Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Michango yetu wanachama wa LAPF ndio inajenga hiyo bus stand nakukumbusha kua serikali ni kama washangiliaji tu
 
Ni kweli mdau, Stand za mbezi mwisho na mawasiliano jijini dar zimejengwa vizuri ila haziwezi kufikia stand ya msamvu pale morogoro kwani pale msamvu pamejengwa hadi mall na sehemu za kupumzikia zikiwa na ghorofa.
Soon nakuletea picha ya pale stand msamvu
Master plan katika ubora wako.
Nmeanzisha thread ya Arusha kule kwenye Kenya forum njoo upinge na kutukana
 
Master plan katika ubora wako.
Nmeanzisha thread ya Arusha kule kwenye Kenya forum njoo upinge na kutukana
Acha hizo mdau jonax,
Njoo tujenge nchi huku, sababu huwa simuelewi Mh Makonda kila siku anatoa matamko hapa jijini Dar lakini anaiacha stand ya ubungo ikiwa na ukiwa yani ni kama gofu sasa pale ubungo au kichaka cha wahuni. Anashindwa na halmashauri ya mji wa morogoro kwa mipango yao endelevu kama ya ujenzi wa kisasa wa stendi kama ile ya msamvu.
 
Acha hizo mdau jonax,
Njoo tujenge nchi huku, sababu huwa simuelewi Mh Makonda kila siku anatoa matamko hapa jijini Dar lakini anaiacha stand ya ubungo ikiwa na ukiwa yani ni kama gofu sasa pale ubungo au kichaka cha wahuni. Anashindwa na halmashauri ya mji wa morogoro kwa mipango yao endelevu kama ya ujenzi wa kisasa wa stendi kama ile ya msamvu.
Embu weka picha kwanza ya stand ya msamvu ili niisaminishe maana huu mwaka sijafika Moro zaidi ya kupapita kwa juu nikielekea mbeya.
Ila stendi ya pale Mbeya iliyoko Nane nane ndo nmeona iko poa balaa
 
Ndg yangu usiumize kichwa bure. Ile Stendi ya Msamvu inajengwa na LAPF, Manispaa ya Moro na Wachina. Haijengwi kwa fedha za manispaa ya moro au bajeti kutoka serikali kuu. Ule ni uwekezaji unaofanywa na LAPF wakishirikiana na manispaa ya Moro. Stendi ya Nane nane Mbeya imejengwa kwa msaada wa World Bank. Walitoa pia fedha kwa ajili ya ujenzi wa stend ya mkoa wa Iringa. Stendi ya mkoa wa Iringa mpaka leo haijajengwa kulikua na mvutano wa mahali pa kujenga

Michango yetu wanachama wa LAPF ndio inajenga hiyo bus stand nakukumbusha kua serikali ni kama washangiliaji tu
Hawa LAPF kwa kushirikiana na Halmashauri ya mji na uongozi wa mkoa wa Morogoro wanatakiwa wapewe pongezi katika hili la ujenzi wa kisasa wa stand ya mabasi msamvu.
 
Hakuna atakalolifanikisha. Yote hayo hayapo katika mamlaka take and more worse anawa discourage wale wenye mamlaka Mayo (madiwani na mameya) kwa kuwa tu in Wa upande mwingine.
Bahati nzuri ni kwamba as of now, nafasi ya RC wa imeshafanyiwa shortlisting ya mtu mpya. Makonda si kiungo kizuri...wala mtu sahihi Ku fit pale.
Ana kelele nyingi, kuliko matokeo na hizo kelele ndiyo only cover ya mapungufu take.
 
Akomae na Ma-jobless kwanza.Awarudishe wote bush wakalime mpunga
 
Chadema watatetea kila aina ya uozo mwaka huu.

Majizi, mafisadi, mashoga, vibaka, wakwepa kodi, wavuta shisha wote mtetezi wao ni chadema!!!

Hii ndio maana ya chama kubadili gia angani.
duu kichaa chako kimekurudia tena,tatizo unakatsha dozi.
 
Pia ni vizuri kupata uzoefu kwenye jiji la kigali au nairobi.
 
Ndugu mleta mada umeleta mada kwamnajili gani? Mbona mfugaji anamengi juu ya mfugo wake kuliko hats Yale anayasema na kuleta taharuki? Kwani ujuwi baada ya Kabwe kutumbuliwa kuliundwa kikosi kazi kuchunguza ilikuwaje mpaka yakatokea Yale? Na nikwanini Rais alichukua maamuzi magumu ambayo yalileta taharuki? Ukweli Ni kwamba kijana alitimia nafasi vibaya yakuwa karibu na baba akaitumia nafasi hiyo kumtia drip yakutosha ndipo rahisi kwa hasira .

Mambo hili alikuwa sawa maana zipo taratibu zakupeleka issue kwa Rais na sio kutumia nafasi ya ukaribu wako nayeye kupeleka umbea mambo linafanya Rais achukue maamuzi mabaya. Ikumbukwe all issue nzito team tiss pamoja na wataalam ndani ya ikulu wanafanyia uchunguzi ndio anafanya decision. Makonda hats kabla issue haijaisha bado anaendeleza Yale Yale...

Zidhani Kama tunaitaji kumshaur. Wakati fulani Mungu alipokea maombi toka kwa tajiri alie kuwepo motoni na kutokana na uchungu wa moto akamwambia Mungu tafadhali niruhusu nirudi duniani au mtume mtu akawaambie wakuche wew ili wasije huku. Mungu akamwambia wasipo wasikiliza hao hawawezi kuwasikiliza nyie.

Makonda asipo wasikiliza wasio karibu na yeye hawezi kutusikiliza sisi ni swala la muda.......
 




Kwanza ningependa kukupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuliboresha jiji letu hili la Dar. Nimekuwa nikifuatilia juhudi zako tangu ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Naamini jitihada zako za kutaka kuboresha wilaya ya Kinondoni ndizo zilizomfanya Raisi akuongezee majukumu kutokana na kuona jinsi unavyochapa kazi.

Kwa muda sasa nimekuwa nikiona unaibuka kila siku na matamko ambayo baadhi ya matamko hayo hayajafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano suala la ombaomba. Kwa ushauri wangu kabla ya kutoa matamko naomba ufanye utafiti mdogo kwanza na kujiridhisha na kuweka mpango kazi wa namna ya kutatua tatizo kabla ya na kutoa tamko kwamba hutaki jambo fulani katika mkoa wako. Kuna vita vingine hutaviweza zaidi ya kujifedhehesha.

Kwa ushauri wangu naomba uweke vipaumbele katika mambo yafuatayo.

=Kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule zetu

=Kuongeza na kuboresha maabara katika shule zetu

=Kujenga maktaba katika shule na maeneo mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya kata na kuhakikisha kunapatikana huduma za inteneti na magazeti ya kila ziku hapa unaweza kuzishirikisha kata kutenga maeneo kwa ajili ya kujengwa kwa maktaba hizo ili kuhimiza watu kujisomea na kuongeza maarifa na sio kupiga soga vibarazani na kunywa kahawa

=Kuhakikisha jiji linakuwa safi kwa kuweka sheria ndogo ndogo kali zitakazowabana wachafuzi wa mazingira na ili kulitekeleza hili unaweza kupata uzoefu kutoka kwa viongozi wa mji wa Moshi

=Kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutumika hapa jijini na badala yake wenye viwanda hivyo kulazimishwa kuzalisha mifuko ya karatasi kwa ajili ya matumizi au kushirikiana na SIDO kuja na njia mbadala ya mifuko ya karatasi ambapo ubunifu huo unaweza kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya vijana na kina mama..

=Kutengeneza maeneo ya vivutio kwa watalii wanaokuja katika jiji letu kwani wengi hupita tu kwa sababu hakuna vivutio. Hili unaweza kuwashirikisha wabunifu na wakandarasi wetu na kutenga maeneo ambayo yana historia na kuyaboresha kwa kiwango ambacho kitavuta wataalii wengi kutumia siku kadhaa katika jiji letu kwa mfano kama mji mkongwe wa Zanzibar, na Makumbusho ni eneo mojawapo ambalo linaweza kuboreshwea zaidi.

=Kuweka utaratibu mzuri wa boda boda, kwa sasa bodaboda pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar lakini zimekuwa ni chanzo kikuu cha ajali hapa jijini na vijana wengi wamekufa au kupoteza viungo na hivyo kutishia nguvu kazi hapa nchini. Tusipoweka utaratibu na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na madereva kuheshimu sheria za barabarani na kuweka sheria kali kwa watakaokiuka miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na ukosefu wa nguvu kazi.

=Tenga maeneo mengi kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na maeneo haya yakabidhiwe VETA ili vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo wapate fursa nyingine ya kujifunza masomo ya ufundi lakini pia ni vyema kukitengwa maeneo ya mafundi wetu kwa mfano mafundi wa magari kuwe na eneo lao, mafundi seremala wae na maeneo yao kama vile Keko, mafundi wa kuchomea vyuma wawe na maeneo yao ili wenye kuhitaji huduma hizo wawe wanajua zinapatikana wapi na kuondoa hizi vurugu mitaani

=Rejesha viwanja vya michezo vilivyovamiwa na hakikisha swala la viwanja vya michezo linapewa kipaumbele, na michezo isiwe ya aina moja, ongeza wigo wa michezo mbalimbali ili na sisi tuweze kushiriki michezo ya olimpiki.

=Mabango na matangazo yawekewe utaratibu maalum siyo kila mtu akiwa na tangazo lake anapita mitaani na kuchafua kuta za watu itungwe sheria kuondoa tatizo hilo n ahata haya makampuni ya matangazo nayo pia yawekewe utaratibu maalum kuondoa mabango mengi mitaani na kufanya jiji lisionekane nadhifu.

=Wanaohubiri usiku kucha na kelele za mziki kwenye mabaa katika makazi ya watu zipigwe marufuku na kila Pub kama watataka kupiga mziki kwa sauti ya juu basi lazima wawe na ukumbi usioruhu sauti kutoka nje.

=Njoo na njia mbadala ya kuhimiza matumizi ya baiskeli kwa wale wanaofanya kazi maeneo ya karibu na hili litafanikiwa kwa wakandarasi wetu kubuni njia ya waendeshao baiskeli ili kuepuka bughdha kwa watembeao kwa miguu. Mpango huu unaweza kuanza na zile barabara ndefu kama Tegeta mpaka Posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Mbagala mpaka Posta.

Mimi naamini kama ukiweka vipaumbele kwenye mambo hayo machache kati ya mengi ambayo sijayazungumzia utaacha historia katika jiji hili na utakumbukwa na vizazi vijavyo.

Unaweza kuitisha mdahalo kwa wakazi wa jiji hili ili kupitia mdahalo huo uweze kuibua mbinu mbalimbali za kuboresha jiji letu. Naamini wakaazi wa jiji hili hawafurahishwi na hali jinsi ilivyo kwa sasa na wangependa hali iwe nzuri zaidi kwa kuondoa kero nilizozitaja hapo juu, iwapo utawaalika kwenye mdahalo watakupa ushirikiano.

Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako ya kila siku.

Ni mimi Mzee Mtambuzi.
hiki ulichoandika natamani sana makonda ,wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya,meya wote na wenyeviti wa halmashauri wasome ili iwe ni muongozo wao wa mpango kazi.i salute you
 
Awe anasimamia matamko yake.... Alaf kuna vitu havina tija kama kusaka wasio na ajira... Kama anashida ya kujua wasio na kazi ,atuite pale uwanja wa taifa alaf uone kama hataomba poo...
Vp kuhusu ubovu wa barabara za kuingilia vituo vya daladala SIMU2000 na MAKUMBUSHO... ??
 
Back
Top Bottom