Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ni kweli Nordic kwa sasa ndiyo kuzuri.

lakini kwa angalizo ni kwamba inabidi huyo mchumba alieko kwenye nchi za Nordic awe amezoeana sana na mke/ mume mtarajiwa na huwa kwenye "initial stage" wanataka kuona mahusiano ya kweli.

Wanaweza kutaka kuona mkiwa mmetembelana kwa mfano mmoja kaenda Tanzania na mwingine Sweden lakini isiwe ni "one way ticket" hiyo inahesabiwa kuwa siyo "genuine relationship".
Ni kweli mkuu, lkn wengi wanaofunga ndoa tu waingiapo huko huwa haina usumbufu.... Ila kama unataka visa ya kwenda na anaekualika ni huyo mchumba huwa wanataka hizo mambo za genuine relationship but ukipata rafiki akakualika then ukajilopua na ndoa unaruhusiwa ku extend visa au kupewa ukaazi.....
 
Mimi nipo Stockholm kwa zaidi ya half decade ntaeleza badae Ni kwa njia gani waweza tumia but briefly Kuna timu ya mpira huku inaitwa Kilimanjaro ipo under Athuman Machupa Na Shekhan Rashid and co wanaweza kusaidia pia kuwaleta wabongo huku. lusungo

Mkuu habari za Stockholm.

Nimewahi kuja Sweden kwenye mji mmoja waitwa Sundsvaal, mji umetulia sana.
 
Alaf passport. Nilipoona masuala ya cheti cha kuzaliwa cha mzazi.hapo ndo nilichoka.sasa tunafanyaje kuipata.ya 50,000.ila naomba usiwe kama britanicca tu. 😀 😀 😀 😀 😀 😀
Britanica alikutenda nini? Mimi sihitaji pesa yoyote nakupa ramani tu...

Kuhusu cheti cha kuzaliwa cha mzazi kisikutishe... Pale uhamiaji hutoa hati za kiapo cha baba au mama, ukienda kuna wanasheria wanakusainia kwa elfu 10 tu ambapo utapatiwa affidavit then utaambatanisha. (muhimu uwe na taarifa kamili za baba au mama)
 
Vipi kwa nchi ya Italia..nataka nikachume zabibu kwa wataliano.....ila nasikia ni wabaguzi balaa

Katika nchi rahisi kupenya na kuingia Italy ni rahisi sana ila kuna tatizo la kazi.

Wataliano wengi na hata wageni ambao tayari wana passport za Italy huwa wanakimbilia Uingereza ambako zipo kazi hata za ufagizi na usafi ambazo wenyeji hawazitaki.

Wasichana wa kitaliano huwa wanafanya kazi za mahotelini na kwenye migahawa, hivyo ukiongea kitaliano unaweza kuoa binti wa kitaliano na mkaishi majuu.

Ndiyo utakuta waghana wengi wanafanya kazi hizo lakini wanazungumza kitaliano.

Kwa kifupi Italia pana pilikapilika nyingi kuhusu kutoka kwenda juu zaidi yaani UK na Germany.
 
Ni kweli mkuu, lkn wengi wanaofunga ndoa tu waingiapo huko huwa haina usumbufu.... Ila kama unataka visa ya kwenda na anaekualika ni huyo mchumba huwa wanataka hizo mambo za genuine relationship but ukipata rafiki akakualika then ukajilopua na ndoa unaruhusiwa ku extend visa au kupewa ukaazi.....
Sasa ukikosa mtu wa kuoa hapo inakuaje? Au wao wanapatikana kama njugu?
 
Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji. Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya,

Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.

Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda.
Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu,
Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao

HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.
Mkuu mimi natafuta nauli na pesa ya visa kuondoka rais mno.
 
Mimi nipo Stockholm kwa zaidi ya half decade ntaeleza badae Ni kwa njia gani waweza tumia but briefly Kuna timu ya mpira huku inaitwa Kilimanjaro ipo under Athuman Machupa Na Shekhan Rashid and co wanaweza kusaidia pia kuwaleta wabongo huku. lusungo
Kweli hata kwa vikundi vya ngoma... Izuri wa hizo nchi raia wake wana upendo na huheshimu sheria sana... Hizo nchi wakuja mnaheshimika kama wenyeji alimradi uwepo kihalali.
 
Niliona wengine huja kwa vikundi vya ngoma... Sweden... Denmark... Norway wanavipenda sana hivi vikundi so wengi huchomekwa humo....
 
Kweli hata kwa vikundi vya ngoma... Izuri wa hizo nchi raia wake wana upendo na huheshimu sheria sana... Hizo nchi wakuja mnaheshimika kama wenyeji alimradi uwepo kihalali.

Mkuu, tatizo moja tu la nchi za Nordic ni muda wa kujifunza lugha zao khasa Sweden na pia kazi ni shida kidogo ingawa zipo.

Inawezekana kupata kazi mara moja lakini huwa inasumbua.

Halafu pili, fedha ya Sweden ni mgogoro kwani ni ngumu sana na ukitumia mara moja inapotea.

Hivyo itakuwa jambo la busara ukipata fedha ya Sweden unaiwekeza mara moja TZ, bila kuchelewa.

Naomba ufafanuzi kwenye hili mkuu maana twanyooshana mawazo.
 
Mkuu, tatizo moja tu la nchi za Nordic ni muda wa kujifunza lugha zao khasa Sweden na pia kazi ni shida kidogo ingawa zipo.

Inawezekana kupata kazi mara moja lakini huwa inasumbua.

Halafu pili, fedha ya Sweden ni mgogoro kwani ni ngumu sana na ukitumia mara moja inapotea.

Naomba ufafanuzi kwenye hili mkuu maana twanyooshana mawazo.
Sweden hela yao sio ngumu.... Then kule unaweza lipwa hata usipofanya kazi.... Mradi uwe legal migrant... Mfano ukiwa unasoma unalipwa n.k

Kwenye lugha ni kweli kugumu... Na lugha yao ni ufunguo wa mambo mengi sana ikiwemo kazi... Ukijua lugha kazi unapata kirahisi mno...

Wenzetu hutumia lugha kama kigezo cha kujua mapenzi yako halisi kwa nchi yao......
 
Back
Top Bottom