute kakusanya laki 5 tu 😂

Bongo ina mambo yake. Inawezekana ikawa Waziri Mkuu amesikia tu story za mtaani then anatoa amri ili aonekane anachapa kazi. Hii ni kawaida sana kwa Mjaliwa. Tumemuona anavyokwenda kuko mikoani na Wilayani anasoma data za upigaji .... Mwisho wa siku hatuoni mafanikio yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…