Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443


Kwanza ningependa kukupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuliboresha jiji letu hili la Dar. Nimekuwa nikifuatilia juhudi zako tangu ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Naamini jitihada zako za kutaka kuboresha wilaya ya Kinondoni ndizo zilizomfanya Raisi akuongezee majukumu kutokana na kuona jinsi unavyochapa kazi.

Kwa muda sasa nimekuwa nikiona unaibuka kila siku na matamko ambayo baadhi ya matamko hayo hayajafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano suala la ombaomba. Kwa ushauri wangu kabla ya kutoa matamko naomba ufanye utafiti mdogo kwanza na kujiridhisha na kuweka mpango kazi wa namna ya kutatua tatizo kabla ya na kutoa tamko kwamba hutaki jambo fulani katika mkoa wako. Kuna vita vingine hutaviweza zaidi ya kujifedhehesha.

Kwa ushauri wangu naomba uweke vipaumbele katika mambo yafuatayo.

=Kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule zetu

=Kuongeza na kuboresha maabara katika shule zetu

=Kujenga maktaba katika shule na maeneo mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya kata na kuhakikisha kunapatikana huduma za inteneti na magazeti ya kila ziku hapa unaweza kuzishirikisha kata kutenga maeneo kwa ajili ya kujengwa kwa maktaba hizo ili kuhimiza watu kujisomea na kuongeza maarifa na sio kupiga soga vibarazani na kunywa kahawa

=Kuhakikisha jiji linakuwa safi kwa kuweka sheria ndogo ndogo kali zitakazowabana wachafuzi wa mazingira na ili kulitekeleza hili unaweza kupata uzoefu kutoka kwa viongozi wa mji wa Moshi

=Kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutumika hapa jijini na badala yake wenye viwanda hivyo kulazimishwa kuzalisha mifuko ya karatasi kwa ajili ya matumizi au kushirikiana na SIDO kuja na njia mbadala ya mifuko ya karatasi ambapo ubunifu huo unaweza kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya vijana na kina mama..

=Kutengeneza maeneo ya vivutio kwa watalii wanaokuja katika jiji letu kwani wengi hupita tu kwa sababu hakuna vivutio. Hili unaweza kuwashirikisha wabunifu na wakandarasi wetu na kutenga maeneo ambayo yana historia na kuyaboresha kwa kiwango ambacho kitavuta wataalii wengi kutumia siku kadhaa katika jiji letu kwa mfano kama mji mkongwe wa Zanzibar, na Makumbusho ni eneo mojawapo ambalo linaweza kuboreshwea zaidi.

=Kuweka utaratibu mzuri wa boda boda, kwa sasa bodaboda pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar lakini zimekuwa ni chanzo kikuu cha ajali hapa jijini na vijana wengi wamekufa au kupoteza viungo na hivyo kutishia nguvu kazi hapa nchini. Tusipoweka utaratibu na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na madereva kuheshimu sheria za barabarani na kuweka sheria kali kwa watakaokiuka miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na ukosefu wa nguvu kazi.

=Tenga maeneo mengi kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na maeneo haya yakabidhiwe VETA ili vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo wapate fursa nyingine ya kujifunza masomo ya ufundi lakini pia ni vyema kukitengwa maeneo ya mafundi wetu kwa mfano mafundi wa magari kuwe na eneo lao, mafundi seremala wae na maeneo yao kama vile Keko, mafundi wa kuchomea vyuma wawe na maeneo yao ili wenye kuhitaji huduma hizo wawe wanajua zinapatikana wapi na kuondoa hizi vurugu mitaani

=Rejesha viwanja vya michezo vilivyovamiwa na hakikisha swala la viwanja vya michezo linapewa kipaumbele, na michezo isiwe ya aina moja, ongeza wigo wa michezo mbalimbali ili na sisi tuweze kushiriki michezo ya olimpiki.

=Mabango na matangazo yawekewe utaratibu maalum siyo kila mtu akiwa na tangazo lake anapita mitaani na kuchafua kuta za watu itungwe sheria kuondoa tatizo hilo n ahata haya makampuni ya matangazo nayo pia yawekewe utaratibu maalum kuondoa mabango mengi mitaani na kufanya jiji lisionekane nadhifu.

=Wanaohubiri usiku kucha na kelele za mziki kwenye mabaa katika makazi ya watu zipigwe marufuku na kila Pub kama watataka kupiga mziki kwa sauti ya juu basi lazima wawe na ukumbi usioruhu sauti kutoka nje.

=Njoo na njia mbadala ya kuhimiza matumizi ya baiskeli kwa wale wanaofanya kazi maeneo ya karibu na hili litafanikiwa kwa wakandarasi wetu kubuni njia ya waendeshao baiskeli ili kuepuka bughdha kwa watembeao kwa miguu. Mpango huu unaweza kuanza na zile barabara ndefu kama Tegeta mpaka Posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Mbagala mpaka Posta.

Mimi naamini kama ukiweka vipaumbele kwenye mambo hayo machache kati ya mengi ambayo sijayazungumzia utaacha historia katika jiji hili na utakumbukwa na vizazi vijavyo.

Unaweza kuitisha mdahalo kwa wakazi wa jiji hili ili kupitia mdahalo huo uweze kuibua mbinu mbalimbali za kuboresha jiji letu. Naamini wakaazi wa jiji hili hawafurahishwi na hali jinsi ilivyo kwa sasa na wangependa hali iwe nzuri zaidi kwa kuondoa kero nilizozitaja hapo juu, iwapo utawaalika kwenye mdahalo watakupa ushirikiano.

Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako ya kila siku.

Ni mimi Mzee Mtambuzi.





 
Kwani majukumu ya mkuu wa mkoa ni yapi? Mimi naona kama wamepewa mamlaka na uwezo wa kuagiza na kutoa matamko majukwaani, basi wana uwezo sana wa kushauri na kuyasimamia hayo mambo kama anavyosema mkuu mtambuzi, tofauti na hapo hii position ya mkuu wa mkoa iondolewe tu kwenye katiba.
 
Mkuu KayScarpetta unayosema ni kweli kwani kwa sasa matamko anayoyatoa hayana impact kubwa kwa jiji letu la Dar katika kulifanya kuwa bora. Yeye kama Mkuu wa mkoa wa Dar anatakiwa kushirikiana na Jiji ili kutekeleza hayo niliyoyasema najua anao uwezo huo kwa nafasi yake aelekeze nguvu zake hapo
 
Ushauri mzuri sana.

Bahati mbaya mambo haya akiamua kuyatekeleza hayatampa airtime sana kwenye media.

Na yeye anapenda kupewa airtime.

Mimi naamini kwamba muungwana ni vitendo na siyo kelele za majukwaani.
 
Ushoga na shisha kwanza mengine badae.
Kuna mambo ni madogo lakini yanakera sana hasa uvutaji sigara hadharani. kama tukiwa serious jambo hili linaweza kumalizwa ndani ya muda mfupi sana.mimi namuunga mkono kwasababu anataka kuleta ustaarabu! siyo kila mahali unakuta mtu anavuta misigara yake.

Ama kuhusu mashoga, dawa ni nyepesi tu ni kuweka adhabu kali kwa wateja wao wakikamatwa walipishwe shs mil kadhaa wakishindwa wafanye kazi ya kusafisha mitaro michafu na kusaidia kuzoa taka kwa muda wa miezi mitatu.
 
Leo akiwaapisha wakuu wa wilaya wapya amewaagiza wakapambane na omba omba kwenye wilaya zao. Hili linashangaza sana! Hivi ombaomba, madada poa, wabwia shisha na mashoga ndo matatizo ya Jiji la Dar? Au anatafutia umaarufu tu?

Tatizo kubwa kuliko yote hapa Dar ni msongamano wa magari, tatizo sugu la maji, uchafu ambao hata ofisi yake na maeneo yake ni machafu! Hivi huyu aliyeanzisha program ya usafi aka-fail, program ya usalama aka-fail, walimu kusafiri bure aka-fail, machangudoa aka-fail ndo ataweza omba omba?

Si amuulize mzee Makamba aliyempa Matonya nauli akarudi Dodoma akaondoka kwenye ukuu wa mkoa akamuacha. Amuulize mzee wa watu alivotaka kuwaondoa madada poa aliambulia majina gani. Hii inaonyesha jinsi gani wakuu wa mikoa hawana kazi maana anajua wapo wanaofikiria maji, barabara na miundombinu kwa ujumla, afya, elimu, nishati nk.
 
Chadema watatetea kila aina ya uozo mwaka huu.

Majizi, mafisadi, mashoga, vibaka, wakwepa kodi, wavuta shisha wote mtetezi wao ni chadema!!!

Hii ndio maana ya chama kubadili gia angani.
 
Chadema watatetea kila aina ya uozo mwaka huu.

Majizi, mafisadi, mashoga, vibaka, wakwepa kodi, wavuta shisha wote mtetezi wao ni chadema!!!

Hii ndio maana ya chama kubadili gia angani.
Chadema inaingiaje hapo? Au ukilala unaota Chadema?
 

Mkuu zipo Tobacco Regulations zinazozuia uvutaji wa sigara hadharani,sema tu sheria nchi hii hazitiliwi manani.
 
Natamani umpe kichwa chako maana yule sifa zimemzidii
 
MKOA HUU BWANA. SAFARII HII UMEPATA KIONGOZI MKALI KWERI KWERI narudia mkali kweRI kweRI . nakumbuka mdogo wangu mmoja anasema walikuwa na mwalimu mmoja WA NIDHAMU alikuwa anaitwa BOB MIKWARA alikuwa anatoka ofisini kwake anasimama assembly akiwa juu na wanafunzi wake chini anatoa matamko kwa sauti kali sana akitokwa na mate,jasho na mishipa ya kichwa kumsimama. halafu anarudi ofisini kwake anapiga selfie anarushia mtandaoni huku ameweka miguu juu ya meza ndo inakuwa imepita hiyo mpaka Jumatatu ijayo tena.
haya mawazo ya Wadau mbali mbali kuhusiana na Matamko mbali mbali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa DSM.

.SIPINGANI NA MAKONDA KUHUSU MAAGIZO YA JANA Dar Es Salaam LAKINI NINA "VIJIWAZO VYANGU KIDOGO":
●Mkuu kasema watu wasiwafollow mashoga (facebook, instagram, tweeter n.k) na adhabu baada wiki itafuata, JE MBONA NYIE MNAGUSANA NAO NA PICHA MNAPIGA NAO? JIKAMATENI KWANZA!!!!!!
●Suala la kukataza uvutaji shisha na sigara uko sahihi mkuu, LAKINI MBONA UNATAFUTA "KIKI" KWENYE MAMBO MADOGO WAKATI NDUGU ZENU WANATESEKA NA MADAWA YA KULEVYA KILA UCHAO? KATI YA SHISHA, SIGARA NA COCAINE/HEROINE KIPI UNADHANI KINATEKETEZA NGUVU KAZI YA TAIFA?
■■Pamoja na nia yako njema chief Makonda hebu anza na mambo makubwa haswa hili la madawa ya kulevya maana inaaminika kuwa hilo ‪#‎HALIGUSIKI‬
: MH MAKONDA:
■Umetenga maeneo ya kuvutia sigara (smoking zones) kama ilivyo ktk miji mingine mfano Nairobi Mombasa n.k?
■Vp suala la usafiri bure kwa walimu kwenye daladala liliishia wapi?
■Ishu ya ombaomba imeishia wapi?
■Madada poa je?
 
huyu anaongoza kufanya hata majukumu ya madiwani. binafsi siafiki tabia hii...
 


mkuu wa mkoa unatakiwa kufuata sheria ya barabara kwa kuwaonyesha mfano wananchi hapo haujafunga mkanda ni kosa kubwa sana kama trafiki akikushika ni sawa na yule mke wa waziri na trafiki aliyerushiwa maneno.Jaribu kuwa mstari wa mbele kuwaonyesha wananchi sio kuvunja sheria.

swissme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…