Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Shukran mkuu, nimejaribu kucheki hii shule,naona monthly fees inalipwa na wale ambao tayari wanaishi ndani ya japani,ila cha kutia moyo wanasema unaweza kwenda kwa tourist visa ukifika kule unaswit to student visa, ushauri wenu please lusungo izzo Tokyo40
 
Mkuu,
Serikali ya Japan ina ubaguzi sana kwa Waafrika. Kuna baadhi ya nchi tu ndio wanaruhusu raia wao kubadili tourist viza to student visa. Wanawapendelea zaidi raia wa nchi masikini wa Asia vile vile inapikuja kutoa scholarship za vyuo kuanzia Bachelor's. Waafrika mara nyingi wanapewa kuanzia Doctorate unless umetokea serikalini.

Ushauri wangu ni kuomba student visa kutoka Dar moja kwa moja. Lakini uwe tayari kujibu maswali. Uwe na sababu muhimu ya kutaka kusoma Kijapani kwa mfano kuwaelewa watalii wao zaidi au kujitayarisha kufanya kazi inayohitaji hio lugha.

Good luck.
 
Kama Mtanzania, ubalozi wa Japan utategemea uonyeshe una uwezo wa kulipa kwa mwaka pamoja na gharama za kuishi kabla ya kupewa viza ya mwanafunzi.

Kwa hesabu za haraka ni kama US$12000.
 
Mkuu Tokyo40 ulipotea sana, karibu tena.
 
Uzi huu umekuwa na unaendelea kuwa msaada kwa vijana wengi..big up kwa muasisi na wachangiaji wote.
 
Kama Mtanzania, ubalozi wa Japan utategemea uonyeshe una uwezo wa kulipa kwa mwaka pamoja na gharama za kuishi kabla ya kupewa viza ya mwanafunzi.

Kwa hesabu za haraka ni kama US$12000.
shukran kwa mchango wako mkuu, bado naangalia options hapa either language or masters route,still researching......
 
Ukiwa tayari niambie.... Nitakupa namba ya kijana atamaliza yote ndani ya siku 2. Hiyo gharama haitofika.
Mimi nahitaji ndugu yangu niandae kiasi gani....? Ila Sina Nia ya kusafiri nataka tu kumiliki passports
 
Jamani msaada nimepewa invitation Na shirika la dini marekani mwezi September Na barua nimepewa ya kuombea visa ila upande wa nauli nauli sjajipanga Na sijajua gharama zikoje Na usawa uliopo kwakweli nashindwa cha kuwajibu
Jiandae kumconvice consular kwamba ukienda marekani utarudi, otherwise unapigwa chini.

Viza ya Marekani kwa watu wenye shughuri za hapa na pale ni mtihani.

Kikubwa ni commitment na bond uliyonayo Tanzania ndio kigezo pekee kikubwa cha kupata US Viza.
 
Huna mtu huko usijidanganye, hata ukifanikiwa kupata Viza ukifika airport atakuzimia simu.

Jipange tafuta connection upya, nakuonya huna rafiki hapo huyo amekutosa kiaina.

Mimi naweza kukusaidia mwaliko lakini huyo jamaa yako ni mnafki jipange upya usiende kuteseka, changamoto za kukosa mwenyeji mwenye upendo wa dhati nazijuwa unaweza kwenda na ukageuza mwenyewe bila kupenda.
 
Umeharibu maaana nahata uandishii wako ni mbovu
 
uko nchi gani mkuu, watu wakutumie kama daraja
 
Ubarikiwe sana komredi Matola unawapa mwanga wengi sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…