Nimetembelea mikoa yote mikubwa Tanzania nikajionea vituo vya mabasi makubwa katika namna tofauti, nikianza na Ubungo jijini Dar, Nyegezi cha jijini Mwanza, Stand kuu na kile cha nanenane vikiwa jijini Mbeya, Stand kubwa jijini Arusha, Stand kuu ya jijini Tanga na kuna vingine vya miji kama Iringa, Moshi, Dodoma, Bukoba n.k
Kilichofanya niandike huu uzi ni maendeleo ya ujenzi na uboreshaji wa kituo cha mabasi Msamvu kilichopo mkoani Morogoro. Kwa aliyepita hivi karibuni pale Msamvu Morogoro atakuwa amenielewa nini namaanisha.
Kituo cha mabasi msamvu kitakuja kuwa kituo bora na cha kisasa cha mabasi Tanzania nzima kwa ujenzi wa kisasa unaoelekea kuisha katika kituo kile unaofanywa na kampuni kubwa ya ujenzi ya GROUP SIX.
Swali nililojiuliza fedha za ujenzi wa kile kituo umetokana na bajeti ya serikali 2017 kuhusu miundombinu, ni hela za makusanyo ya halmashauri ya mji wa morogoro mjini, kuna mfadhili binafsi wa ule ujenzi au ni pesa iliyopatikana katika tozo za kuingia na kutoka za watu na magari pale kituoni?
Nimesema ni somo kwa Mh Paul Makonda na Dar kwa sababu hali ninayoiona Stend ya ubungo jijini Dar kila siku inasikitisha na ikizingatiwa ndio kituo cha mabasi kikubwa kinachoongoza kukusanya mapato makubwa kwenye vyanzo tofauti kama parking ya mabasi makubwa, frem za biashara, mbao za matangazo na ndio kituo pekee nchini Tanzania kinachotoza pesa kwa mtu anayetaka kuingia kituoni kama si msafiri.
Jiji la dar lina milango mikuu ya kuingilia kama minne ukianzia uwanja wa ndege, stesheni ya treni, bandarini lakini mlango mkubwa ni stand ya ubungo ambao ndio mlango mkubwa sana wa jiji la dar unaohudumia maelfu ya watu kila siku.
Swali langu kwa mkuu wa mkoa Mh Makonda kwanini hali na mazingira ya stand ya ubungo inaendelea kuwa mbaya kila siku ilihali ina kusanya mamilioni ya fedha katika vyanzo vingi?
Tunajua ulifanya mpango mkamsimamisha ndugu Kabwe baada ya kugundua ubadhirifu wa pesa aliofanya pale ubungo kwa mikataba ya ulaghai, nafikiri ni mda mzuri sasa kwako ndugu Makonda ukishirikiana na wenzako kuirekebisha ile stand ya ubungo ikizingatiwa kwamba inahudumia maelfu ya watu kila siku, na ikizingatiwa imekuwa inakusanya mabilioni ya fedha kila mwaka mana stand ya ubungo imekuwa kama jumba lililo gofu ambalo halina mmiliki.
Nimetumia stand ya Msamvu mkoani Morogoro kama mfano kwa kuwa ni stand itakayokuja kuwa ya kisasa nchini baada ya kukamilika, na na shauri halmashauri za miji na majiji mengine nchini Tanzania ziige kutoka halmashauri ya mji wa Morogoro kwa ujenzi wa kisasa wa ile stand.
Nitawaletea picha za stand ya Msamvu mjionee mapinduzi ya vituo vya mabasi makubwa Tanzania