Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

PAULO MAKONDA MBABE WA VITA HHHAHAHAH
 
lile tamko lako la kugushi WEWE MZUSHI Mwanahabari huru kuwa meya ndio kalitoa kupingana na Makonda ulilitoa wapi?

Meya kalikanusha naona umebadilisha staili sasa unaandika wewe ndio Julius Mtatiro.Ina maana Mwanahabari huru ndio Julius Mtatiro au unaendelea na mchezo wako wa kujifanya wewe ndie wakati sie kama ulivyofanya kwa meya?

unaweweseka wakati dawa inaingia
 
lile tamko lako la kugushi WEWE MZUSHI Mwanahabari huru kuwa meya ndio kalitoa kupingana na Makonda ulilitoa wapi?

Meya kalikanusha naona umebadilisha staili sasa unaandika wewe ndio Julius Mtatiro.Ina maana Mwanahabari huru ndio Julius Mtatiro au unaendelea na mchezo wako wa kujifanya wewe ndie wakati sie kama ulivyofanya kwa meya?

Mkuu sometimes na kuona kama hukwenda shule. Ndo maana Watu Kama nyinyi ngosha akichkua chama mtaishi kwa shida sana. Maana hata propaganda hamzijui Kabisa. Hata ungekuwa umejitoa ufahamu lakini kwa uelewa WA chini kabisa hata wewe unajua hiyo plan ya mkuu WA mkoa haitekelezeki. How? Ofcourse kwa level yako...I would be asking too much lakini I suggest uwe unajiongeza. Hiki in kipindi cha Magufuli. Mtalia na kusaga meno Kama hamtabadilika.

Sometimes naona Baadhi ya vijana wanatuangusha wakipewa madaraka. Dar tuna changamoto nyingi sana ambazo RC angeweza akazitatua kwa Faida ya wote. I mean akina Jerry Slaa, Masha etc...in vijana walikuwa na potential ta kung'aa...Leo wako wapi?
 
Rc wangu Paul Makonda naomba ujirekebishe Tabia yako ya kutaka kusikika kila siku kwenye media ukitoa matamko yasiyotelelezka kama hayo ya ushoga na sheesha yanakuharibia credit yako kwa JPM.

Una m-let down mh JPM maana tangu uingie madarakani ni kutoa tu matamako bila utekelezaji.Mara usafi ambao hadi leo jiji ni chafu , mara omba omba bado wamezaga, mara ushoga mara shisha yani una matamko mengi ambayo hayatekeleziki na kwa kiasi kikubwa unakichonganisha chama na wanachi maana unavyoboronga watu hawasemi Makonda kaboronga wanasema CCM imeboronga.Yani sasa kila mtu anakuzungumzia kwa mabaya. Mara msako wa nyumba kwa nyumba yani natamani mh JPM akuhamishe akupeleke hata Katavi maana kadri siku zinayokwenda unazidi kuboronga.

Nakushauri achana na kina Steve Nyerere na wasanii wasioenda shule kupiga nao picha na kupost instagram, nenda pale UDSM kakutane na wasomi wakusaidie jinsi ya kutatua kero za mkoa wako.

RC gani kila siku unakutana na wasanii utafikri umekuwa mshamba wa wasanii!! Ina maana hujawazoea tu.?

Piga kazi kaka usimuangushe Rais ukamfanya ajute kukuteu, kumbuka kuna vijana wengi wanangojea kwa hamu kubwa ukosee upigwe chini wachukue nafasi hiyo kaka.

Ni ushauri tu, tuliza kichwa utatue kero za msingi za wana dsm.

Wasalaaaam, mimi nduguyo ALWATANI KIZIGO
PO BOX ILALA
 
unaweweseka wakati dawa inaingia

Habari zako hazina credibility.Mtu anayejiamini haanzishi habari na kuandika jina la mtu mwingine.Ina maana wewe huwezi simama kama wewe ukaandika habari yako kwa kujiamini hadi usingizie kuwa hili ni tamko la meya au nani sijui.Una matatizo ya kisaikolojia unahitaji kuwaona madaktari hasa wa magonjwa ya kichaa
 
Mkuu hizo marufuku zimezidi kila kitu ni marufuku sijui tunaelekea wapi... baada ya muda utasikia na wale mafundi viatu hawatakiwi hapa mjini hao wauza kahawa wanajishuhulisha tayari wanafanya kazi halali,nadhani atekeleze moja kwanza.
 
Mkuu wetu wa mkoa na kijana mwenzetu, huna haja ya kuzungusha Polisi mitaani kukamata Raia wasio na hatia kwa kutumia mamlaka yoyote unayodhani unayo. Common Sense peke yake haikubaliani na jambo hilo;

1. Zoezi lenyewe haliwezekani na halitekelezeki hata kidogo. Halina BASIS za kisheria wala KIMAADILI, kwa hiyo ni NULL and VOID tangu tu ulipolitangaza.

2. Litazua vurugu, balaa na machafuko mitaani na litashindwa kwa asilimia 100 na ni aibu sana kwa kijana mwenzetu ku attempt vitu visivyowezekana.

3. Nakupa ushauri wa bure ndugu yangu, kwamba kama anataka kuwabaini na kuwakamata wakazi wa DSM wasiofanya kazi na wasio na ajira, hebu pitia daftari la Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2012. Takwimu za sensa zimeeleza vizuri sana, mtaa gani una vijana wangapi na hali zao zikoje. Usiwahangaishe polisi.

4. Kisha, toa maelekezo kuwa vijana hao na wananchi wasio na shughuli za kufanya waje wenyewe ofisini kwako, taja tarehe na muda. Mimi kwangu ninao kama 7 hivi, ntawaleta mimi mwenyewe kisha ntakuachia uchukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria kwa makosa yao ya kutokuwa na shughuli za kufanya.

5. Wewe ni kijana mwenzetu na kila unapotoa matamko dhaifu na yasiyo na tija kwa taifa unafanya wananchi wote waamini kuwa VIJANA wa taifa hili hawajakomaa na hawako tayari kuongoza nchi. Ikiwa viongozi vijana tunashindwa kupigania ajenda muhimu za kijamii pindi tunapokabidhiwa mamlaka ya uongozi wa nchi, tunaiandaa jamii itupe hukumu gani mbeleni?

6. Comrade Paul, wewe ni kiongozi mwenye utashi na kwa tunaokufahamu tunajua unayo talanta bora ya uongozi, lakini umeiweka kando. Hivi sasa unaendeshwa na ukuu na kutikisa watu bila sababu. Yuko wapi yule Makonda ambaye aliendesha kampeni ya usafi jijini DSM? Iliishia wapi kampeni ile? Mbona wananchi walikuunga mkono brother? Usafi uliona hautoshi sasa unataka kuwasaka wasio na kazi? Ili iweje? Na unadhani nani atakubali kusakwa na kukamatwa kwa sababu hana kazi, kazi ambayo hajawekewa mazingira ya kuipata kwa kuajiriwa au kujiajiri?

7. Ndugu Paul, unakumbuka ulitangaza kuendesha msako wa ombaomba? Unakumbuka tulivyokuunga mkono? Jamii nzima ya DSM. Ombaomba ni kero kubwa sana na hawapaswi kuchekewa, ukifanya zoezi la kuwarudisha vijijini kila mtu atakuunga mkono. Unakumbuka zoezi la kukamata SHISHA na watumiaji wake? Unakumbuka tulikupongeza na tulikuusia kuwa ungelianza na wasambazaji wa madawa ya kulevya kwanza? Maana COCAINE na HEROIN zinauzwa kama njugu hapa jijini tena huenda unawajua wauzaji hadi majumbani mwao, tulikushauri tu.

8. Kaka Paul, kwa mtizamo wangu, anza kujifunza kujenga DAR yenye utulivu, yenye mipango inayotekelezeka na yenye maelewano. Kamwe usijifunze kuanzisha mazoezi yasiyotekelezeka au ambayo yakitekelezeka yanaweza kuleta balaa kubwa. Unaikumbuka ARAB UPRISING? Ilianzaje? Kijana hana ajira, anajiuzia mbogamboga askari wakaenda kulivunja na kulichoma banda lake na mboga zake, kijana yule akaamua kujitia PETROLI, akaungua hadharani, video zake zikasambazwa, jamii ikashikwa na ghadhabu, maandamano yakaanza mataifa ya Uarabuni, watawala wakang'olewa. Chanzo cha maafa ya Uarabuni ni watawala kushindwa kuweka mazingira rafiki ya ajira kwa jamii zao na kisha watawala hao hao wakaanza kuwanyanyasa watu wasio na ajira.

9. Kiongozi wangu Makonda, UKOSEFU WA AJIRA au SHUGHULI ZA KUFANYA ni bomu lililotulia mahali na aliyelilea anafahamika, ni chama chako, CCM. Chama ambacho kimekupa ukuu wa mkoa ndicho kimeongoza taifa hili kwa miaka 50 sasa, kimeshindwa kuitumia nguvu kazi ya taifa na leo tuongeapo, mamilioni ya vijana hawajui nini wafanye. Hata ajira za kuuza pipi zinafanywa na WACHINA. Hawa vijana unaotaka kuwasaka majumbani watafanya nini? Kwa nini unataka kulitegua BOMU lililojituliza huku hauna utaalamu huo? Likilipuka kwa vyovyote vile hautabaki salama! Utapata madhara. Bomu hili linahitaji PATIENCE na CALMNESS, linahitaji wataalamu waliobobea waje na vifaa vyao. Huwezi tu kubeba ndugu zetu POLISI na kuwabambikizia oparesheni isiyo na nguvu ya kisheria na inayoweza kuleta vurugu na matatizo mitaani.

10. Mdogo wangu Paul Makonda, wanasiasa wengi huwa hawapebdi kushauriwa hadharani, hukasirika na kuwaona washauri wa namna hiyo kama watu wanaowachukia. Mimi ni mwanasiasa kijana kama wewe na huwenda nimewahi kushika majukumu makubwa sana. Huwa nafurahi sana kila nionapo watu wananishauri hadharani, hasa kwa lugha ya heshima kama niliyotumia hapa. Mara kadhaa umewahi kuwa na hofu nami hasa nilipowahi kukukosoa sana kwa hatua ya kumkamata mbunge Kubenea na kumuweka ndani, niliwahi kukukosia pia ulipowaweka ndani watumishi wa halmashauri kwa kuchelewa kazini. Sijawahi kufanta hivyo kwa nia mbaya ,mara zote dhamira yangu inanisuta napoona kijana mwenzangu anaharibu kwenye uongozi. Huwa natoa ushauri huo kwa kijana yeyote yule bila kujali anatoka chama gani. Ni kama mimi mwenyewe navyopenda kupokea ushauri kutoka kokote, ilimradi utumie lugha inayokubalika. Mimi ni kati ya watu ambao wataendelea kukushauri na kukukosoa, bila kujali kuwa unaweza kuchukia na kukasirika kama wanavyoogopa wanasiasa wazee, wanapokosolewa hadharani. Sitajali, ntaendelea na kazi. Kumbuka, anayekukosoa ANAKUPENDA NA KUKUTAKIA MEMA, anayekusifia wakati unakwenda kutegua mabomu bila wataalamu, ANAKUTAKIA MABAYA.

Julius Sunday Mtatiro,
Likes 1000
 
Vijiwe vya pombe ni poa lakini vya kahawa tatizo?

Kila nchi ina utamaduni wake, nchi zingine utamaduni wao kutwangana risasi sasa unataka wakae nje sehemu gani wanywe kahawa kwa amani?
 
Kuna watu wameteuliwa maeneo flani kwa sababu maalumu ndio maana unaona kuna yule aliekua anapiga vita nafasi za ukuu wa mkoa/wilaya katolewa kule na kuwekwa hapo.

Wengi hawafahamu sababu ni nini ila amini nawaambia sababu ilishakuwepo na sasa ipo ila hawa wote na utawala huu utapita kama tawala zingine zilivyopita.
 
Back
Top Bottom