Ushauri: Lwandamila afukuzwe haraka sana Yanga

Ushauri: Lwandamila afukuzwe haraka sana Yanga

Huyu ni kati ya makocha wabovu kabisa waliowahi kuifundisha yanga katika kipindi cha miaka 20 iliyopita , ni mara mia kazi hiyo angepewa Kataraia Minziro .

Wana Yanga mtakubaliana na mimi kwamba tangu ameichukua timu hii , kile kiwango cha kimataifa ilichokuwa inacheza timu yenu , kile kiwango kilichoifanya Tanzania ijivunie yanga kimepeperuka mithili ya Njiwa wa uganga .

Fukuzeni huyu jamaa haraka sana kuinusuru timu yenu na aibu inayokuja .
Acha roho mbaya wewe, unajua na yeye ana watoto wanamtegemea? mbona wakati mnafunga hamkusema?

Tulieni mliwe kiboga jamani, mpeni mda ndugu Lwandamina 4G.
 
Kuweka kumbukumbu sawa mimi sio Yanga ni Simba damu ila nawajua watani zangu hawana vifua vya kupokea mabaya!huyu kocha kesho pakikucha atakijua kilichomnyonyoa kanga manyoya.
Utaolewa shauri lako, huku kwetu hainaga ushemeji......
 
Unajua mimi ni Simba damu lakini uzalendo umenisukuma kuitetea yanga , ambayo ni kama imelogwa ! Hivi utaachaje kocha mzuri ( Pluijm ) na kuchukua hili garasa ?
Mkuu kwanini usishughulikie na yahusuyo team yako?
 
Unajua mimi ni Simba damu lakini uzalendo umenisukuma kuitetea yanga , ambayo ni kama imelogwa ! Hivi utaachaje kocha mzuri ( Pluijm ) na kuchukua hili garasa ?
Nani? Kasema Pluijm kaachwa baadhi ya wachezaji wa yanga wana mapenzi na simba wakicheza na timu nyingine utafikiri wanatoka ulaya wakicheza na simba duuuu urojo
 
mi jana nimebishana na watu hadi nikataka kupigwa chupa ...huyu kocha ni kimeo ........nilichoona kipya ni kuwa kipa hapigi mpira mbele direct wanaanziana...kocha gharasa kabisa huyu ...yule mzungu pasi zilikua zinaonekana huyu hata pasi 4 hakuna ...mbinu hatuzioni ...na wamemleta kipindi kibaya mno simba wako kwenye form .....
 
Jamani Wanayanga wenzangu hili nililisema tokea mwanzo,sikuridhia kabisa suala la kumtoa Pluijm na kumleta huyu Mzambia.

Niliwaambia kabisa hofu yangu ni kubwa,haya sasa mambo mnayaona.
cc Guasa Amboni nasmapesa mgaagaa na upwa na wengine wote tuliojadili kuhusu suala la ujio wa kocha mpya kwenye mechi za mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara.
Nifah upo sahihi binafsi naumizwa sana na matokeo mabovu ya yanga..kiukweli yanga kwa sasa haitabiriki, azam si wakutufunga goli 4, zaid Jana nilimshangaa kocha kwann Dida apige penati wakati kina Niyonzima walikuwepo?
Lwandamila haiwezi yanga bora atotelewe tumrudishe babu wa kizungu.
 
1.Juzi wakati mabao ya spid ya 4G yakiwa yanafungwa hamkusema hayo

2. Kumbuka , kocha hukumuana hata mara moja anasimama ama kutoa maelekezo zaidi ya jukumu hilo kuchukuliwa na mwambusi , unadhani itakuwa hivyo daima?

3. Alitumia mashindano haya , kusoma ligi za bongo na kuwajua vizuri wachezaji wake , ubora na mapungufu yao, na amemaliza research sasa subiri ligi ndio utamjua vizuri.
Hana jipya aende zake huko
 
Jamani Wanayanga wenzangu hili nililisema tokea mwanzo,sikuridhia kabisa suala la kumtoa Pluijm na kumleta huyu Mzambia.

Niliwaambia kabisa hofu yangu ni kubwa,haya sasa mambo mnayaona.
cc Guasa Amboni nasmapesa mgaagaa na upwa na wengine wote tuliojadili kuhusu suala la ujio wa kocha mpya kwenye mechi za mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara.
Mkuu hz mbio za mita 100 tulizianza kwa speed kubwa sana kwa kumpa mtu goli 6,ttz letu lilianzia pale kwa uongozi hadi wachezaji,mechi ya azam yale matokeo yakaamsha hamasa ya wengine na kutufanya kukumbuka shuka wakati kushakucha,tunarudi kwenye marathon(vpl) kurudisha heshima,hao wanaopiga kelele huu ni wakati wao,muda utaongea tu
 
Manji anaharibu yanga kocha kutwa anajishika shavu mrudisheni plujin
 
Ni mapema mno kuchukua maamuzi ya kumfukuza.
 
Jamani Wanayanga wenzangu hili nililisema tokea mwanzo,sikuridhia kabisa suala la kumtoa Pluijm na kumleta huyu Mzambia.

Niliwaambia kabisa hofu yangu ni kubwa,haya sasa mambo mnayaona.
cc Guasa Amboni nasmapesa mgaagaa na upwa na wengine wote tuliojadili kuhusu suala la ujio wa kocha mpya kwenye mechi za mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara.

Huyu mzambia hajui mpira timu haijawahi kufungwa goli 8 mechi mbili,i suggest wamrudishe babu mzungu mpaka ligi iishe. Mpira wetu umekuwa mbovu na wenye makosa mengi sioni namna ya kutetea vikombe vyetu vikubwa tanzania na kufanya vizuri ligi ya mabingwa 2017 tukiwa na huyu mzambia.
 
Huyu ni kati ya makocha wabovu kabisa waliowahi kuifundisha yanga katika kipindi cha miaka 20 iliyopita , ni mara mia kazi hiyo angepewa Kataraia Minziro .

Wana Yanga mtakubaliana na mimi kwamba tangu ameichukua timu hii , kile kiwango cha kimataifa ilichokuwa inacheza timu yenu , kile kiwango kilichoifanya Tanzania ijivunie yanga kimepeperuka mithili ya Njiwa wa uganga .

Fukuzeni huyu jamaa haraka sana kuinusuru timu yenu na aibu inayokuja .
Mtu wa mikia kutaka kocha wa Yanga afukuzwe inasema mengi. Mikia wanamwogopa kama ukoma.
 
Kama kawaida mnyama kamfundisha ndala mpira.pole kama we mwana-yanga.
Unakumbuka mtani jembe.. Si mlikuwa mnashinda watoto mfurahi... Dida anapiga penalt ya kwanza BONANZAAAA
 
Back
Top Bottom