Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Sawa
Unaweza kutafuta/kutumia sababu nyingine tu Mkuu, kama utalii,biashara,michezo,dini nk,ilimradi ukidhi vigezo katika category husika,ilimradi umepata tu!!.View attachment 777301
Sawa mkuu nmekupata,,sasa nikijaza biashara na ntkappenda hapo uhamiaji vipi upande wa maswali..na je sehemu ya kujaza namba ya nyumba inakuje na hapa napoishi hakuna namba.
 
Sawa

Sawa mkuu nmekupata,,sasa nikijaza biashara na ntkappenda hapo uhamiaji vipi upande wa maswali..na je sehemu ya kujaza namba ya nyumba inakuje na hapa napoishi hakuna namba.
Kuhusu maswali inategemea Mkuu sometimes wanaweza kuuliza maswali au usiulizwe kabisa,ila ni maswali ya kawaida tu,na yanajibika kikubwa confidence Mkuu,namba ya nyumba sio lazima ujaze ni option tu,mimi sikujaza na ila nilipata.
 
Nchi nzuri ya kwenda kuishi baada ya Tanzania ni Yemen, Somalia, Syria. Unashauriwa kwenda na mabomu ya kujilipua tu.
 
Mimi ni mmojawapo wa watu waliofidika na huu uzi kwa msaada mkubwa wa lusungo na izzo.

uliwekwa kipindi nipo katikati ya mipango yangu nami nikaufanyia kazi.

Vikwazo na changamoto ni nyingi saana ila kama umenuiya kufanya ulitakalo hutaona kama ni changamoto. nitaendelea....
 
 
Naamini ni wakati sasa wa Daby uukamwaga mrejesho hapa kama kuna hatua umepiga mkuu, hii itawapa wadau wengine nguvu ya kusonga mbele..hakika ulikuwa mchangiaji mzuri sana wa uzi huu.
 
Nakumbuka mkuu
 
Nakumbuka mkuu
Mzee baba huwa nikiulizwa mrejesho nashindwa nianzie wapi. naona kama nitaanika maisha yangu hapa.

labda uniulize maswali nitaweza kukujibu.

ninachoweza kusema tu Huu uzi ulinisaidia na lusungo izzo wengineo kwa maelekezo ya nje nyuma ya keyboard yalinisaidia pia.

tulianzisha hadi group nje ya uwanja sema wengi wetu tuna fantasy na kuongea saana ila kuendelea mbele kutenda ni wagumu.


Naamini ni wakati sasa wa Daby uukamwaga mrejesho hapa kama kuna hatua umepiga mkuu, hii itawapa wadau wengine nguvu ya kusonga mbele..hakika ulikuwa mchangiaji mzuri sana wa uzi huu.
 
Hongera sana mkuu... kama ulifika kile kiwanja karibu Copenhagen
 
umeshaenda wewe?


Niende huko kutafuta nini wakati naishi mbinguni hapa Tanzania. Kuna watanzania ma-alosto wanaona Somalia, Yemen, na sehemu zingine za kujilipua mabomu zina raha zaidi ya hapa Bongo na ndiyo maana nimewashauri waende huko ili watuachie nchi yetu.
 
acha nijibu na hapa itawasaidia na wengine pia na wenye kujua zaidi wataongezea.

kwanza, unapotoka Tanzania kwenda nchi fulani aidha tuseme Dubai jua unaenda kufanya nini. Na hicho unachoenda kukifanya hakikisha kwa research yako kweli kinafanyika huko na kitaweza kukupatia kilichokutoa bongo na kwenda huko.

kwanini nasema hivi.. mfano vijana wengi wamekuwa wakiambiwa South Afrika ukifika tu kazi bwerere unapiga lakini uhalisia South sio kurahisi na mwisho wanaishia kuwa wakabaji. hivyo unapotoka bongo na kwenda nchi yoyote jua unachoenda kukifanya na dadisi kama kweli kipo na utaweza kupata hiyo kazi ASAP.

pili, Awepo mwenyeji wako atakayekupa miongozo na namna ya kufanikisha kilichokupeleka. nitawatolea mfano. kuna mtu namjua alitoka bongo akaenda Dubai alipofika akapokelewa na Mtanzania wanaofahamiana tu lakini hakuwa na ufahamu kama ataenda huko. kilichofuatia ni huyo mwenyeji wa jamaa kum-frustrate jamaa kwa lawama na vijembe kibao mwisho jamaa aliamua kurudi Tz.

Watu wanaoishi nje wengi mioyo yao ilishabadilika kutokana na aina ya maisha wanaoishi usifikiri kutoka bongo kwenda kwa mtu Germany ni sawa na unavyoenda kwa shangazi Mbeya. otherwise jipange kifedha uwe umejitosheleza hakuna atakayekataa kukupokea.

Nne, Viza sio guarrantee ya kukubaliwa kuingia nchi ya watu, unaweza kuwa nayo ukafika border ukarudishwa. jipnge mapema kama ni visit nani anakupokea, utalala hotel gani, gharama nani anagharamia na ni kiasi gani vyote unatakiwa uvijue. wakiona haueleweki unarudishwa kwenu.

hapa kwenye viza kuna swali niende na viza ipi ili nipate kazi?

Viza zipo za aina nyingi kutokana na nchi. ila kwa ujumla niseme kujilipua kwa kuzamia melini siku hizi hakupo.

siku hizi watu wanachofanya anaomba aingie tu nchini mwa watu kihalali kisha anapotelea huko harudi... wanasema unaweka pass uvunguni.

hivyo unaweza kuomba visit au kuhudhuria conference let say Sweden ukishaingia huendi kwenye conference unaingia mtaani. ukikamatwa mtajuana na aliyekukamata.

viza nzuri ni Student.. hii unaruhusiwa kufanya kazi.

unaweza pia kutafuta demu ukapewa spouse.. hii utapewa permit ya kuishi kwanza lakini inaprocess ndefu hadi upewe wamejiridhisha kwanza kweli ni mpenzi wako au ni mkeo. na unaweza kuwa nayo na hauruhusiwi kufanya kazi.

mambo ni mengi saana....


NB: Yote ya yote kuanalyze analyze mambo kuna vhelewesha. wewe unataka kutoka bongo.. tafuta nauli apply viza beba pesa yako ya matumizi lala mbele yatakayotokea mbele utapambana nayo.

kikubwa zingatia tu nchi ya kwenda usije ukaruka maji ukakanyaga pupu.
 


Mwakani when you ready, nitafute nikuchangie $200
 
Njoo upambane na maisha! Acha uoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…