Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Hivo vikundi wanazichangamkia wanaijeria Na wakenya mfano kupitia ubalozini mfano via Belgium embassy Dar Kuna BTC uwa wanatoa scholarship though Kuna ukiritimba adui wa mbongo ni mbongo mwenzake so ukitegemea ubalozini Kuna urasimu kibao .
Kweli mkuu... Uliahidi kurudi kutoa nondo... Karibu....
 
Then si wote wapendao kuukana uraia wao... Watu wanaenda saka fursa tu.... Leo sweden au DK ukipata long stay visa unakula mema ya nchi alimradi ujue lugha tu
Lugha imekuwa ni tatizo sana kwa nchi hizo
 
Kweli mkuu... Uliahidi kurudi kutoa nondo... Karibu....
Ni kweli mkuu wakati naingia Sweden niliingia kwa lengo la kusoma via scholarship ya shirika fulani lengo lilikuwa Ni after three years nitarudi Bongo kuendelea na mambo mengine according to their principles kumbuka by then nilikuwa nimefukuzwa Chuo na sikuwa na hili wala lile but uncle wangu alinichomeka katika hiyo chance wakati naendelea na masomo nilimpata rafiki wa kike Swedish ambaye tulijaliwa kupata mtoto then ikawa nimepewa uraia wa Sweden ila uraia wa Bongo sijaukana bado but nilichofurahi Ni kwamba Sweden Kuna watanzania wengi Sana I'm feeling like I am in Tabata.
 

Una dual citizenship yaTanzania na Sweden?
 
Ninawajua wemgi tu waloanzia Sweden baada ya kupata kibali wakahamia DK....

Ok maisha ya hapa ulaya yaani siri kubwa saana wengi hawasemi ukweli,na kupata karatasi sio Kwamba ndio ticket ya kwenda Europe union countries na kufanya kazi kuna kitu inaitwa personal number kila nchi ina yake,pia watu kibao wa karatasi za Italy lkn hawapewi kazi Scandinavia,mpk uwe na contract ya kazi,nani sasa anakupa hiyo contract ya kazi?kuna kampuni moja tu inatoa contact nayo ni kusambaza mataganzo hapa wanaita REKLAM.hiyo kazi hailipi hata kidogo ni bora ubaki bongo uuze nyanya.
 
Sasa watu wanakwenda ULAYA au America kujilipua...ushasikia MTU amejilipua China?au Vietnam?

Mkuu Mwandende
kama baharia wa miaka hiyo unaonekana umefika karibu continents zote na nchi karibu zote.
Hebu tufahamishe maisha in general kule Italy na Greece. Kuna fursa gani?
Maana kuna jamaa zangu wengi wamekaa huko since 1980s wamepewa permits lakini mzungu kagoma kuwapa passports
 
Kwahyo mkuu nikifika majuu naweza kuhamisha mkwanja kutoka akaunti yangu ya NMB kwenda akaunti ya nchi niliyoenda?
Je utaratibu ukoje?
Je nikiwa na mastercard si natoa pesa benki yoyote dunia nzima?
Inawezekana kabisa. Ilimradi kadi yako ni mastercard, unaweza kutoa hela popote duniani. unazama kwenye ATM na kutoa hela kama kawaida. Ila kama una foreign account, unaweza instruct bank itume kiasi kadhaa kutoka kwenye account yako na kwenda kwenye account ya Ndugu uliowaacha home. kwa technlogy ya leo, hata wewe unaweza fanya hivo kwa sekunde chache tu...
 
Alaf passport. Nilipoona masuala ya cheti cha kuzaliwa cha mzazi.hapo ndo nilichoka.sasa tunafanyaje kuipata.ya 50,000.ila naomba usiwe kama britanicca tu. 😀 😀 😀 😀 😀 😀
Mkuu hapo unatengeneza hata ya kiapo inaitwa affidavit... Unapiga muhuri wa mahakama kwisha habari... Hii hati ni ipo form of paper yaan una type like Bibi yko au babu yako ana thibitisha Kuwa alimzaa mama ako au baba ako tarh flan na Mwaka flan...then Jina lake chini na sahihi then una gonga muhuri wa mahakama basi umemaliza.
 
Affidavit
 
Hizo website ni zipi tutajiee
 
Na jina la bwana lihimidiwe....sema amen Prof
 
Karibu kwa michango, mawazo na ushauri mkuu.

Miaka hiyo ya zamani jirani yetu mmoja alifanya hii daring and most adventurous journey to Denmark kama ifuatavyo:
Jamaa alipanda basi from Dar to Nairobi miaka hiyo stendi ya mabasi ya Arusha ilikuwa Kisutu. Alibeba mfuko wa rambo akiwa na nguo chache na mswaki.
Alipofika Nairobi akachukua basi hadi Uganda. From Uganda akapata lifti ya lori la mizigo hadi Juba.
Kutoka Juba akaungaunga Safari hadi Khartoum na hatimae akaingia Cairo, Egypt. After a few days akaenda Port Said. Baada ya wiki kadhaa akapata jahazi from Port Said hadi Syria.
Akaishi Syria for several months akipiga dei waka na finally akapata mchongo wa kuingia Turkey.
Alikaa Turkey for 3 years akapata mchongo wa kuingia Denmark ambako alioa huko na ana Danish wife na familia ya watoto 3. Alijiendeleza kielimu na ana kazi nzuri tu na maisha mazuri
Hutembelea bongo once in 2 years na alisema atafia huko

Pengine kwa wale wapiganaji mnaweza kujifunza kitu hapa
Asanteni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…