acha nijibu na hapa itawasaidia na wengine pia na wenye kujua zaidi wataongezea.
kwanza, unapotoka Tanzania kwenda nchi fulani aidha tuseme Dubai jua unaenda kufanya nini. Na hicho unachoenda kukifanya hakikisha kwa research yako kweli kinafanyika huko na kitaweza kukupatia kilichokutoa bongo na kwenda huko.
kwanini nasema hivi.. mfano vijana wengi wamekuwa wakiambiwa South Afrika ukifika tu kazi bwerere unapiga lakini uhalisia South sio kurahisi na mwisho wanaishia kuwa wakabaji. hivyo unapotoka bongo na kwenda nchi yoyote jua unachoenda kukifanya na dadisi kama kweli kipo na utaweza kupata hiyo kazi ASAP.
pili, Awepo mwenyeji wako atakayekupa miongozo na namna ya kufanikisha kilichokupeleka. nitawatolea mfano. kuna mtu namjua alitoka bongo akaenda Dubai alipofika akapokelewa na Mtanzania wanaofahamiana tu lakini hakuwa na ufahamu kama ataenda huko. kilichofuatia ni huyo mwenyeji wa jamaa kum-frustrate jamaa kwa lawama na vijembe kibao mwisho jamaa aliamua kurudi Tz.
Watu wanaoishi nje wengi mioyo yao ilishabadilika kutokana na aina ya maisha wanaoishi usifikiri kutoka bongo kwenda kwa mtu Germany ni sawa na unavyoenda kwa shangazi Mbeya. otherwise jipange kifedha uwe umejitosheleza hakuna atakayekataa kukupokea.
Nne, Viza sio guarrantee ya kukubaliwa kuingia nchi ya watu, unaweza kuwa nayo ukafika border ukarudishwa. jipnge mapema kama ni visit nani anakupokea, utalala hotel gani, gharama nani anagharamia na ni kiasi gani vyote unatakiwa uvijue. wakiona haueleweki unarudishwa kwenu.
hapa kwenye viza kuna swali niende na viza ipi ili nipate kazi?
Viza zipo za aina nyingi kutokana na nchi. ila kwa ujumla niseme kujilipua kwa kuzamia melini siku hizi hakupo.
siku hizi watu wanachofanya anaomba aingie tu nchini mwa watu kihalali kisha anapotelea huko harudi... wanasema unaweka pass uvunguni.
hivyo unaweza kuomba visit au kuhudhuria conference let say Sweden ukishaingia huendi kwenye conference unaingia mtaani. ukikamatwa mtajuana na aliyekukamata.
viza nzuri ni Student.. hii unaruhusiwa kufanya kazi.
unaweza pia kutafuta demu ukapewa spouse.. hii utapewa permit ya kuishi kwanza lakini inaprocess ndefu hadi upewe wamejiridhisha kwanza kweli ni mpenzi wako au ni mkeo. na unaweza kuwa nayo na hauruhusiwi kufanya kazi.
mambo ni mengi saana....
NB: Yote ya yote kuanalyze analyze mambo kuna vhelewesha. wewe unataka kutoka bongo.. tafuta nauli apply viza beba pesa yako ya matumizi lala mbele yatakayotokea mbele utapambana nayo.
kikubwa zingatia tu nchi ya kwenda usije ukaruka maji ukakanyaga pupu.