Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Kwa Japan, njia rahisi ni kwa ndoa. Watu hawaoani huku wala kuzaliana. Wanigeria wanaoa kila siku na Wajapani.

Kwa kusoma hapa, mpaka uletwe na serikali. Scholarship wanatoa kuanzia Ph.D level.

Unaweza kuja kwa kusoma Kijapani. Naifahamu shule moja ya lugha, gharama ni $1000 kwa mwezi. Wachina wanakuja hivo na kutafuta maisha wakiingia. Pia, viza hazina tabu za kuishi. Unaweza kusoma hapo kwa $500, na $500 unalipa chumba katika dorm yao. Pia, viza yako ya mwaka unaruhusiwa kufanya kazi na shule ina contact na makampuni. Baada ya hapo, akili kichwani.

Maisha ya Japan sio ghali kama unavyosoma katika magazeti. Unaweza kula kwa $10 kwa siku na kushiba. Kazi zipo nyingi tu, viwandani wanatafuta wafanyakazi, Wajapani hawazitaki na hawataki kuzaa. Kama ukitaka, nimeweka link ya vyumba vya kulala vya $500 kwa mwezi kutoka kwa agent. Unaishi kigeto, katika chumba kimoja, katikati ya jiji la Tokyo. Mgeni yoyote anakaribishwa.

Shule ya Kijapani: 東京近郊埼玉県さいたま市の日本語学校

Chumba Tokyo: www.realestate.co.jp
Shukran mkuu, nimejaribu kucheki hii shule,naona monthly fees inalipwa na wale ambao tayari wanaishi ndani ya japani,ila cha kutia moyo wanasema unaweza kwenda kwa tourist visa ukifika kule unaswit to student visa, ushauri wenu please lusungo izzo Tokyo40
 
Mkuu,
Serikali ya Japan ina ubaguzi sana kwa Waafrika. Kuna baadhi ya nchi tu ndio wanaruhusu raia wao kubadili tourist viza to student visa. Wanawapendelea zaidi raia wa nchi masikini wa Asia vile vile inapikuja kutoa scholarship za vyuo kuanzia Bachelor's. Waafrika mara nyingi wanapewa kuanzia Doctorate unless umetokea serikalini.

Ushauri wangu ni kuomba student visa kutoka Dar moja kwa moja. Lakini uwe tayari kujibu maswali. Uwe na sababu muhimu ya kutaka kusoma Kijapani kwa mfano kuwaelewa watalii wao zaidi au kujitayarisha kufanya kazi inayohitaji hio lugha.

Good luck.
 
Kama Mtanzania, ubalozi wa Japan utategemea uonyeshe una uwezo wa kulipa kwa mwaka pamoja na gharama za kuishi kabla ya kupewa viza ya mwanafunzi.

Kwa hesabu za haraka ni kama US$12000.
 
Mkuu Tokyo40 ulipotea sana, karibu tena.
 
Uzi huu umekuwa na unaendelea kuwa msaada kwa vijana wengi..big up kwa muasisi na wachangiaji wote.
 
Kama Mtanzania, ubalozi wa Japan utategemea uonyeshe una uwezo wa kulipa kwa mwaka pamoja na gharama za kuishi kabla ya kupewa viza ya mwanafunzi.

Kwa hesabu za haraka ni kama US$12000.
shukran kwa mchango wako mkuu, bado naangalia options hapa either language or masters route,still researching......
 
Ukiwa tayari niambie.... Nitakupa namba ya kijana atamaliza yote ndani ya siku 2. Hiyo gharama haitofika.
Mimi nahitaji ndugu yangu niandae kiasi gani....? Ila Sina Nia ya kusafiri nataka tu kumiliki passports
 
Jamani msaada nimepewa invitation Na shirika la dini marekani mwezi September Na barua nimepewa ya kuombea visa ila upande wa nauli nauli sjajipanga Na sijajua gharama zikoje Na usawa uliopo kwakweli nashindwa cha kuwajibu
Jiandae kumconvice consular kwamba ukienda marekani utarudi, otherwise unapigwa chini.

Viza ya Marekani kwa watu wenye shughuri za hapa na pale ni mtihani.

Kikubwa ni commitment na bond uliyonayo Tanzania ndio kigezo pekee kikubwa cha kupata US Viza.
 
Kaka Izzo mimi nilikuwa naomba msaada nipate mtu wa kunipa barua ya mwaliko kwenda usa,kule nina mtu wangu ambae awezi kunipa mwaliko kwa sababu tofauti so kanipa nafasi nipate mtu wa kunipa mwaliko kisha nikienda nitafika kwa mtu wangu msaada wako plz
Huna mtu huko usijidanganye, hata ukifanikiwa kupata Viza ukifika airport atakuzimia simu.

Jipange tafuta connection upya, nakuonya huna rafiki hapo huyo amekutosa kiaina.

Mimi naweza kukusaidia mwaliko lakini huyo jamaa yako ni mnafki jipange upya usiende kuteseka, changamoto za kukosa mwenyeji mwenye upendo wa dhati nazijuwa unaweza kwenda na ukageuza mwenyewe bila kupenda.
 
SASA JAMANI HEBU FANYA HIVII MAAANA NAONA UZI NI MREFU NA KUSOMA HADI UMALIZE NI KAZI

KAMA UKIONA COMMENT HII pLZ REPLY (Quote) NCHI UNAYO PENDEKEZA MTU KWENDA AU MTU KUTO KWENDA ILI TUJUE NCHI GANI NI NZURI KWA MAISHA YA MTANZANIA AU MABAYA YA MTANZANIA AU NA SEHEMU AU NCHI ZENYE BATA SAFI AMBAYO MTANZANIA ANA WEZA KU ENJOY.

kwa wenye uelewa tu. mimi nimependa scandnavia
Umeharibu maaana nahata uandishii wako ni mbovu
 
Mimi ni mmojawapo wa watu waliofidika na huu uzi kwa msaada mkubwa wa lusungo na izzo.

uliwekwa kipindi nipo katikati ya mipango yangu nami nikaufanyia kazi.

Vikwazo na changamoto ni nyingi saana ila kama umenuiya kufanya ulitakalo hutaona kama ni changamoto. nitaendelea....
uko nchi gani mkuu, watu wakutumie kama daraja
 
Huna mtu huko usijidanganye, hata ukifanikiwa kupata Viza ukifika airport atakuzimia simu.

Jipange tafuta connection upya, nakuonya huna rafiki hapo huyo amekutosa kiaina.

Mimi naweza kukusaidia mwaliko lakini huyo jamaa yako ni mnafki jipange upya usiende kuteseka, changamoto za kukosa mwenyeji mwenye upendo wa dhati nazijuwa unaweza kwenda na ukageuza mwenyewe bila kupenda.
Ubarikiwe sana komredi Matola unawapa mwanga wengi sana!
 
Back
Top Bottom