Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Kakate tu ticket mkuu sema kuna ambazo ni visa free na zingine ni visa on arrival hapa immigration wa nchi husika watakuchaji kiasi kidogo , but ujiandae kwa maswali tu. mfano utakaa muda gani? shughuli gani imekuleta? Utafikia wapi?
Mkuu, hii visa on arrival ikoje?!
 
Requrements for replacement of lost or stolen Passport


MAHITAJI YA PASIPOTI ILIYOIBIWA/KUPOTEA/KUUNGUA

Ili kupata Pasipoti mpya baada ya ile ya awali kupotea, kuibiwa, kuharibika au kuungua zingatia yafuatayo:-

Taarifa ya Polisi (Police report)

Tangazo la gazeti

Barua ya maelezo inayoeleza kwa kina mazingira ya Pasipoti kuibiwa, kupotea, kuungua au kuharibika. Barua iandikwe kwa:-

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,

Idara ya Uhamiaji,

S.L.P. 512,

DAR ES SALAAM.

Hati ya kiapo kinachoelezea kwa kina mazingira ya kuibiwa, kupotea au kuharibika kwa Pasipoti (Sworn declaration of the circumstance surrounding the LOSS, THEFT OR DAMEGE of Passport).

Kama mazingira yanatokana na kuungua kwa nyumba ama kuvunjwa inahitajika ulete barua ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa kulipotokea tukio hilo na ripoti ya zimamoto kwa wale waliounguliwa na nyumba

Uthibitisho wa safari

Cheti cha kuzaliwa muombaji na cheti/kiapo cha kuzaliwa baba au mama wa mwombaji

Kwa waombaji ambao wamepoteza Pasipoti nje ya nchi anatakiwa alete Shahada ya Dharura (Emergency Travel Document) aliyotumia kuingia nchini

Pamoja na vielelezo hapo juu viambatanishwe na fomu ya maombi ya Pasipoti iliyojazwa vizuri. (Form CT 5(Ai))

NOTE:

Ada ya Pasipoti iliyoibiwa au kupotea ni Tsh. 100,000/= kwa waliopoteza mara ya kwanza, iliyopotea au kuibiwa mara ya pili ada ni Tshs. 200,000/= na malipo kwa Pasipoti iliyoharibika/kuungua ni Tshs. 50,000/=
Sijutii kutumia bando jf, asante mkuu
 
Mkuu ni kweli... Uhamiaji hawatoi passport bila reason.... Nafikiri tungebadili huu utaratibu tuwe kama wenzetu ambao passport kwao ni haki ya msingi na unaweza miliki tu.
na wew usichanganye mada hapa tunaongelea visa
passport kupata haina shida embu changamkeni hata passport hamna? iyo nayo mpaka uambiwe
 
kadi ya kiliniki 5,000/
kadi ya kuzaliwa 30,0000/
Passport express(east africa) 15,000/
Passport 50,000/ ya serikali na 300,000/ ya wasee.
viza uliza wazoefu.

Anyway tanzania kila kitu kinawezekana ila tu uwe na chapaa, kama huna chapaa jamani watanzania wana roho mbaya usipime.

Mkuu okyoma sio WaTanzania wote wana roho mbaya.Nchi yeyeto duniani unahitaji pesa kufanya unayo yataka Ndio maana kwenye biashara kunakitu kinaitwa (cost of doing business) Gharama za kufanya biashara.
Kama passport NI Muhimu kwako inabidi uipate Kwa njia yeyeto Kama nchi yetu Ingekuwa tajiri mshahara mzuri.Unakwenda uhamiaji unapata passport bila ya kutizamani MIKONO.
 
Naisoma kwa mara ya tano hii post yako mkuu. You have a point for real. Binafsi naamini unaweza tuhumiwa na tuhuma zingine nzito zaidi ya hizi, na matusi juu, pamoja na nia njema ulio nayo. I can only guarantee you a lot of disappointment on your way to help us, kama ni picha basi halijaanza hilo ni trela.

But Brother we have come a long way to just give up now, naiona kiu ya kweli kutoka ndani ya moyo wako ya kua msaada kwa watu kama sisi, kamwe usiache kiu yako ikakatizwa na watu wapuuzi tu, tena wepesi mno! tangu uzi huu uanze umekua nuru gizani, kwa sisi tulio na ndoto za kufika ughaibuni kusaka maisha. Umekua honest na role model kwa kila alietembelea hapa. Martin Luther Junior alipingwa hata na blacks wenzie, mitume na manabii wa Mungu waliuwawa na kuteswa sababu ya upendo, wakristo watanikumbusha mahali furani paliandikwa kwamba yesu alifanya mambo mengi sana kiasi kwamba dunia haitoshi kuyaandika na kuyahifadhi, lkn binafsi naamini kazi kubwa aliyoifanya ni pale goligota aliposema Ee Baba wasamehe maana hawajui walitendalo. luther junior alisema pia "It's Only When It's Dark You Can See the Star" Its dark brother and you are one of those shining the stars. Please don't give up now. Just hang on there. nitafanya maombi kwa ajili ako, ile taa ya yenye nuru ang'avu ndani yako ambayo Mungu ameiwasha, kamwe isipungue makali wala isizimwe na mpango wowote wa kishetani. Go Bless you Brother. God Bless us all.

Binafsi nashughulikia issue ya Malta I will do may Best every step nitakua nawaupdate hapa kwa kila hatua though uchumi unasumbua kdg lakini Mungu akipenda this December nitakua nawapa updateas nikiwa Malta.
Mkuu hata mm plan yangu ni Malta, Pasport na nauli ninayo nishauri nitumie njia gani ? kujisajiri workaway ni $ 29 sasa najiuliza wale wanaotaka watu wa volunteering anaweza kunitumia mwaliko?? au tutishia kuchat tu ??? au nitumie njia gani nyepesi ya kupata visa ???? Naomba ushauri wako mkuu
 
Kakate tu ticket mkuu sema kuna ambazo ni visa free na zingine ni visa on arrival hapa immigration wa nchi husika watakuchaji kiasi kidogo , but ujiandae kwa maswali tu. mfano utakaa muda gani? shughuli gani imekuleta? Utafikia wapi?
immagration inchi husika watachaj hela kidogo baada ya kuingia airport yao ????? au hapa hapa bongo kabla ya kuondoka ???? Kuhusu maswali nikisema nimekuja kutembea pia nikaonyesha bank statment yenye salio la kutosha kuna la ziada hapo ???? Naomba mwongozo wako mkuu.
 
Back
Top Bottom