Huu uzi ni mzuri maana utasaidia wenzetu pia kimawazo na kifikra pia,mtu anaweza kujua wapi pa kuanzia Kama akitaka kusafiri,sema me naanza na hapo kwenye faida ulizopata,ni kweli faida ni nyingi sana ukitofautisha na bongo,lakin kaka sijaelewa kitu,umesema umeishi miaka 8 na umeweza kujenga ghorofa bongo na mashine,sasa me najiuliza mbona miaka 8 midogo sana??uliwezaje??au ulikuwa hauli vizuri??ulikuwa unajibana sana au ulikuwa unaishi nje ya mji(maana huko ndo kila kitu kinakuwaga poa,tofauti capital city au capital ya uchumi)???
Swali langu la 2,Kujilipua,sijaelewa kidogo hapo,unazungumzia kujilipua kWa aina gani??maana zipo nyingi sana,mfano kuna kujilipua kwa kujipa uraia wa nchi zenye vita ili kuomba hifadhi(mfano wa nchi,Somalia(watoto wa kinzanzibar wanajilipua sana na kujipa uraia wa kisomali,Eritrea,Africa ya Kati,Sudan n.k),au kujilipua pia kWa kuchana passport kWa ajili ya kuomba hifadhi Kama mtu ambaye hana uraia wa nchi yeyote ile,hiyo ni mifano tu na kuna wengine wanaweza ongezea,sasa kaka wewe unazungumzia ipi hapo??maana kutafuta mke mzungu kuoa na kupata karatasi,hiyo siyo kujilipua(mawazo yangu).
Kingine kwenye changamoto,naweza ongezea hali ya hewa maana sisi wengi tushazoea joto au jua kWa mwaka mzima lakin wenzetu kuna baridi sana baadhi ya miezi na kuna joto kWa miezi 4 tu katika mwaka,changamoto nyingine inaweza ikawa karatasi mfano Europe kila unachokifanya inabidi ufanye photocopy,unabaki na original unatoa copy na katika kila kitu utakachofanya na wakati kwetu siyo hivyo,wengine wanaweza ongezea.
La mwisho naweza ongezea pia hapo jinsi ya kwenda,unaweza pia kwenda nchi yeyote ya Europe kWa kisingizio cha kutaka kusoma lugha yao,kWa mfano ujeruman,unaweza ukatafuta chuo au center yoyote ambayo hipo ujeruman ambayo inajulikana na serikali ya ujeruman na ambayo inaweza kukualika kWa ajili ya masomo ya lugha yao ya Dutch,hao jamaa wakishakubali uwa wanakutumia barua ambayo inaonyesha ushajiandikisha katika chuo chao kWa ajili ya kwenda kusomea lugha,hiyo barua wanatuma pia ubalozi wa ujeruman Dar,so ukienda pale wanaweza kukupa visa ya kusoma,inaweza ikawa ya mwaka na ukawa unaruhusiwa kufanya kazi labda kWa masaa 20 kwa week(kihalali)na kuweza pia kufanya kazi masaa mengi zaidi ya hayo,ukapata sana mpunga lakini isiwe kazi ya kihalali,nikimaanisha black work(watu walioishi Ulaya na USA wanaelewa naongelea nini),baada ya hiyo visa unaweza omba card ya kuendelea kusoma kWa mwaka wa pili au unaweza mpata mtu mwenye uraia au resident permit akakuoa na maisha yakaendelea au ukapata kazi ya kudumu na ukaweza badilisha status kutoka kwenye uwanafunzi na kuwa na status Kama mfanyakaz,hapa wanaweza kukupa kabisa resident permit ukaweza kuvuta na ndugu zako wengine kupitia mgongo wako.
Jingine unaweza tafuta mtu mwenye uraia wa Ulaya au USA ukaongea naye,ukampa pesa mnafunga ndoa ya uongo,yeye anasimamia kila kitu mpaka unapata permit yako halafu anafanya divorce lakin anakuacha na permit yako,nafikiri wengine watakuja kuongezea,sema kaka naomba unijibu hilo swali langu hapo juu kuhusu kujilipua.
Shukrani sana[emoji1317]