Ushauri: Mahari ifutwe?

Ushauri: Mahari ifutwe?

Mahari iendelee.
-Ni shukrani kwa wazazi kwa kukubali muunge udugu.
-Kuonesha upo tayari kuwajibika kwa mke na familia.
-Kuonesha upendo na kumkubali mtu.
-Ni jaribio tosha la kuonesha utayari wa kuiishi ndoa.
NB:Utoaji mahari uendelee ila viwango viongezwe ili mtu akiona mwanaume kaoa awe na heshima kwa ndoa za watu.
 
nimsomeshe halafu kamaliza anataka kuolewa aende bure
So unamsomesha ili iweje ,na wakiume husomeshi. Mie Nina dada na nimetanguliza mabinti kuzaa Ila sijaona logic. Yaani Kama unafanya kitu kwa mdogo wako ama kwa mwanao kwa mategemeo fulani usipoyapota utaumia Mara mbili ama sio kumi.
 
Labda wewe tuu ndio uamue kwamba hutahitaji mahari kwa binti yako. Lakini katika jamii hilo jambo haliwezi kuja kutokea. Niamini mimi
 
Basi
Mahari iendelee.
-Ni shukrani kwa wazazi kwa kukubali muunge udugu.
-Kuonesha upo tayari kuwajibika kwa mke na familia.
-Kuonesha upendo na kumkubali mtu.
-Ni jaribio tosha la kuonesha utayari wa kuiishi ndoa.
NB:Utoaji mahari uendelee ila viwango viongezwe ili mtu akiona mwanaume kaoa awe na heshima kwa ndoa za watu.
Basi why watu mna bargain Kama Ni kuunga mkono kuunganisha undugu
 
Ila inakera sana 🤣🤣yaani nikama bizinesi.....yaani next week kuna watu wameniandikia barua wanataka 3.5m..........ila nitapeleka Kwa heshima ya mchumba wangu tu cos nilimkuta bikra 🤣, tofauti na hapo ingekuwa ngumu
 
So unamsomesha ili iweje ,na wakiume husomeshi. Mie Nina dada na nimetanguliza mabinti kuzaa Ila sijaona logic. Yaani Kama unafanya kitu kwa mdogo wako ama kwa mwanao kwa mategemeo fulani usipoyapota utaumia Mara mbili ama sio kumi.
Hili jambo ni utamaduni. Ndio maana kiafrika mwanamke anaolewa na mwanaume anaoa na siyo kinyume chake
 
Basi

Basi why watu mna bargain Kama Ni kuunga mkono kuunganisha undugu
Kuomba punguzo muhimu.Mtanzania/Mwafrika/binadamu bila punguzo hata kidogo haridhiki.Halafu,kwa tabia za familia zetu usipoomba punguzo unaonekana ni jeuri,unajidai,una dharau na siyo mbembelezaji.Unajipunguzia sifa.
 
Why ung'ang'anie traditional ambazo sio productive or faida zake hazina Mana. Watu huwa wanaumia mahari zao mke akiaanza kuzingua
Kuzinguana ni ajali kama ajali zingine.Ukiweka mawazo ya kushindwa kabla haujatenda unajishushia pointi.Usiwaze sana ulichotoa kama mahari mwisho wake ndiyo utaanza kuishi na mwenza wako kama mfugo.Au hata kumtendea ubaya na vipigo juu.Fanya kama ulinywea "bia" ukafurahisha nafsi tu.
 
Habari!

Hii mada imejadiliwa mara nyingi na sehemu nyingi.

Je, Mahari inayotolewa ili kijana aozeshwe ifutwe?

Kama ifutwe toa sababu, kama uendelee toa sababu.
Dah ukiwa Muislamu ni Raha sanaaa huna muda wa kuwaza wala kuuliza maswali kama haya

AM PROUD TO BE MUSLIM
 
Habari!

Hii mada imejadiliwa mara nyingi na sehemu nyingi.

Je, Mahari inayotolewa ili kijana aozeshwe ifutwe?

Kama ifutwe toa sababu, kama uendelee toa sababu.
Hakuna cha bure toeni mahali, hiyo ipo ni utamaduni kufutika ni kazi nzito labda unaweza badilika kwa format nyingine lakini si kufutika.
 
Mahari ifutwe, hata waliotuletea huo utaratibu ambao ni Wazungu wameuacha.
Nani kasema walioleta huo utaratibu ni wazungu??? Hivi kumbe hujui kama ni sehemu ya utamaduni wa Mwafrika sio Kila kitu kaleta mzungu, yaani unataka kusema na ule utani unaokuwepo Wakat wa kutoanmahari ni mzungu kaanzisha ?? Yaani unataka kutuambia Kwa wachaga mzungu aliwaambia unapoenda kutoa ni mahari lazima uweke na mbege, kama hujui useme sijui, na kama hauna mahari ya kwenda kulipa narudia tena sema Watu wakuchangie uoe utulie, otherwise weka hoja
 
Habari!

Hii mada imejadiliwa mara nyingi na sehemu nyingi.

Je, Mahari inayotolewa ili kijana aozeshwe ifutwe?

Kama ifutwe toa sababu, kama uendelee toa sababu.
Daah hiili suala linahuzunisha sana kuna Jamaa Jana alikua anasimulia ameshindwa kuoa sababu ya Mahari yaani unaambiwa ukweni walimwambia alipe Million 2 na Laki 5, shughuli anazofanya na malipo ya mahari haviendani kabisa hivyo amebaki kuishi uchumba sugu huu mwaka wa 10 bado hajaoa mke kashamzalisha watoto watatu ila ndoa hawajafunga kisa Mahari parefu

Mahari hizi au vikwazo vya kutokuoa?
 
Back
Top Bottom