Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Maisha ni popote sikatai.

Ila kwa ITALY nisingekushauri.

Na tukija kwenye Ubaguzi kwa hapa Ulimwenguni bora kuondoa hiyo dhana maana kila Nchi ina Ubaguzi ila Ubaguzi unatofautiana.

Kwahiyo suala la Ubaguzi lisikutishe
Mbn Hussein Machozi kalowea Italy anakula bata ...hahaha
 
Wadau mm kipindi sijaoa nilikuwa na ndoto za kuishi ulaya lakini sasa nimeoa naona ndoto zangu kama zinafifia hivi.
Hapana mkuu mbona unakata tamaa?
Tena kama umeoa utakua makini zaidi ili kutimiza ndoto,pia ata elimu kwa watoto wako inakua poa sana ukifika abroad na familia.
 
Wakuu unaposhiriki dv lottery visa ni lazima uwe na paspoti?
Passport ni lazima uwe nayo.
DV2019(diversity visa lottery) inaanza rasmi
October 03 mpaka November 7th 2017
www.travel.state.gov
Hii program ni BURE ukiulizwa pesa kimbia.
.GOV ni ya serikali.
Uwe makini wakati unajaza hizo forms (ukiweza ziandike kwenye daftari) maana maswali uliyo yajibu utaulizwa tena.
Kila la kheri
 


CC: impelle .

-Kaveli-
 
Aise mimi natamani sana kwenda huko ili nikasome, masomo ya uzamili na nikipata baada ya masomo nijilipuwe kama unavyosema.....



Basi sasa kwa kuwa wewe unauzoefu , mimi binafsi sinauzoefu ila nina passport ...


Please tushare skolaship za masomo ya uzamili zinazo husiana na Economics, public policy na nyinginezo labda zinaweza kutupa mwanga wa kutoboa


Nimelipenda sana wazoo lako kweli linafunguwa machooo na roho kama unania ya kupata exposure ....na kutafuta maisha
 
Nimeipenda boss please , mimi passport ninao ninachohitaji ni allowable basi, please tushare bas hizo kama huwa unaziona ili tujilipuwe
 
Mkuu, mwaka huu nimeomba scholarship kwenda kusoma Australia, China na UK
Niombeeni nifanikiwe ,nijilipue huko, nafanya kaxi ila haina maslahi na wategemezi lukuki, bora nitokomee huko kwanza
Nilifanikiwa ndugu zangu
Mungu awabariki nanyi mfanikiwe
Kama kuna mtu atataka muongozo Kwa ajili ya kujiunga masters na PhD huku nilipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…