Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanachama toka zamani sana. Au amejitoa uanachama lini?Ni kweli kwani tanzapol ni mwanachama.
Waliompa michango huyu mdada michango ya maafa ni dalili ya kwamba serikali haiaminikiLeo Waziri mkuu katembelea eneo ambalo ajali imetokea huko Kariakoo na baadae akateta na wananchi na viongozi mbalimbali wa mkoa na serikali akiwemo waziri alie chini yake William Lukuvi.
Lakini ukweli wabakia kuwa ni uleule kwamba bado wapo watu wamekwama huko chini ya kifusi na hatima yao ya maisha haijulikani wataweza vipi kujiokoa au kuokolewa.
Serikali kupitia kamati ya maafa imezembea na ni wazi wale wote wanohusika huu ni wakati wa kuketi kikao cha kutathmini uzembe ulotokea na kisha kujipanga upya kwani tayari maji yamemwagika.
Sasa katika maongezi yake mheshimiwa waziri mkuu kaagiza kuwa mtu ambae anatuhumiwa kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa ajali hiyo ni lazima akamatwe na ahojiwe kwanini amefanya shughuli iso yake na mamlaka hayo ni nani amempatia.
Yasemekana mtu huyo kwa juhudi zake binafsi ameweza kuchangisha kiasi cha shilingi za kitanzania au fedha za madafu milioni 37! ambazo ametumiwa kupitia muamala ya simu yake yaani watu walikuwa wakidondosha humo kila alie nacho.
Mimi namshauri waziri mkuu amsamehe mtu huyo ila apewe onyo kali na polisi kwamba asirudie kitendo hicho. Ni wazi kuwa umaskini na kukosa ajira ndo moja ya sababu kuwa ilompelekea mtu huyo kuja na wazo la kiakili kuweza kukusanya shilingi milioni 37 ndani ya masaa 48 ukizingatia kuwa wale waathirika ambao wameokolewa huenda hadi leo hawakuwa wameonwa na kamati ya maafa.
Pili, litakuwa ni jambo la busara kubwa endapo mtu huyo ataajiriwa na kamati ya maafa ili nae achangie mawazo yake na awe huru zaidi kuweza kuonyesha mbinu na njia kadhaa za kuchangisha fedha kwa uharaka na ufanisi mkubwa kwani yasemwa kuwa ametumia moja ya mitandao ya simu na ameingiza fedha hizo kwa uharaka mkubwa hiyo ni wazi kuwa mtu huyu ana maarifa (skills).
Tatu, kwa kuwa mtu huyo ameingiza fedha hizo basi si mbaya kama serikali itamfikiria kumlipa posho kiasicha kuweza kujitayarisha endapo kamati ya maafa itamujiri rasmi.
Mwisho, hali ya maisha ya watanzania wa hali ya chini ni ngumu na linapojitokeza tatizo kama hilo kubwa wengi wa wale waso na ajira hujikuta wakipatwa na majaribu ya shetwani kiasi cha kuacha kuokoa watanzania wenzao ambao wamekumbwa na madhoruba na kuanza kufanya uporaji yaani "looting" yote hiyo ni umaskini na kukosa kipato cha uhakika.
Ni juzi tu tumeona jinsi watanzania walivyochoka na maisha kiasi cha kuwaangalia tu wale watanzania wenzetu wakijaribu kumteka raia wa kawaida bwana Bonge ili waende kumdhuru.
Natarajia waziri mkuu atapata muda wa kunywa gahawa huku akiperuzi JF na akiona mada hii basi tafadhali azingatie ombi hili.
Ni mie mdau wa fikra mpya kwa watanzania.
Yule nwye anajichetua...amesahau ana biashsara..serikali sio ya kutunishia msuliAmesema ana strong army...
Nendeni taratibu nae..
Hi ivi unajua mfuko wa maafa una shilingi ngapi mzee baba?? Kwamba nifa achangishe kuliko serikali.ha ha ha watu mnapenda kujichekesha wenyeweYawezekana kabisa usemayo lakini kwa jicho la tatu Nifa ana potential kwa maana kwamba ana nguvu ya kuhamashisha.
Na uwezo wa kuwafanya watu washawishike kufanya jambo fulani kama kununua kitu fulani, kwasababu ya nafasi yake redioni na mitandaoni na uhusiano wake na hadhira.
Hivyo hata kama atakuwa amekosea lakini bado fact yabaki kuwa amekusanya (kama sijakosea) zaidi ya kamati ya maafa.
Kuna "huge difference" kati yake na wao.
Yule ujuaji utamponzsduh...kweli kabisa?mshauri! au ulimaanisha mhamasishaji? ila pipo wako na confidence sana nwdayz is it true she reply 2 PM that she has strong army? hii kama ni uhuru ss umepitiliza
🤣Siye twamchora tuYule nwye anajichetua...amesahau ana biashsara..serikali sio ya kutunishia msuli
hapana sidhani kama ni ujuaji ni overconfidence,hilo neno that she has a strong army sio la kulipuuzaYule ujuaji utamponzs
Jeni ni muongo ukute kakusanya laki 5 tu 😂