Haha, mkuu Richard umenifurahisha hapo pa kuwa mweusi kama M Sudan ili upate uraia. Wengine wanadharau sana hiyo rangi kumbe inaweza kuwa the best kwa uhamiaji...lol
Lakini hili suala la refugees limekuwa pia gumu sasa worldwide, it's not that easy anymore. Hayo mashinikizo yanayowekwa sasa against refugees, from Brexit, to America first, to...God knows chaguzi zijazo za France and German kama zina muelekeo huo pia. It's mayhem.
Baadhi ya nchi kibano kwa wanaojilipua/wakimbizi pia kimekuwa kikali sana, na haijalishi ni mkimbizi wa vita, njaa au majanga ya dunia.
I don't think it was this strict before, lakini siku hizi naona watu wanavalishwa bracelets wakati cases zinaendelea, and once they're under the radar, they're not at peace.
Immigration officers walikuwa wanawa visit at least once per week, lakini sasa naona kuna watu wanatakiwa kupiga simu ku report every single day. Na uki miss kihama. Imagine huyo ni mkimbizi na familia, na huko alikotoka ni kihama pia.
Nimetumia mfano huo wa MSudan kwasababu kuna kijana wa kutoka Sudan ambae aliamua liwalo na liwe na akaingia ndani ya njia ya reli ya Channel Tunnel (kama sikosei) ili atembee na atokee pale Ash ambacho ni kijiji kilichopo maili tatu kutoka Dover.
Polisi walimsubiri na alitumia masaa zaidi ya 24 kuja kutoka lakini alikuwa tayari yupo ndani ya ardhi ya UK na akajisalimisha akajieleza na akakubaliwa maombi yake ya Ukimbizi hapohapo na akaelekea kwenye nyumba za muda.
Sasa huyu alikuwa ni msudan na wanajulikana hivyo haikuwa kazi ngumu kukaa na kusikiliza kesi yake.
Ila bado mfumo wa kupokea Asylum cases upo na ukipita hapo kwenye (Asylum claim) ndiyo baadae unaingia hatua ya kupewa hadhi ya ukimbizi na baadae mkazi ya kudumu.
Hatua ngumu ni hiyo ya kujilipua yaani asylum seeking ambayo huenda ukawekwa kizuizini (detention) au ukiwa na bahati unawekwa kwenye nyumba maalum wakati kesi yako inachunguzwa, hapo unakuwa unatakiwa kuwa unakwenda kusaini kila mwezi au kila wiki kwenye kituo cha uhamiaji kilichopo karibu.
Pia kwenye hatua hii ya kujilipua unakuwa huruhusiwi kufanya kazi na unakuwa uko kama kifungoni vile.
Kuna aina mbili za kukubaliwa kesi yako yaani unakuwa unapewa ukaazi wa kudumu uitwao "humanitarian protection" kwamba kwa huruma ya wewe kupatwa na maswahibu yalokukuta basi ni uamuzi wa busara kukulinda na kukusaidia kwa muda na hiyo unaweza kupewa miaka 3 au 5 ambayo baadae inaweza kuongezwa au unaweza kurudishwa kweu kutokana na hali ya nchi ulikotoka kuwa shwari. hii mara nyingi hupewa watoto walo chini ya miaka 18.
Aina ya pili ni ile iitwayo "Refugee Status" ambayo unaweza kupewa ya muda mfupi inayoweza kuangaliwa upya au ya muda mrefu ambayo hupelekea mkimbizi kuwa raia wa nchi hiyo.
Ukikubaliwa kesi yako ndiyo unapewa hadhi ya ukimbizi au refugee status na unakuwa unaruhusiwa kufanya kazi, kwenda shule na kadhalika ili uweze kuzoea zaidi mazingira ya nchi yako mpya.
Ila kama unavyosema kesi nyingi za ukimbizi zilikuwa kati ya 2000 hadi 2008 na baaada ya hapo zimekuwa ni ngumu sana kufanikiwa khasa kama hazitokei kwenye nchi kama Eritrea, Syria, na Sudan.
Ila bado waafrika wanakwenda na kujaribu si tu Marekani bali hata katika nchi kama Canada, Uingereza, Italy, Ujerumani, Sweden, Denmark na Holland.
Ukiondoa Uingereza nchi za Italy, Ujerumani, Sweden, Holland, Denmark wao wanataka uwe tayari kujifunza lugha zao ikiwa ni moja ya masharti ya kupewa uraia kabisa.