Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza


I always underpin your posts. I always pay homage to your school of thoughts.

Mkuu Lizarazu, stay always blessed.

-Kaveli-
 
Bibi mzaa mama yupo.sasa nikifika kurasini nisemeje.
 
Naomba kujuzwa , mfano ukiwa na tourist visa ya france inatakiwa ufanye booking hotel ya kufikia sasa hapo kwenye kufanya booking n lazma ubook cku zote utakazo kaa au?

Chukua shengena viza kisha book hotel hata kwa siku tano unalipa kwa kadi ya viza ila hawakati pesa kisha tafuta booking ya ndenge lazima ukate insuarance pia uwe na bank statement sasa sijui kama na tz wanatumia utaratibu huo maana mimi niliombea kwa nchi ninayoishi huku nje ya nchi mimi nilikwenda tu kutembea haikuwa tabu kabisa ukisha pata viza unacansel booking yako ya hotel ila unakuwa na ile copy ikusaidie kuingia kama wakikuuliza ukifika huko utajua ila france maisha ni magumu kidogo
 
Uzi mzuri sana. Ila nina angalizo moja: siasa za Ulaya na Marekani zinabadilika kwa kasi sana siku hizi. Vyama vyenye mrengo wa kulia ndivyo vinazidi kushika madaraka. Vyama hivi vina itikadi za ki-nationalist, ki-racist, ki-conservative n.k. Havipendi wageni kwenye nchi zao; na havipendi kutoa misaada kwa nchi maskini. Hivyo ni vyema kuelewa hili pia katika mipango yetu ya kujilipua.
 
Siku hizi polisi wanapiga simu hoteli uliyobook.
 
Reactions: Qj_
Kwa muda mfupi sana , tena bila hata ving'ora umefanya jambo la maana kuliko HATA KILICHOFANYWA NA AWAMU YA 5 TANGU IINGIE MADARAKANI , Mungu akubariki sana kwa moyo wako wa huruma kwa watanzania wenzako ambao taarifa za sasa zinasema kwamba wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku.
 
Afu hii timu ya mpira ndio nimekumbuka sasa, kuna ndugu yangu nadhini alipitia timu hii ya mpira maana na mwona na timu hii mara kapiga pictures nini! Now yupo Sweden anakomaa huwa anarudI bongo, kule ananiambia anapiga kazi za usafi barabarani na zingine. Ila na hisi inabidI uwe na pesa nzuri kuwapata hao wamiliki wa timu, maana jamaa yangu kwao wako njema. So naulI, visa lazima ujitegemee.
 
Kwa mfano kama nimeoa lakini nahitaji kupata kipotabo kama njia ya kwenda nje ili kupunguza michosho je naweza kufanyaje?Pia kama ni mchungaji unayetambulika ramsi unaweza kufanyeje?
 

Nimetumia mfano huo wa MSudan kwasababu kuna kijana wa kutoka Sudan ambae aliamua liwalo na liwe na akaingia ndani ya njia ya reli ya Channel Tunnel (kama sikosei) ili atembee na atokee pale Ash ambacho ni kijiji kilichopo maili tatu kutoka Dover.

Polisi walimsubiri na alitumia masaa zaidi ya 24 kuja kutoka lakini alikuwa tayari yupo ndani ya ardhi ya UK na akajisalimisha akajieleza na akakubaliwa maombi yake ya Ukimbizi hapohapo na akaelekea kwenye nyumba za muda.

Sasa huyu alikuwa ni msudan na wanajulikana hivyo haikuwa kazi ngumu kukaa na kusikiliza kesi yake.

Ila bado mfumo wa kupokea Asylum cases upo na ukipita hapo kwenye (Asylum claim) ndiyo baadae unaingia hatua ya kupewa hadhi ya ukimbizi na baadae mkazi ya kudumu.

Hatua ngumu ni hiyo ya kujilipua yaani asylum seeking ambayo huenda ukawekwa kizuizini (detention) au ukiwa na bahati unawekwa kwenye nyumba maalum wakati kesi yako inachunguzwa, hapo unakuwa unatakiwa kuwa unakwenda kusaini kila mwezi au kila wiki kwenye kituo cha uhamiaji kilichopo karibu.

Pia kwenye hatua hii ya kujilipua unakuwa huruhusiwi kufanya kazi na unakuwa uko kama kifungoni vile.

Kuna aina mbili za kukubaliwa kesi yako yaani unakuwa unapewa ukaazi wa kudumu uitwao "humanitarian protection" kwamba kwa huruma ya wewe kupatwa na maswahibu yalokukuta basi ni uamuzi wa busara kukulinda na kukusaidia kwa muda na hiyo unaweza kupewa miaka 3 au 5 ambayo baadae inaweza kuongezwa au unaweza kurudishwa kweu kutokana na hali ya nchi ulikotoka kuwa shwari. hii mara nyingi hupewa watoto walo chini ya miaka 18.

Aina ya pili ni ile iitwayo "Refugee Status" ambayo unaweza kupewa ya muda mfupi inayoweza kuangaliwa upya au ya muda mrefu ambayo hupelekea mkimbizi kuwa raia wa nchi hiyo.

Ukikubaliwa kesi yako ndiyo unapewa hadhi ya ukimbizi au refugee status na unakuwa unaruhusiwa kufanya kazi, kwenda shule na kadhalika ili uweze kuzoea zaidi mazingira ya nchi yako mpya.

Ila kama unavyosema kesi nyingi za ukimbizi zilikuwa kati ya 2000 hadi 2008 na baaada ya hapo zimekuwa ni ngumu sana kufanikiwa khasa kama hazitokei kwenye nchi kama Eritrea, Syria, na Sudan.

Ila bado waafrika wanakwenda na kujaribu si tu Marekani bali hata katika nchi kama Canada, Uingereza, Italy, Ujerumani, Sweden, Denmark na Holland.

Ukiondoa Uingereza nchi za Italy, Ujerumani, Sweden, Holland, Denmark wao wanataka uwe tayari kujifunza lugha zao ikiwa ni moja ya masharti ya kupewa uraia kabisa.
 
Scandinavia ndiyo mpango huko malta labda ramani zisisome kabisa....
Mkuu nakusanya data nikiamsha staki mtu wa kunishika mkono.

Ofisini umeaga lakn! !
Hakuna wa kumuaga pale ofisini zaidi ya kuniletea uchuro tu, nimemwaga mama angu ameshanitemea mate mkononi kama baraka ya safari yangu huko niendako nikafanikiwe.
 
Kwa mfano kama nimeoa lakini nahitaji kupata kipotabo kama njia ya kwenda nje ili kupunguza michosho je naweza kufanyaje?Pia kama ni mchungaji unayetambulika ramsi unaweza kufanyeje?

Katika kujaza fomu za maombi kuna sehemu wameuliza kama umeoa na una familia na una kazi ambayo ni ya kudumu.

Hiyo unafanya kama vile waenda vekesheni na huyo kipotabo utapata hukohuko ukiwa kwenye mgahawa au ukumbi wa starehe jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kiafrika yaani unaacha mke nyumbani halafu unakwenda vekesheni wewe mwenyewe ili kukidhi haja zako za kibaradhuli.

Kama wewe ni mchungaji (kama ni kweli) basi unatafuta haya makanisa yetu kama ya akina Gwajima na wao wana contacts nje wanaweza kukuombea kwenda kutoka semina na kama unatema kimombo vizuri basi inakuwa haina shida.
 
Ndugu usimsumbue bibi, elfu kumi yako tu pale utapata hiyo hati.
Jaman mimi mbona naona mambo magumu sana.ngoja kesho naenda uhamiaji ya bagamoyo.ila ujinga wao watakwambia wanataka barua ya mualiko
Na tiketi ya kwenda na kurudi hapo ndipo patamu.
 
Hakuna wa kumuaga pale ofisini zaidi ya kuniletea uchuro tu, nimemwaga mama angu ameshanitemea mate mkononi kama baraka ya safari yangu huko niendako nikafanikiwe.
Njoo basi inbox tuongee.

Kuna jamaa yupo korea. Alichukua mkopo ofisini kwake akapotea ila alipofika ikabidi ajirudi aombe msamaha akaulipa
 
Jaman mimi mbona naona mambo magumu sana.ngoja kesho naenda uhamiaji ya bagamoyo.ila ujinga wao watakwambia wanataka barua ya mualiko
Na tiketi ya kwenda na kurudi hapo ndipo patamu.

Barua ya mwaliko au offer ya chuo ndiyo msingi wa safari yako ya matembezi au kwenda masomoni.

Tiketi ya kwenda na kurudi (kwa matembezi) ni jambo la pili na la msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…